Kwanini kila wanapokwenda viongozi wakuu wa nchi Rostam anatangulia kufika?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kila eneo tunapotegemea kwenda kitaifa kufanya majadiliano ya kiuchumi Rostam anakuwa mstari wa mbele. Je, hakuna wafanyabiashara wengine wanaoweza kupewa hizi fursa? Nini faida ya huyu bwana kutangulia kwenye mataifa anayokwenda mkuu wa nchi kiuchumi?

Anakwenda kutangaza biashara binafsi kwa nembo ya Taifa au anabeba biashara za Tanzania? Wapo wapi wakina bakharesa kwenye hizi deals?
 
Rostam sio size yako

wakati wa Jk kwny Ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama alijipenyeza hadi moja ya matukio lilikuwa ni Obama kuzindua mitambo yake ya Symbion ambayo aliibadilisha kutoka Dowans hadi symbion na kuanzia hapo Wapinga ile mitambo wakaufyata milele

Rostam ndio alimuamuru Benjamin Mkapa atoe yale mabilion ya EPA

wakati wa JPM, Rostam ndio mtu pekee alikaribishwa Ikulu na picha zika trend anakunywa Chai na Rais Ikulu

huyu Mtu ni zaid hatare
 
Anasafisha njia atakuwa ni TISS🤣🤣🤣🤣💺
 
Mfalme Rostam Aziz

Hivi karibuni atakuwa Kenya kwenye ziara ya King Charles wa UK ambaye ndiye mkuu wa Anglo Catholic Church duniani
 
Ulisikia wapi dereva anakaa siti za nyuma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…