Kwanini kila anayeondoka CHADEMA anamtaja Mbowe?

Mwembe wa babu ulikuwa na mawe mengi chini yake kuliko idadi ya maembe mtini mwisho wa msimu
 
Huwezi kuwa mwenyekiti wa chama for 30yrs wenye akili wakakaa kimya kukuangalia tu. Ni wapumbavu tu watashangilia huu ujinga. Amekuwa Ayatollah?
Kwani Katiba inasemaje?Hili ni jambo ambalo linalindwa na katiba
 
Namshauri Mbowe ang'atuke kwa heshima.
asidhani bila yeye chadema haiendi.wapo viongozi wenye uwezo zaidi kuliko anavyo fikiria.

ailikiuza Chama mwaka 2015 tukampoteza Dr. SLAA.
amekihodhi chama kama mali yake.
 
Kazi kwelikweli
 
Mudi wamefuta huu uzi...
 

Attachments

  • Screenshot_20240822-111806.jpg
    349.9 KB · Views: 4
Sasa kama wameondoka CDM si wafurahie uwepo wa Mh. Mbowe sababu anaivunja? Mbona wanaweweseka kila siku? Mwamba is there to stay. Pole zao sababu kazi wanazopewa ni ngumu
 
Waliingia Chadema kwa mkakati wa wa kukiua chama sasa baada ya kuona Mwamba umekuwa mgumu lazima warudi waliko toka wakiwa na sura za mtj alie jipaka mavi usoni na kulalamikia Mwamba. Yaani Mbowe ni mwamba wa siasa. Hata Ccm hawa lali kwa kupambana na Chadema
 
Freeman Mbowe amekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa muda mrefu, jambo ambalo linaweza kuwa na madhara kadhaa, kama vile:

1. Kukosa Uvumbuzi na Mawazo Mapya:
- Uongozi wa muda mrefu wa kiongozi mmoja unaweza kuzuia kuingia kwa mawazo na mikakati mipya ndani ya chama. Hii inaweza kusababisha chama kuwa na mtazamo wa kizamani au kupoteza ubunifu katika kukabiliana na changamoto za kisiasa.

2. Migawanyiko ya Ndani ya Chama:
- Uongozi wa muda mrefu unaweza kusababisha kutokuwepo kwa fursa za uongozi kwa wanachama wapya au vijana, hali ambayo inaweza kusababisha migawanyiko au migogoro ya ndani, huku baadhi ya wanachama wakihisi kutengwa au kukosa nafasi za kuongoza.

3. Kufifisha Nguvu za Upinzani:
- Kwa kuwa kiongozi wa chama kwa muda mrefu, Mbowe anaweza kuwa amechoka kisiasa au kukosa msukumo wa kutosha wa kupambana na chama tawala (CCM). Hii inaweza kupunguza nguvu za upinzani na uwezo wa CHADEMA kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania.

4. Kuonekana Kama Chama Kinachomtegemea Kiongozi Mmoja:
- Uwepo wa Mbowe kwa muda mrefu kama Mwenyekiti unaweza kufanya chama kuonekana kuwa kinamtegemea sana yeye, hali ambayo inaweza kuathiri taswira ya chama kuwa ni taasisi inayoweza kuendeshwa bila kiongozi mmoja maalum.

5. Kukosa Kuwavutia Vijana:
- Vijana wanaweza kuona chama kama kinachoendeshwa na kizazi kilichopita, na hivyo kukosa mvuto kwa wapiga kura vijana ambao ni muhimu kwa mustakabali wa chama chochote cha kisiasa.

6. Uaminifu Usio na Changamoto:
- Uongozi wa muda mrefu unaweza kusababisha utamaduni wa kutomchallange kiongozi ndani ya chama, jambo ambalo linaweza kupunguza uwajibikaji na kuzuia maamuzi mazuri.

7. Kuzuia Kukua kwa Uongozi wa Mbadala:
- Uwepo wa kiongozi mmoja kwa muda mrefu unaweza kuzuia au kupunguza nafasi kwa viongozi wapya kujifunza na kujitokeza ndani ya chama, hali inayoweza kudhoofisha uimara wa chama katika siku zijazo.
 
Mkapa = Mbowe
JK = Mbowe
JPM = Mbowe
Samia = Mbowe
Bob Makani alirithi chama kwa Edwin Mtei, Makani kaoa dada wa Mtei(SHEMEJI). Freeman Mbowe karithi kwa Makani, Mbowe kaoa mtoto wa Mtei (mkwe). Hicho ni chama cha FAMILIA, mkitaka Mbowe atoke anzisheni chama chenu
 
Mbona mimi nimeondoka CDM mwaka 2015 sababu kubwa ilikuwa Lowassa.
 
Chama Saccos ya Mtei,
Hata nyumba ya Chadema makao makuu Mikocheni ni ya dadaake Mbowe Grace.
Nyie mnalipa kodi tu .
Ndio mana mwenyekiti anawadai hela nyingi sana.
Mkipigwa mpigike.
Mi sio mfuasi wa chama chochote
 
Ni masharti ambayo yako kwenye mkataba wa kununuliwa kwao .
 
Ni masharti ambayo yako kwenye mkataba wa kununuliwa kwao .
 
Mbowe kwa kweli ni wakati sasa ku step aside na aruhusu Mabadiliko, Changes ni nzuri na Huleta mambo Mapya na Positive zaidi, Tunaheshimu sana Upambanaji na Mafanikio makubwa aliyoyaleta Freeman Mbowe ila sasa ni wakati Wa yeye kuruhusu Mtu mwingine kuhuduma kwenye hio nafasi ya Juu kabisa sisi wengine tunawaza mpaka kuwa hichi chama mbona ni kama Genge la wahuni tu kaskazini mana hata Mnyika na Lissu ku operate kwao ni shida sana basi kwa vile Lissu ni Mbishi na ana Fan base yake Kubwa
Wazungu wanasema, A good dancer must know when to leave the stage
 
Kingine ulichosahau kuuliza ni hiki, kwanini hawa unaowasema wakiondoka Chadema huko waendako wanapewa vyeo, na kuwapiku wanaccm wa miaka mingi wafia chama?

Ukiunganisha hoja hizi mbili tunaweza kupata jibu kirahisi sana
Wanapewa vyeo Kwakuwa wanauwezo
 
Kingine ulichosahau kuuliza ni hiki, kwanini hawa unaowasema wakiondoka Chadema huko waendako wanapewa vyeo, na kuwapiku wanaccm wa miaka mingi wafia chama?

Ukiunganisha hoja hizi mbili tunaweza kupata jibu kirahisi sana
Wanapewa vyeo Kwakuwa wanauwezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…