Kwanini mabasi yote ya mikoani yana tabia hii?

Kwanini mabasi yote ya mikoani yana tabia hii?

Au video za Mkojani na movie za kizungu zilizotafsiriwa kwa kiswahili..aisee shidaa
 
Mbona kama unamakasiriko Mkuu.
Ila nimecheka.
Awavumilie tu mana wao ndio wenye mamlaka na chombo chao.
Abood mwenye Ni muisalmu ila magar yake yote yanapiga nyimbo za injili haswa mm mwenye Kuna nyimbo ndio nimekuna kusikia kwa abbodi kuwa Nani kaimba mnk nilikuwa nasikilizaga tu bila kujuwa
 
Kwanini kila basi la mkoani lina tabia ya kupiga nyimbo za injili ama gospel nusu nzima ya safari?
Kwani tumeshachukuliwa kuwa wasafiri wote ni wakristo?
Ukishaingia kwenye public transport kubaliana na kila hali.
 
Majibu mengi kwenye hii thread yametolewa kana kwamba nimekashifu dini ya kikristo ama nimesema izo nyimbo zisipigwe kwenye mabasi ya mikoani. Acheni kujibu kwa jazba mimi simply niliuliza nijue sababu maana nimeona ni desturi ya mabasi mengi.
Utachoka kwa majibu.Weye tulia tu ndugu.Teh!
 
Kwanini kila basi la mkoani lina tabia ya kupiga nyimbo za injili ama gospel nusu nzima ya safari?
Kwani tumeshachukuliwa kuwa wasafiri wote ni wakristo?
Jaza nyimbo unazopenda kwenye simu yako ukipanda basi weka headphone masikioni biashara imekwisha.

Au kama unaenda Dodoma au Arusha panda luxury kila siti ina tv yake, free WiFi na seat ni two by one.

Dunia ni yako chaguo ni lako.
 
Abood mwenye Ni muisalmu ila magar yake yote yanapiga nyimbo za injili haswa mm mwenye Kuna nyimbo ndio nimekuna kusikia kwa abbodi kuwa Nani kaimba mnk nilikuwa nasikilizaga tu bila kujuwa
Download app ya shazham.
 
Kwanini kila basi la mkoani lina tabia ya kupiga nyimbo za injili ama gospel nusu nzima ya safari?
Kwani tumeshachukuliwa kuwa wasafiri wote ni wakristo?
mbona mabasi ya mkoa wa Tanga yote hayana hizo na wanapiga kaswida na mihadhara ya kiislam mwanzo mwisho au tafiti zako umefanyia wapi?
 
Nakubaliana na wachangiaji wanao sisitiza uvumilivu katika dini, lkn katika muktadha wa customer care ni wajib wa wamiliki na wasimamizi wa mabasi kuangazi mila, tamaduni na miiko ya kila abiria na kutengeneza uwiano katika utoaji wa huduma.
 
Nivyema wasiweke kitu chochote mana makelele sio mazuri.
 
Back
Top Bottom