Kwanini mabasi yote ya mikoani yana tabia hii?

Kwanini mabasi yote ya mikoani yana tabia hii?

Nilikuwa najua wanaopenda gospel ni waumini wa imani ya kikristo. Nimestaajabu kuna gospel ujumbe wake unawakuna hadi wake za masheikh na wanasikiliza kwenye simu zao.

Ila kiukweli mimi swala la kuweka mamziki au movie kwenye mabus huwa naona kelele sana. Kila mtu abebe entertainment zake kama Music kwenye Simu etc.
 
Majibu mengi kwenye hii thread yametolewa kana kwamba nimekashifu dini ya kikristo ama nimesema izo nyimbo zisipigwe kwenye mabasi ya mikoani. Acheni kujibu kwa jazba mimi simply niliuliza nijue sababu maana nimeona ni desturi ya mabasi mengi.
 
Inategemea na wamiliki wa gari, kuna zile basi zinapiga nyimbo za kwaya, wengine wanaweka mahubiri, wengine mawaidha, nyingine kaswida, wengine michezo ya kina Majuto, wengine ni mwendo wa ndombolo na kiwazenza...

Kuna wakati nilikuwa nasafiri kwenda Mtwara, kuanzia Temeke hadi nafika Mtwara, tulipigwa kaswida na mawaidha...

Zamani ile nasafiri mara kwa mara kwenda Moshi au Arusha, ilikuwa ukipanda Dar Express, huko utakutana na kwaya mwanzo mwisho...
 
Kwanini kila basi la mkoani lina tabia ya kupiga nyimbo za injili ama gospel nusu nzima ya safari?
Kwani tumeshachukuliwa kuwa wasafiri wote ni wakristo?
Sasa mheshimiwa unataka wapige za Diamond na Harmonize kwani abiria wote ni wapagani?🙄
 
Unataka wapige hizi za matusi za vijana?
Imefika wakati basi zifunge tablet kila siti
 
Watanzania wengi hampendi kujisomea hivyo acha waweke muziki tu ila muziki kama sio live hautakiwi kwenye chombo cha umma.
 
Kikubwa ni ujumbe unaotolewa kwenye Gospel song, Je zina maudhui mabaya? Hata muislam anaweza sikiliza na kuburudisha. Mimi ni mkatoliki ila nasikiliza kwaya zote, mfano kuna nyimbo fulani ya kilokole, "nina baba yangu asiyeshindwa kamwe" ukisikiliza lazima upate mzuka tu. .
 
Track bora ya gospel ya muda wote

"Shetani na mama mkwe wake wanalia, shetani na mama mkwe wake wamekalia misumari ... " [emoji23]
 
Kwanini kila basi la mkoani lina tabia ya kupiga nyimbo za injili ama gospel nusu nzima ya safari?
Kwani tumeshachukuliwa kuwa wasafiri wote ni wakristo?

Afrika bado kuna ushamba mwingi sana, hususani hapa kwetu. Tofauti sana na nchi zilizostaarabika kama vile nchi za kiarabu ustaarabu ni mwingi mno mpaka safari unaihisi nyepesi, na usafi wa hali ya juu. Huku sasa😁 unapanda bus halafu linafunguliwa limziki ama movie ama kwaya sometimes wanaweka sauti ya juu dah 😁 utafikiri wote waliopanda humo ni dini moja/wasikiliza miziki.
 
Kuna wahubiri wanaoingia na kuhubili injili kisha wakishamaliza wanaomba sadaka....
 
boat za zenj tunapigwa mawaidha na hakuna kitu tunafanya zaidi ya kuweka earphone😐
 
Kuna dereva mmoja aliweka kaswida hadi wakamgombeza ndo akatoa, kwanza hatuelewi kinachoimbwa
 
Inategemea na wamiliki wa gari, kuna zile basi zinapiga nyimbo za kwaya, wengine wanaweka mahubiri, wengine mawaidha, nyingine kaswida, wengine michezo ya kina Majuto, wengine ni mwendo wa ndombolo na kiwazenza...

Kuna wakati nilikuwa nasafiri kwenda Mtwara, kuanzia Temeke hadi nafika Mtwara, tulipigwa kaswida na mawaidha...

Zamani ile nasafiri mara kwa mara kwenda Moshi au Arusha, ilikuwa ukipanda Dar Express, huko utakutana na kwaya mwanzo mwisho...
bila kusahau na nyimbo za kimakonde kwa sana tu zinapigwa
 
Kwanini kila basi la mkoani lina tabia ya kupiga nyimbo za injili ama gospel nusu nzima ya safari?
Kwani tumeshachukuliwa kuwa wasafiri wote ni wakristo?
ulishawahi kupanda shabiby? nao pia wanapiga gospel wakichanganya na diamond (domo). binafsi, kati ya situations huwa nalaani na kutamani kushuka kwenye bus ni kupigiwa mziki wa bongo flavour, bora waweke hata bongo movie to kuliko huo uchafu wa condeboy na domo. wameharibu watoto sana nchini kwa miziki yao hiyo.
 
Back
Top Bottom