Kwanini kusiwe na sheria ya mtu kuchagua dini/dhehebu akifikisha miaka 18?

Kunielewa mtu mwenye akili kiduchu kama wewe ni ngumu sana,wapi nimeongelea kubadili dini kama siyo kukurupuka??
Wanachosema unapokuwa mtoto unakuwa hauna maamuzi yako mwenyewe mambo mengi wanakuamulia wazazi ikiwemo na hilo la dini, kwahiyo hoja ni kwamba kwanini wewe unaona dini tu ndio inatakiwa mtoto aachwe hadi afikishie miaka 18 aje kuamua mwenyewe wakati kuna mambo mengine pia aliyoamuliwa na wazazi kabla ya kufikisha hiyo miaka 18 aje kuchagua mwenyewe?
 
Kwanini unataka kuruhusiwa wakati hujakatazwa?

Wewe hapo ukiamua kubadili dini yako kuna sheria inakuzuia?
Swala lake ni kwamba kabla ya miaka 18 awepo tu yaani asilazimishwe kuabudu popote na akifika umri huu wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ndio aamue anaenda dini gani.
 
Habarini,
Kumekuwa na mgongano wa maslahi karibu kwenye kila famila ya kiafrika pale linapokuja swala la wazazi kuanza kumpeleka mtoto mdogo kuabudu dini fulani wakati mtoto hajui lolote na baadae anafuata na kukubali asichokijua bali alichoaminishwa tangu utoto.

Kama mambo mengi ikiwemo ajira,nida,kuoa,ubunge,nk yanafanyika baada ya mtu kufikisha miaka 18 basi na kuabudu pia kuwekewe sheria hiyo ili mtu aabidu anachokijua baada ya kuwa mtu mzima.

Nawasilisha!!
Huenda dini ingekuwa kama siasa
 
Wanachosema unapokuwa mtoto unakuwa hauna maamuzi yako mwenyewe mambo mengi wanakuamulia wazazi ikiwemo na hilo la dini, kwahiyo hoja ni kwamba kwanini wewe unaona dini tu ndio inatakiwa mtoto aachwe hadi afikishie miaka 18 aje kuamua mwenyewe wakati kuna mambo mengine pia aliyoamuliwa na wazazi kabla ya kufikisha hiyo miaka 18 aje kuchagua mwenyewe?
Hayo mengine utaandika uzi wako mie nimeona hili la dini
 
Huko kuamua kuona hilo la dini tu na kuacha hayo mengine wakati yote yapo kwenye kapu moja ndio hufanya hoja yako kukosa mashiko.
Hayo mengine yalete wewe kwanini unanielekeza kitu cha kuandika siuandike wewe hayo
 
Mimi natoa maoni humu, kwani wewe ulichoandika unaelekeza wazazi cha kufanya kwa watoto wao?
Unatoa maoni humu kwahiyo mimi nimetoa matako yako siyo maoni eti?

Uandishi una aina nyingi yaweza kuwa kwa maswali,kejeli,nyimbo,ngonjera,nk we vp?
 
Sasa mtu mwenye miaka 18 umletee kwa mara ya kwanza story za nyoka anaeongea, bikira anazaa si atajua unamdanganya.

Msingi wa dini ni kumfanyia muumini brain programming, na ni rahisi zaidi kumfanyia hivyo mtoto kuliko mtu mzima.

Hata hivyo mamlaka haziwezi kufanya unachosema kwa sababu zinahitaji hizo dini ili kutengeneza wanyonge wanaobagazwa kirahisi
 
Kwahiyo mkuu hii mada yako kuileta humu ulikuwa unategemea watu wachangie vp? Maana watu wamekupinga kwa kukuonyesha udhaifu wa hoja yako na inaonyesha hukutegemea hilo.

Siku nyengine ukileta mada humu uweke na maelezo basi kuwaelekeza watu wachangie vp vile unavyotaka wewe.
 
Sasa mtu mwenye miaka 18 umletee kwa mara ya kwanza story za nyoka anaeongea, bikira anazaa si atajua unamdanganya.

Msingi wa dini ni kumfanyia muumini brain programming, na ni rahisi zaidi kumfanyia hivyo mtoto kuliko mtu mzima.

Hata hivyo mamlaka haziwezi kufanya unachosema kwa sababu zinahitaji hizo dini ili kutengeneza wanyonge wanaobagazwa kirahisi
Hiyo hoja sio kweli mkuu maana mbona hata sasa watu ambao wamelelewa kwenye familia sizizoamini dini ila wamekuja kuamini dini ukubwani kwao, hata sasa mbali na story za dini watu wazima bado wanaamini sana story za kusadikika.

Shida ni kwamba mmechagua kuona dini tu katika mambo mengi ambayo mtoto hufundishwa na kufanyiwa.
 
Swala lake ni kwamba kabla ya miaka 18 awepo tu yaani asilazimishwe kuabudu popote na akifika umri huu wa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ndio aamue anaenda dini gani.
Hata akifika huo umri asilimia kubwa wengi wataishia kuchagua dini ambazo ndio zimeenea sana kwenye jamii yake tu, kama hapa Tanzania watoto wanakuwa wakiziona sana dini mbili ukristo na uislamu ndio zimeenea. Hivyo mwisho wa siku mie sioni mantiki ya hii hoja maana naona ni yaleyale tu ni sawa kubadili chupa mvinyo uleule.
 
Habarini,
Kumekuwa na mgongano wa maslahi karibu kwenye kila famila ya kiafrika pale linapokuja swala la wazazi kuanza kumpeleka mtoto mdogo kuabudu dini fulani wakati mtoto hajui lolote na baadae anafuata na kukubali asichokijua bali alichoaminishwa tangu utoto.

Kama mambo mengi ikiwemo ajira,nida,kuoa,ubunge,nk yanafanyika baada ya mtu kufikisha miaka 18 basi na kuabudu pia kuwekewe sheria hiyo ili mtu aabidu anachokijua baada ya kuwa mtu mzima.

Nawasilisha!!
Kwani ukifika umri huo nani amekulazimisha ufuate dini yoyote. Kama bado uko unakula kwa wazazi fuata sheria yao mpaka utakapoondoka hapo nyumbani uende bila dini au kufuata yoyote urakayoipenda
 
Back
Top Bottom