Sasa mheshimiwa unataka wapige za Diamond na Harmonize kwani abiria wote ni wapagani?🙄Kwanini kila basi la mkoani lina tabia ya kupiga nyimbo za injili ama gospel nusu nzima ya safari?
Kwani tumeshachukuliwa kuwa wasafiri wote ni wakristo?
Track bora ya gospel ya muda woteKikubwa ni ujumbe unaotolewa kwenye Gospel song, Je zina maudhui mabaya? Hata muislam anaweza sikiliza na kuburudisha. Mimi ni mkatoliki ila nasikiliza kwaya zote, mfano kuna nyimbo fulani ya kilokole, "nina baba yangu asiyeshindwa kamwe" ukisikiliza lazima upate mzuka tu. .
Kwanini kila basi la mkoani lina tabia ya kupiga nyimbo za injili ama gospel nusu nzima ya safari?
Kwani tumeshachukuliwa kuwa wasafiri wote ni wakristo?
bila kusahau na nyimbo za kimakonde kwa sana tu zinapigwaInategemea na wamiliki wa gari, kuna zile basi zinapiga nyimbo za kwaya, wengine wanaweka mahubiri, wengine mawaidha, nyingine kaswida, wengine michezo ya kina Majuto, wengine ni mwendo wa ndombolo na kiwazenza...
Kuna wakati nilikuwa nasafiri kwenda Mtwara, kuanzia Temeke hadi nafika Mtwara, tulipigwa kaswida na mawaidha...
Zamani ile nasafiri mara kwa mara kwenda Moshi au Arusha, ilikuwa ukipanda Dar Express, huko utakutana na kwaya mwanzo mwisho...
ulishawahi kupanda shabiby? nao pia wanapiga gospel wakichanganya na diamond (domo). binafsi, kati ya situations huwa nalaani na kutamani kushuka kwenye bus ni kupigiwa mziki wa bongo flavour, bora waweke hata bongo movie to kuliko huo uchafu wa condeboy na domo. wameharibu watoto sana nchini kwa miziki yao hiyo.Kwanini kila basi la mkoani lina tabia ya kupiga nyimbo za injili ama gospel nusu nzima ya safari?
Kwani tumeshachukuliwa kuwa wasafiri wote ni wakristo?