Huheshimiki kwa sababu wewe binafsi unashindwa kuwaheshimu wenzako hapo juu nimekuuliza wapi Pope alisema anaunga mkono ushoga hujanijibu.
Ndani ya Kanisa Catholic ipo wazi linajua waumini wake ni watenda dhambi za aina mbali mbali so halioni haja ya kukemea dhambi fulani na kuacha dhambi fulani sababu zote ni dhambi na zinachukuliwa kwa uzito ule ule wewe unadhani unapoingia msikitini huingii na mashoga?huingii na wafiraji?huingii na wezi sasa kwanini kutolewa tahadhari tu kwa wezi na wazinzi wafiraji na wafirwaji wanaachwa it means wanayoyafanya ni mazuri kwa mujibu wa imani yako?
Papa kama kiongozi aliapa kuwa mjumbe wa Mungu so anao wajibu wa kusema yaliyo mema na yaliyo mazuri alimradi watu wote wavuke salama,America kama taifa inatambua ushoga ndani ya katiba yao na ndani ya Marekan kuna waumini wakatoliki ndani ya hao kuna wafiraji na wafirwaji wapo pia wasiokuwa waumini wana tabia hiyo hao nao wanapaswa kuambiwa kwa unyenyekevu kwamba japokuwa sheria za nchi zao wanazoona zinawalinda na kuwafariji wajue ipo dhambi kubwa wanayoitenda na wa kusema hayo siyo mwengine ni papa,sheikh au mchungaji kama hawajasema hayo hao nao hawafai kuwa wajumbe wa Mungu kwa sababu yale yaliyo maovu hawayakemei na huo ni unafiki.