Kwanini kujenga nyumba imekuwa ni fashion kwa Watanzania?

Kama ambavyo wewe unaamini una akili timamu ya kung’amua na kuwashangaa wanaojenga na wao wanakushangaa unachowaza! Kikubwa kila mtu afanye kinachompa furaha.

Yaani we uaamini kodi ya nyumba miaka 15 ni ndogo kuliko kujenga na kukaa kwako freely?!
 
maisha ni kuchagua. uchaguzi wa mwingine hauwezi ukafanana na wako. kila mtu anajua tafsiri ya maisha kivyake.
 
Hujamuelewa mleta uzi hatakataa kujenga ila jenga ukiwa ushazungusha hela yako mara kadhaa yaani kama una biashara tayari ushazungusha faida hata mara kumi ndo uanze kujenga ili kukuza mtaji.
Acha ajenge kwanza ndo akakusanye za kuzungusha. Hela ina kasumba. Unaenda kuizungushia kwenye biashara, biashara zinasuasua TRA WANAKUJA KUKUNG’OA, mara ulikopa uendeleze
Basi na Yono nao wamefika. Unajikuta hela yote imepotelea kwenye β€˜kukuza biashara’.

Acheni watu wajenge kwanza ndo wakakuze hizo biashara hata wakikwama wana uwezo wa kupangisha alipojenga, akaenda kupanga chumba anachomudu huku anakula kodi na anaendelea kupambana.

It’s just an act of
Thinking outside of the box!
 
Tatizo hizo m 20 huwezi kuzikamata kwa mara moja ila kujenga unakuwa unapata kidogo unaweka kwenye ujenzi
 
Nakuunga mkono. Kuna watu hadi wanaacha kula vizuri kisa wanajenga.
 
Mkuu uko sahihi 100%.
 
Nyumba ni asset pia na wengi wana ndoto za kuishi kwenye nyumba zao kuepuka usumbufu wa kodi masharti ya wenye nyumba zao
Masharti ya kufagia na usafi mwengine wakati mnakaa na watu wachafu sana
 
Hapana. Ana future na ana mawazo mazuri. Na ana taarifa fulani za dunia ya pili na ya kwanza, lakini yupo dunia ya tatu.
Tip yangu kwake akiweza kukwepa viunzi vya dunia ya tatu basi atafika mbali.
Fundi seremala mfano anatakiwa afikirie kuwa na workshop na maduka ya furniture na awe kampuni, akope bank KWA TIJA ya kupanua biashara hata ktk majiji matatu Dar,Arusha na Mwanza. Ajenge au apange nyumba kwa jina la kampuni ili awe anapunguza kodi kama matumizi.
Ajilipe mshahara na watu wake nao ukawekwe katika sehemu ya matumizi ya kampuni.
Humo akizeeka anaifanya kuwa family business, watoto kama wana akili wanazeeka na hela, ajira wanapata humo humo na kuacha kutoa jasho kwa hawa less than 30% (Asians,Arabs na Indians), mnaukwepa "ukoloni-fala" wa Baba alifanya kwa Mo/Bakhressa mtoto nae humo n.k WATUMWA KIUKOO[emoji38].
Bibi NSSF,mpaka mjukuu nae afanye NSSF!!!
Unaajiriwa mpaka unafikisha miaka 60-65 ni upumbavu[emoji1549][emoji1549]Basi tu.
 
Point yake hamjaielewa wakuu, ni point ya kuandaa income streams mkuu, japo hajapata miongozo mizuri.Nchi yetu ilivyo kujenga ni muhimu sana kwa sababu biashara zetu zina mambo mengi na unaweza didimizwa any time.
Ila kwa mawazo yake ya mfanano wa dunia ya kwanza na ya pili kiuchumi yuko sawa.
 
[emoji38][emoji38]Kuna raia wamekuja na jazba kwa jamaa, ni opinion badala ya kumtukana mlitakiwa kumuonyesha ugumu uliopo katika mifumo yetu ya kiuchumi, mfano katika suala la nyumba hatuna mfumo mzuri wa kupata nyumba nafuu za kununua na kulipa taratibu kutokana na kipato chako. Inabidi ujenge taratibu kwa hatua.
Sasa labda ana alternative ya hilo, angeulizwa. Anyway ni jamii forums, ni online watu wanakuwa na tabia tofauti na wakiwa live, mtu huyu huyu hamtukani rafiki yake wakiwa sehemu akatoa kauli kama hizi, ila wanajadiliana fresh tu.
 
Mleta mada anadhani Mtanzania huwa anajenga akiwa na mpunga wote kuanzia msingi hadi finishing ili huo mpunga badala ya kujengea auingize kwenye biashara wapo wenye uwezo huo ila ni wachache

Iko hivi wengi tunajenga kwa kuungaunga vipato. Hivyo kusema mtu angewekeza kwenye biashara ni ngumu sana maana hela ilikuwa ya danadana

Kwa mfano mtu anaweza akawa na nyumba ya thamani tufanye tu 30 mln wewe mpita njia unaweza kusema huyu jamaa aliiipataje hii milioni 30 akajenga mbona inaonekana ana maisha ya kawaida sana. Kumbe yeye mwenyewe alijenga kwa kuungaunga mpaka imefika hapo.

Na ndio maana Watanzania wengi huwa hatujui exactly thamani za nyumba zetu
 
Mmekuja na mihemko lakini point yangu ya msingi ilikuwa ni kwamba kwanini watu wanawaza kuanza kujenga kabla hawajamiliki uchumi mkubwa
Hauwwzi ukaeleweka. Wangekuelewa kama ulivyokusudia ningeshangaa sana
 
Unazidiwa akili na Hawa ndege πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 

Attachments

  • images.jpeg
    30.3 KB · Views: 8
  • images (1).jpeg
    8.3 KB · Views: 9
  • images (2).jpeg
    11.5 KB · Views: 9
Kama unaweza kujenga nyumba jenga, tena sio moja tu. Hutajuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna muda kujenga ni hasara sana, bora ukafanya mambo ya msingi kwanza ila kama kujenga ni swala la msingi kwa mtu basi na alifanye tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…