Kwa nilivyo andika hapo ni kipi unakitilia mashaka? Huo ni ukweli 100% ingia hata kwa google utaona. Mashule yao ya umma ndio best school, yaani mtu akisoma shule ya serikali ndio anaonekana amepiga bingo kama ilivyokuwa kwetu miaka ya 1990 kurudi nyuma. Na hii imefanya watu wao walio wengi wapate Elimu nzuri sana kwani wengi wanasoma shule za serikali (za umma).Unaongelea Kenya ama Ulaya? Kama ni Kenya basi sio kweli
Unajua hata kihistoria baada ya uhuru wao hawajawafukuza wazungu kwa hiyo kama viwanda vyetu tuli viua vyote; vya kwao vyote vipo; KRA inakusanya kodi nyingi sana kutoka kwa hivyo viwanda; Hii ni pamoja na kuwa na kodi rafiki za kuwafanya wawekezaji na matajiri wakue zaidi Ili waweze zaidi na kuweza kuajiri zaidi.
Usidanganyike na watu ambao hawana takwimu!!!