Kwanini magari aina ya Nissan yanasumbua mafundi kwenye matengenezo?

Ni nini kinakufa mkuu mimi ndio hapo nataka kujua...
Sensors ikifa angalia na mashine yenye updated software, nunua sensor original, gari isiwe ya mikono mingi, oil service kwa wakati, hakikisha haichemshi, zingatia coolant engine inapinda block kirahisi ila zinauzwa cheap.
 
Nissan Terano lipo linadunda tu miaka zaidi ya kumi,fundi wake ni mzee mmoja mstaafu wa Sub Scania.
Kuna kipindi ilisumbua sana Cylinder head mzee akakagua mfumo wa cooling system aliporekebisha mfumo wa cooling na tatizo la cylinder head likaisha.
 
Lakini walioweka thermostat walifanya research ya kutosha. Ndiyo maana hata magari yatokayo UAE, pamoja na joto la kule, bado yanakuwa na thermostat.

Nina uzoefu wa kuondoa thermostat, na simshauri mmiliki wa gari kutoa. Miaka kama kumi iliyopita nilipata breakdown ya gari, tena Toyota nikiwa Ruvu darajani, fan clutch ilikufa, na gari ikaanza kuchemsha. Nikaiendesha mdogomdogo mpata chalinze. Pale hawa mafundi wetu wakaibana fan, lakini wakanishawishi niitoe thermostat wakidai huku kwetu haina haja ya kuwemo kwenye engine.

Kwa shingo upande, nikakubali kuitoa thermostat lakini sikuwaachia. Nikaanza tena safari kuelekea Mbeya, ila sikufika Iringa. Kila nilipotaka kukanyagia, temperature ilipanda. Nikapumzika comfort motel (enzi zile), baada ya engine kupoa, nikapanda kitonga kwa shida mpaka Iringa.

Pale Iringa nikatafuta Fundi akarudishia thermostat yangu, nikaanza tena safari kwenda Mbeya. Nikakanyagia mashine kwa hasira, haikupandisha temperature kabisa na gari nipo nayo mpaka leo na thermostat sijaitoa.

Kwa uzoefu huu, Mimi simshauri mtu yeyote kuondoa thermostat kwenye engine ya gari yake, labda iwe imekufa, lakini ikifa pia, mpya zipo, una replace tu.
 
Sensors ikifa angalia na mashine yenye updated software, nunua sensor original, gari isiwe ya mikono mingi, oil service kwa wakati, hakikisha haichemshi, zingatia coolant engine inapinda block kirahisi ila zinauzwa cheap.
Ok hii kanuni ni kwa gari zote Mkuu ndio nilitaka kujua hii Nissan ina utofauti upi na magari mengine maana kama Nissan ya kawaida tuu tunalia jee Rover au Benz hizi za kisasa tutaziweza kweli...
 
Ok hii kanuni ni kwa gari zote Mkuu ndio nilitaka kujua hii Nissan ina utofauti upi na magari mengine maana kama Nissan ya kawaida tuu tunalia jee Rover au Benz hizi za kisasa tutaziweza kweli...
Nissan haitakusumbua sana ukifata hizo kanuni. Toyota mfano rav 4 old hata usipofat hizo kanuni inavumilia,ukifata kanuni inaishi milele ndo watu wanazilinganisha hapo. Rover,BM na Benz hutaziweza kama nissan unalia lia kuihudumia.
 
Mkuu mimi nilikua nauliza kujua hayo magari yanawasumbua nini zaidi ila sipo kwenye hayo sasa hivi nishatoka huko kitambo kidogo...
 
Wengi wao waganga njaa tu sasa mtu anajiita fundi umeme ama fundi waya hana lolote anahangaika kuchuna nyaya na kuunganisha kitesta sijui kimechoooka anaungaunga hajui A wala B, mwisho anakwambia sensor imekufa lete laki tano Mxiuuuuuuuuu , kuna mmoja nilimtandika makofi hana hamu.
 
Shida mafundi wetu wanapiga ramli, gari ni kama binadamu lazima diagnosis ifanyike. Unaweza kununulishwa vifaa na gari isipone
Kuna jamaa gari ilizingua kina Fundi Maiko wakamnunulisha pump na makolokolo ya karibia 700k na haikupona.

Akampa jamaa yangu mmoja k/koo , akabadili plugs tu mwendo mdundo[emoji1][emoji1]
 
Si bure una idea za ufundi au umeendesha gari bovu mda mrefu huko nyuma[emoji1787]
 
wakuu nissan dualis inasauti mbaya kama exahaust ina tundu lakini nilifungua nikakuta yale masega hayapo je hii inaweza kuwa sababu na naweza pata wapi masega
 
na nilifanya engine diagnosis gari haina shida yoyote natafuta fundi mzuri a fix hili tatizo la sauti msaaada wadau gari mpya haina 3 month
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…