Kwanini Lucky Dube hatambuliki kama muasisi ama legend wa muziki wa reggae duniani?

Jarida gani linamtaja Senzo kama nguli wa reggae???
 
Ushuzi mtupu. Muasisi wa nini? Kazi kweli
 
Mwaka 1942 tar 8 Desemba kuna mwamba alizaliwa na kupewa jina la Frederick Nathaniel Hibbert jina maarufu Toots akitoke viunga vya May Pey Jamaica ndio anatambulika kama baba na muasisi wa mziki wa Reggae na ndio mtu wa kwanza kuita muziki wa vionjo alivyokuwa anapiga kuwa ni Reggae, akiwa mtunzi na mwimbaji.

Mwaka 1968 akiwa na bendi yake ya The SKA Toots and Maytals walitoa wimbo "Do The Reggay" huyu mwamba aliwahi kufungwa jela selo namba 54-46 na kutunga wimbo uliovuma sana wa "54-46 that is my number. Baadae bend ya the wailers, wakina Burning Spare, Robert N. Marley (Alizaliwa 1945 Feb 06 na kufariki 11 Mei 1981, Jackson Memorial Hospital, Miami, Florida, Marekani) na wengine wakafuata.
 
Kuasisi ni kuanzisha, na Dube aliikuta Reggae ipo na imeshakita mizizi yake kama muziki kamili, ambao ulitumika kupinga uonevu na dhuluma. Hivyo, hawezi kuwa mwasisi.

Kingine, roots reggae ndiyo uhesabika ndiyo reggae yenyewe, na Dube reggae yake haikuwa sana roots ndiyo maana haimweki katika kapu moja na watu kama akina Burning Wailer au Culture.

Ova
 
I believe Jimmy Cliff ndiyo wa kwanza kuitangaza reggae hata kabla ya hao akina Bob Marley kujulikana.
 
Mm Lucky Dube ndio namuonaga kama mwamba had huwa najiulza mbn BOB MARLEY ndio ana jna zaid!?
Bob anakufa, Dube hajaanza mziki.
Dube ana heshima yake, lakini haifanyi awe Muasisi. Hata Bob sio Muasisi wa Reggae, kabla hajazaliwa reggae IPO. Sema, Bob ndiye aliyeufikisha kila kona ya Dunia mziki.

Bob na Dube hawalinganishiki, ni makosa.
 
Mm Lucky Dube ndio namuonaga kama mwamba had huwa najiulza mbn BOB MARLEY ndio ana jna zaid!?
Ndo yale yale ya kutangulia mkuu,mimi pia namuelewa saaaana mwamba,sema nahisi hapewi maua kisa hakuwa Mjamaica au mwenye asili ya Amerika kusini maana lndustries zimeshikwa na weupe hawa
 
Luck Dube sio muasisi wa muziki wa reggae, kaukuta ulisha asisiwa .
sawa ila mbona hata kwenye ugoat hawamuwek sasa.ukiingia Google au Forbes utatajiwa mpaka wakina Morgan heritage maajabu😅😅
 
Mkuu unafuatilia sana MUZIKI maelezo mazuri
 
Kijana nadhani wewe nyimbo unaxozifahamu za dube hazizidi tatu BACK TO MY ROOT,TOGETHER AS ONE na THE WAY IT IS kwa hiyo ungeishia kusoma tu..DUBE kinachofanya musimuelewe baadhi yenu alichana kwa mtindo wa kisasa.ameimba REGGAE katika mifumo tofauti tofauti na akina Marley ambapo yake ilikua sweet reggae ila ujumbe mkali kiasi kwamba hata kifo chake inasemekana kuna watawala walihusika ile ya kusema ni kisasi ni maneno tuu ya watu,aliimba nyimbo za haki,mapenzi na ambapo akina tosh walibez kwenye mtindo na content za aina moja tuu..mimi nina nyimbo hazizidi tatu za luckydube ambazo pengine sijazisikia,kwenye simu yangu nina album 26 zote na nimezichambua tangia wayback hadi anadead.nyinyi mnazijua za juz na popular tuu,jamaa anazo behind kama JAH SAVE US,TRINITY,RASTA MAN PRAYER,KISS NO FROG,USIZI,RESPECT etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…