Kwanini Kenya inapendwa na wazungu ilihali tumezidi vivutio?

Kwanini Kenya inapendwa na wazungu ilihali tumezidi vivutio?

Haijawahi kutokea watalii wakaipenda nchi ambayo serikali yake ina miliki vikundi vya wafiraji vilivyoundwa kuwashughilikia wakosoaji
Mkuu hujafatilia vzr historia

Kenya ndio kulikuwa na uuaji WA wakosoaji kuliko tz enzi za moi

Hata SASA umefatilia maandamano ya Gen z ?? Umefatilia ilegal abductions zinazoendelea huko??

Sisi hayo mambo yameanza kipindi cha mwendo zake..
 
Ukimuuliza mzungu what is your favourite country in East Africa anakujibu Kenya wakati ukiangalia sifa nzuri tumewazidi.tukiacha hali za kisiasa ila kuanzia vivutio na historia yetu ni ya kuvutia halafu wakenya makauzu makauzu Sana yaani hata wanavyoongea kwa Ku shout tofauti na Sisi tuko calm kwenye negotiations.. What's the extra about Kenya?
Utafiti wako umefanyia wapi na umetumia njia gani vinginevyo hizi porojo na hisia zako tu na pengine we ni mkenya unajaribu kuifanyia nchi yako promotion. We wazungu unakuwaga nao wapi, acha usenge hawa wanaomiminika kila siku Tanzania huwa huwaoni? Nenda kashinde pale KIA uje kutuambia kwa siku wanashuka wazungu wangapi. Bwege lisilo na haya! Umejilaza unatuandika huu uchafu? Pumbav!
 
Mkuu hata mimi sikuwahi na sitakaa niseme kufuata ujamaa ilikuwa ni kosa japo nitasema tungeweza kufanya modification zaidi. Kwa mfano kubadilisha mfumo wa elimu bila matayarisho kulitu-cost sana. Nemebahitika kufika nchi za Scandinavia, mfumo wao hauna tofauti sana na kile alichotaka kufanya mwalimu Nyerere.
Nchi za Scandinavia wanafuata mfumo wa social democracy, ni tofauti kabisa na alichokuwa anakifanyq Nyerere Tanzania.
 
Ukimuuliza mzungu what is your favourite country in East Africa anakujibu Kenya wakati ukiangalia sifa nzuri tumewazidi.tukiacha hali za kisiasa ila kuanzia vivutio na historia yetu ni ya kuvutia halafu wakenya makauzu makauzu Sana yaani hata wanavyoongea kwa Ku shout tofauti na Sisi tuko calm kwenye negotiations.. What's the extra about Kenya?
Nchi yetu hatujajitambua bado.

Tunachoweza sisi ni uchawa tu.
 
Wazungu wengi wanashukia Kenyata Airport Nairobi kwa sababu mwanzo KIA walikua na Tozo kubwa kuliko wenzetu ndio chanzo cha ndege nyingi kuukimbia uwanja wetu iliwafanya wageni wengi kushukia kule harafu tunawafata na shuttles/Coaster na kuwaleta Arusha ila kama wangeweka mazingira ya Tozo mazuri nadhani ndege nyingi zingeshukia hapa hapa KIA ingawaje sasa hivi KLM wameanza kutua hapo KIA.
Hayo ya zamani siyo sasa
 
upande wa Bara tumedumaa sana aisee ila safari za wakubwa ni nyingi hakuna kitu wanafanya kwenye Utalii..
Wanaenda safari kuto-mbana tu kwenye hoteli za kifahari huko nje, huo ndio kitu wanayofanya kwenye utalii nothing else, ukiitangaza Tanzania maana yake umeitangaza Zanzibar ukiitangaza Zanzibar maana yake umeitangaza Tanzania, trick hapa ni kuwavuta Zanzibar kisha kuwavuta Bara ila wengi wakienda Zanzibar hawataki kuja Bara na wakija Bara wengi wanakimbilia Zanzibar, promo za matangazo ya utalii Zanzibar ni tofauti na promo za utalii Bara sio kwamba Bara hakuna vivutio hapana kuna vivutio vingi vingi sana kuliko Zanzibar ila basi tu
 
Juzi Ruto kaipongeza Tanzania tumewapita tayari kwenye East Africa inter trade, kifupi sasa hivi East Africa Yote Tanzania ndio anaongoza kusuplly majirani,


Kuhusu Barabara pia tumewapita hizi nyuzi za zamani ila pitia

Hospitali pia tumewapita, wana Hospitali nzuri chache za wenye pesa ila Hospitali za wala la hoi Tanzania ipo juu ndio maana wakenya wengi huja Tanzania Kutibiwa...

Fanya homework yako vizuri
Acha ujinga wewe , mkenya gani anakuja Shithole country kutibiwa wewe jinga ,hivi mnatuona matako ya bibi zenu au sio ? , hizi takataka ambazo hata vidonge vya panadol hamna ? Au unazungumzia hospitali gani ? ,kwanza hospitali nyingi ziko chini ya taasisi za Roman Catholic na Lutheran ,hebu anza kuorodhesha hospital zilizojengwa na hawa vibakà wenu mnaowaita viongozi from scratch na utuonyesge efficiency yake hapa . Muwe na aibu kujisifia ujinga na upuuzi.
 
Utafiti wako umefanyia wapi na umetumia njia gani vinginevyo hizi porojo na hisia zako tu na pengine we ni mkenya unajaribu kuifanyia nchi yako promotion. We wazungu unakuwaga nao wapi, acha usenge hawa wanaomiminika kila siku Tanzania huwa huwaoni? Nenda kashinde pale KIA uje kutuambia kwa siku wanashuka wazungu wangapi. Bwege lisilo na haya! Umejilaza unatuandika huu uchafu? Pumbav!
Jamaa yangu wewe unaishi wapi? Kumiliki Smartphone haina maana kwamba unajua kila kitu watu wanateembea wanaona na pia kumiliki Smartphone haina maana wewe unamzidi kila mtu uelewa na utambuzi watu wanaona dunia haijajitenga Nchi yako sio kisiwa watu wanatembea wanaona wewe umejifungia hapo kwenu Bonyokwa ndio unajiona km umefika Japan au Uingereza au Canada kumbe upo Kimara tu hapo unapigwa na mavumbi
 
Kenya ni maarufu kuliko Tanzania Duniani. Sababu ni nyingi tu.

Chache
1. Post independence wageni hawakufukuzwa/hawakukimbia.
2. Lugha
3. Kufanya vizuri michezo kimataifa kumewafanya wajulikane zaidi. Mtu akiskia athletics kwa Africa taifa la kwanza Kenya
4. Wakenya wapo wengi nje ya nchi kuliko watanzania[sina data ila nadhani nipo sahihi] imesaidia pia.
5. Mrengo wa nchi toka wanapata uhuru walijitanabaisha na mataifa ya kimagharibi na hadi leo umeona Kenya akipiga kura UN ni tofauti na sisi. Haya mataifa ndiyo yenye wasafiri wengi.
6. Obama amewabeba pia.....Obama ni moja ya watu maarufu saana Duniani.
7. Makampuni mengi ya ndege kutua Jomo Kenyata....
Safiiiii...
Ubabaishaji siyo kama sisi..
Wako serious, more professional na makini...
Hata tubishe, uchumi wao mkubwa, even though we are catching up...
Ki Technology wako mbali, na ujinga ujinga wa kufungia mitandao hakuna, wakijuwa watapoteza hela nyingi sana...
Aina ya siasa yao, capitalism, hatushangai Ina mabilionea wengi kuliko sisi..
Elimu, tusibishe, wametuzidi kuanzia level ya chini mpaka juu!
......
 
Cha kwanza uwa ni Lugha.... Mzungu akienda Kenya haitaji kuwa na Mkalimani, kwa sababu lugha yao kwa asilimia kubwa ni kiingereza... Mzungu akitazama vyombo vya habari anapata taarifa kwa kiingereza, vile vile mabango ya barabarani ambapo Mzungu awezi kupotea kizembe hata akiwa amatembea kwa sababu vitu vingi vipo kwa kiingereza...

Ukija Tanzania, Wazungu wengi uwawia vigumu kuelewa lugha ya Kiswahili hivyo uwabidi kuajiri mtu kuwa mkalimani au kuwaelekeza baadhi ya mambo, vile vile taarifa zetu za habari na mabango uwa yapo kwa Kiswahili hivyo Mzungu awezi kujua nini kinaendelea katika nchi au eneo husika...
 
Wanaenda safari kuto-mbana tu kwenye hoteli za kifahari huko nje, huo ndio kitu wanayofanya kwenye utalii nothing else, ukiitangaza Tanzania maana yake umeitangaza Zanzibar ukiitangaza Zanzibar maana yake umeitangaza Tanzania, trick hapa ni kuwavuta Zanzibar kisha kuwavuta Bara ila wengi wakienda Zanzibar hawataki kuja Bara na wakija Bara wengi wanakimbilia Zanzibar, promo za matangazo ya utalii Zanzibar ni tofauti na promo za utalii Bara sio kwamba Bara hakuna vivutio hapana kuna vivutio vingi vingi sana kuliko Zanzibar ila basi tu
Kuna mgeni mmoja kaenda mara tatu Zanzibar baadae nikamwabia njoo na crater moja trip hii karudi tena crater kaenda Nyerere kamaliza na Zanzibar anashangaa huko Crater harafu tupo kimya kama vile hatuna kitu alitoka Valencia,Spain.
 
Wazungu wengi wanashukia Kenyata Airport Nairobi kwa sababu mwanzo KIA walikua na Tozo kubwa kuliko wenzetu ndio chanzo cha ndege nyingi kuukimbia uwanja wetu iliwafanya wageni wengi kushukia kule harafu tunawafata na shuttles/Coaster na kuwaleta Arusha ila kama wangeweka mazingira ya Tozo mazuri nadhani ndege nyingi zingeshukia hapa hapa KIA ingawaje sasa hivi KLM wameanza kutua hapo KIA.
kwanza wao waliamua kuanzia mwanzo kuwa capitalists na ndiyo mana wameendelea faster kuliko sisi. Sisi mpaka leo hii hatujijui tuko kivipi.

Kutokana na sera zao wao wamekuwa na marketing skills kubwa wakati sisi tumelala, na ndiyo mana hata mlima Kilimanjaro waliutangazia kuwa ni wao, na wazungu wengi wakitambua hivyo mpaka hivi karibuni.

Vile vya kupewa bure bure pale baada ya uhuru (elimu, afya ....) vilitulemaza sana Watanzania, tulijisahau kabisa kuwa lile lilikuwa na jukumu la wazazi. Baada ya kushituliwa na IMF tulilalamika sana na mpaka hii leo hatujakaa sawa kielimu. Sisemi kuwa ni kitu kibaya na baadhi yetu tulifaidika na huo mfumo lakini ukweli ni kwamba ulitulaza usingizi mnono wa kusubiri vya bure.

Baada ya kuvunjia Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, fedha zetu zilikuwa sawa: 1 British Pound = 20 Shillings, 1 US dollar = 7 shillings. Angalia tafauti kwa sasa ni mara ishirini kwa sababu ya sera zetu za ujamaa.
 
Juzi Ruto kaipongeza Tanzania tumewapita tayari kwenye East Africa inter trade, kifupi sasa hivi East Africa Yote Tanzania ndio anaongoza kusuplly majirani,
Ungejua anachofanya wala usingeipa hype hio kitu
 
kwanza wao waliamua kuanzia mwanzo kuwa capitalists na ndiyo mana wameendelea faster kuliko sisi. Sisi mpaka leo hii hatujijui tuko kivipi.

Kutokana na sera zao wao wamekuwa na marketing skills kubwa wakati sisi tumelala, na ndiyo mana hata mlima Kilimanjaro waliutangazia kuwa ni wao, na wazungu wengi wakitambua hivyo mpaka hivi karibuni.

Vile vya kupewa bure bure pale baada ya uhuru (elimu, afya ....) vilitulemaza sana Watanzania, tulijisahau kabisa kuwa lile lilikuwa na jukumu la wazazi. Baada ya kushituliwa na IMF tulilalamika sana na mpaka hii leo hatujakaa sawa kielimu. Sisemi kuwa ni kitu kibaya na baadhi yetu tulifaidika na huo mfumo lakini ukweli ni kwamba ulitulaza usingizi mnono wa kusubiri vya bure.

Baada ya kuvunjia Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, fedha zetu zilikuwa sawa: 1 British Pound = 20 Shillings, 1 US dollar = 7 shillings. Angalia tafauti kwa sasa ni mara ishirini kwa sababu ya sera zetu za ujamaa.
Mkenya anakuja kuchukua kitunguu Manyara anaweka kwenye box huko kwao anaenda kuuza nje sisi vitu vingine vinaozea shambani kwa kukosa usafiri hayo magari ya kusafirisha bidhaa kodi zake bora ufanye shughuli ingine tu angalia hata usafiri bus bora lenye body ya Iriza kodi yake ni kubwa mno tupo tunajificha na mchina gari ikipata ajali kidogo tu lazima watu wafe haina Kinga kwa abiria wake viti vipo karibu karibu balaa..
 
Back
Top Bottom