Hahaha mipango ya CCM. Kama mmemsikiliza MSigwa anasema, Magufuli alikuwa anamshauri sana ahame Chadema aende CCM lakini akamwambia nitakusaidia nikiwa huku(CHADEMA). Kuna kitu alikuwa kaagizwa kufanya, hakuweza kukipata.
Alitaka nafasi ya juu ili akihama awe gumzo, CHADEMA walimuelewa mapema, wakaamua kumuweka anapostahili, ili akiondoka, asiwe na impact yoyote, na sasa ndipo alipo.
Mbowe ni mwiba kwa CCM, wao walitaka vyama vinavyowekwa mifukoni mwao(CCM). Lakini CHADEMA imekuwa tofauti, imekuwa kama mende, ukimuua kwa kumsigina, umemsaidia kueneza mayai na watazaliwa wengi zaidi.
Demokrasia gani wanayoitaka, Kule CCM Magufuli alimfukuza SOFIA SIMBA, na Benard MEMBE kwa kutofautia naye siyo chama, na ilionekana sawa.
Huku wanaoondoka wanakuwa Ma agent wanaotaka kufanikiwa lakini wanakosea, wanaondoka chama kinaerndelea kustawi, ni kama magamba ya nyoka, yanapotoka ndio nyoka anapendeza.
Binafsi naona waondoke tu, na ikiwa wanataka Mbowe aondoke, basi watafute njia nyingine hii ya kumtuhumu iliishashindwa.