Kwanini kusiwe na sheria ya mtu kuchagua dini/dhehebu akifikisha miaka 18?

Huu sasa ni ujinga wa kiwango cha reli. Nani kakukataza kuwa ukifikisha huo umri usibadili?
 
Huna akili ,basi asipelekwe shule mpaka afikishe miaka 18 ili aweze kuchagu kusoma au kutokusoma?
Basi asitahiliwe mpaka 18 ili achague kati ya kutahiriwa na kukaa na govi.

Basi asifundishwe lugha yeyote maana akikuwa anaweza kupenda lugha nyingine tofauti na mliyo mfundisha utotoni.
Basi asihesabiwe kama raia wa Tz mpaka afikishe miaka 18 maana akikua anaweza asiipende Tz akachagua kuwa raia wa nchi nyingine.
Ww unapo zaliwa ni mali ya wazazi na jamii iliyo kuzunguka na ndio maana huwezi kutambulika bila ubini wa baba yako.
 
Kwasababu Imani ni lifed experience, uhuru wa kuchagua Dini unao ila most of the times kama msingi waliokujengea wazazi wako unafanya kazi kwanini utapetape?
 
Muda mwingine sijui huwa mnawaza nini? Kwahiyo huyo mtoto hata shule asipelekwe mpaka atakapofikisha miaka 18 ndio achague asome au asisome? Mbona mbona siasa watoto wanafundishwa wakiwa wadogo? Mbona kuna watoto wanarithishwa ushabiki wa simba na yanga mpaka majez wanunuliwa? Iweje kwenye imani unasema aje afundishwe akiwa na miaka 18? Yaani miaka 18 ndio aanze kujua uzinzi ni dhambi, kuwa na kiburi ni dhambi, kumdhulumu mwenzako ni dhambi? Ni kizazi cha aina gani unataka kukitengeneza
 
Mimi nyumbani ni Roman wote lakini Mimi niliamua kuichagua pentekoste
 
Wapi umekatazwa wakati unajishtukia,hata ukiwa na miaka 5 unaweza kuchagua.
 
Kuchaguliwa mke kuchaguliwa dini kuchaguliwa rais nk siyo tatizo tstizo ni kulazimishwa dini kulazimishwa rais kulazimishwa mke ...mtu akikuchagulia kitu ,unayo hiali ya kukataa ila anaye kulazimisha anajaribu kuondoa hiali yako ya kuchagua
 
Mbona ukishakuwa mtu mzima hakuna anayekulazimisha uwe muumini wa dini Fulani au wewe mwenzetu umelazimishwa
 
Ikiwa hivyo,
Dini zote zitakosa waumini,
Ni ngumu Sana kumhubiria mtu mwenye akili na uwezo wa kuhoji
🤣🤣 Dini bila kuianzia utotoni ngumu Sana kumshawishi mtu na mavuzi yake
 
Atachaguaje kitu asichokijua? labda ungesema apelekwe dini zote kabla hajafikisha miaka 18 ndio aje achague itakayomfaa au aachane nazo zote
Atapelekwa vipi dini zote kabla ya 18 🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…