Kwanini kusiwe na sheria ya mtu kuchagua dini/dhehebu akifikisha miaka 18?

Kwa sheria hiyo, ile dini ya kishetani itakosa waumini
 
Watu mbona wanabadili dini na wengine wanaingia kuamini dini ukubwani.
Kuna dini zinasema mtu akiacha dini yake basi akatwe kichwa au apigwe mawe hadi afe, 🤣🤣 hapo unaonaje mkuu
 
Mzazi anapaswa kumlea mtoto katika njia impasayo....

Mithali 22
6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
 
kwani umekatazwa na nani? Si uende Rita ukabadilishe rasmi dini unayoitaka - Christian, Muslim, Hindu, Bahai, Buddhist..... utapokelewa tu pale utakapoelekea
 

NI wewe tu hujaamua kubadili imani yako lakini kwa mujibu wa katiba imeweka wazi uhuru wa kuabudu na mtu kuchagua imani aitakayo...

Hakuna sheria inayomfunga mtu kuendelea na imani aliyoikuta toka kwa wazazi...
 
Unaeza ukatoa tofauti ya Chama na Dini?
"Chama ni kundi la watu wanaoungana kwa kusudi la kushirikiana ili kufikia lengo fulani, ambalo linaweza kuwa la aina nyingi tofauti, kwa mfano: dini, elimu, siasa, sanaa, michezo n.k."

"Dini ni imani juu ya kuwepo Mungu Muumba Muweza na Mwenye nguvu juu ya kitu."
 
Mbona ukishakuwa mtu mzima hakuna anayekulazimisha uwe muumini wa dini Fulani au wewe mwenzetu umelazimishwa
Kunielewa mtu mwenye akili kiduchu kama wewe ni ngumu sana,wapi nimeongelea kubadili dini kama siyo kukurupuka??
 
kwani umekatazwa na nani? Si uende Rita ukabadilishe rasmi dini unayoitaka - Christian, Muslim, Hindu, Bahai, Buddhist..... utapokelewa tu pale utakapoelekea
Bitimkongwe nimefurahi kuona umeorodhesha imani ya Baha'i, je unauelewa nayo imani hiyo?
 
Mkishashiba makande mnaropoka tuuu
 
Acha k
NI wewe tu hujaamua kubadili imani yako lakini kwa mujibu wa katiba imeweka wazi uhuru wa kuabudu na mtu kuchagua imani aitakayo...

Hakuna sheria inayomfunga mtu kuendelea na imani aliyoikuta toka kwa wazazi...
Acha kihelehele mie naongelea mtoto kutolishwa imani ya wazazi wake hadi atimize miaka 18 ambayo ni mtu mzima kama sheria inavyosema wewe unakurupukia kubadilisha dini,we vipi??
 
A Christian is not one born to Christian parents, it's one who had a personal encounter with Christ. One can be raised a Christian and not know Christ.
 
Kuna dini zinasema mtu akiacha dini yake basi akatwe kichwa au apigwe mawe hadi afe, 🤣🤣 hapo unaonaje mkuu
Dini inasema mengi mkuu sio kwa wenye kuacha dini tu hata kwa wenye kuzini dini inasema ni nini wafanywe hao watu ila wangapi wanazini na hawafanywi kitu na dini? Na ndio hivyo hivyo hata wenye kuacha dini wengi tu wameacha dini na wanadunda tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…