Kwanini Kiporo cha Wali Maharagwe Yaliyo na Nazi ni Kitamu Zaidi ya Chakula Hicho Hicho Kikiwa Fresh from Kitchen

Ila hili nchi ina watu wa hovyo saaanaaa,,,,!!!
Kwa nini msomi mbona mambo ya kawaida tu. Hayo ndiyo maisha yetu , tukianza kufikilia kufika mwezi ni lini bora tupige story za mambo marahisi
 
Jaman jaman 😋😋😋😋sitii neno kwenye hili
 
Kukiwa na msiba au sherehe walikuwa wanakuja kuazima masufuria makubwa mawili,hapo tunamwambia Bi Mdashi sufuria moja lazima lirudi na ukoko,sasa wakirudisha unakuta moja lina ukoko wa pilau/wali,hapo Bi Mdashi anaweka maji ya moto kidogo halafu anatuambia tuiache hadi kesho asubuhi.Sasa tulivyokuwa tunawahi asubuhi kuamka na kufanya usafi hadi chai tunachemsha wenyewe.Sasa dogo yeye alikuwa mzee wa chai,yaani yeye kunywa hata vikombe vi5 kwake poa tu.Hapo kiporo kinakwanguliwa na kuwekwa kwenye sufuria ndogo humo ni mixer na maharage,wanapakua chao halafu mim na dogo tunaachiwa sufuria.Aisee tulikuwa tuna-enjoy sana ila tatizo la dogo lilikuwa ni spidi tu..Kiporo kisikie tu
 
Sasa hapo kwenye hicho kiporo ongeza na kiporo cha kisamvu cha nazi...taste yake haina mfanowe..
 
Hata ugali uliosongwa kwenye chungu na maharage yaliyopikwa kwenye chungu yakawekwa karanga zilizokaangwa na kusiginwa, mtamu sana.
 
I see kwa ushuhuda huu,Wabongo wengi tunakula vipori, Tukiendelea hivi Ccm itatawala Milele.#Tusiwalishe watoto viporo hatakama ni vitamu,Kula mwenyewe #
 
Ndugu kiporo hiki (wali +harage nazi) ...dah hatari sana!!!!
Kiukweli bila kupepesa macho ni kitamu sana!
 
Na ndugu yake choroko ni tamu hasa zinapokua zimepoa kabisa.
 
Ni hatari moja na nusu aisee. Ukila lazima ulewe, kuna kausingizi flani hivi lazima ukapate. 😴😴😴
 
Siyo kiporo cha wali nazi na maharagwe pekee kuongezeka thamani kikiwa kiporo.

Onja pia maziwa yaliyolala na kuganda utofautishe na maziwa fresh, onja kiporo kisichochenshwa cha wali na kisamvu cha tui la karanga ya kutosha, onja kiporo baridi cha ugali wa sembe nyeupe na mboga ya mlenda wenye tui jingi nk nk, maana vipo vyakula vingi ni vitamu vikiwa viporo.

Wataalamu wa afya wanashauri kiporo kiliwe bila ya kuchemshwa kwa afya.

Ndani ya kiporo kuna bacteria wanaosaidia mmeng'enyo wa chakula, ukichemsha unaua hao bacteria rafiki wa mazingira ya tumboni.
 
Ngoja tukamuulize Dr. Janabi
 
Watu wa Dar bhana!! Yaani unasifia wali maharage ya nazi!!🤣🤣
 
Kuna vyakula vingi ambavyo huwa vitamu zaidi vikipoa/vikilala. Baadhi ni kisamvu na Sphaghetti. Bila shaka ni kazi ya bakteria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…