Kwanini Magufuli aliwaogopa sana Nape na January Makamba?

Angewaogopa asingewarekodi na kuvujisha, kama kweli hao watu wangekuwa na ubavu basi hapo walikuwa wamechokozwa au tuseme Magufuli alianzisha shambulizi tungeona wakijibu.
 
Nani alikuwa teyari kuandamana ila kaogopa polisi? Tusijifiche kwenye hicho kivuli cha polisi wakati watu hata hawakuwa na hiyo nia ya kutaka kuandamana.

Mitandaoni humu mlikuwa mnaonesha kuwa hamuogopi jeshi la polisi ni kufa na kupona.

Usitake kutufanya hatukuona polisi wakizunguka mitaani na vitisho juu, au hukuwa hapa nchini nini? Kwa taarifa yako hadi sasa kuna watu wanaendelea kuachiwa kutokana na kesi za kubambikiwa kuhusu kupinga vitendo vilivyofanyika kwenye uchaguzi ule.

Au kwakuwa vyombo vya habari vilidhibitiwa visiripoti matukio yale, basi unadhani hatujui lolote? Kama ulikuwa unategemea taarifa toka TBC1 ndio unajua watu hawakutaka kuandamana.
 
Angewaogopa asingewarekodi na kuvujisha, kama kweli hao watu wangekuwa na ubavu basi hapo walikuwa wamechokozwa au tuseme Magufuli alianzisha shambulizi tungeona wakijibu.

Kitendo cha kuwarekodi ndio woga wenyewe na ni kosa kisheria. Wao wangejibu vipi wakati Magufuli alikuwa anapambana nao kwa kutumia state apparatus, huku wao wakiwa hawana nguvu hiyo? Unataka kufanya kama vile Magufuli alikuwa anapambana nao kama yeye, kumbe yeye kilichokuwa kinambeba ni ulevi wa madaraka.
 
Angewaogopa asingewarekodi na kuvujisha, kama kweli hao watu wangekuwa na ubavu basi hapo walikuwa wamechokozwa au tuseme Magufuli alianzisha shambulizi tungeona wakijibu.
Alivujisha mazungumzo yao sababu walitoa waraka kumvaa yeye kuwa anamtuma Musiba kuwatukana
 
Nimeuliza ni nani walikuwa teyari kuandamana? Tatizo mnakimbilia kujificha kwenye hicho kisingizio cha polisi ila kiuhalisia hakuna hao waandamanaji, nimekwambia huku mitandaoni mlikuwa mnasema lazima muandamane wakati polisi wanapiga mikwara yao ila mkasema hamuogopi sasa ajabu tena unakuja na kisingizio cha kushindwa kuandamana kwa kuogopa jeshi la polisi.

Kama maandamano yale yangefanywa mitandaoni basi kweli pangechafuka.
 
Huku mitandaoni kauli ilikuwa ni moja, au kulikuwa na kiongozi huku jukwaani? Ulitaka huku mitandaoni watu waseme hawataandamana? Huku kwenye mitandao si ndio watu ilibidi hadi watumie VPN?
 
Alivujisha mazungumzo yao sababu walitoa waraka kumvaa yeye kuwa anamtuma Musiba kuwatukana
Walishindwa kumgusa Musiba asiwachafue na walipotoa huo waraka jamaa akajibu kwa kuwarekodi na kuvujisha sauti zao, wengine wakaenda kuomba msamaha.
 
Huku mitandaoni kauli ilikuwa ni moja, au kulikuwa na kiongozi huku jukwaani? Ulitaka huku mitandaoni watu waseme hawataandamana? Huku kwenye mitandao si ndio watu ilibidi hadi watumie VPN?
Ndio maana yake zilikuwa drama tu za mitandaoni wakati huo mitaani hali ni tofauti na ndio maana siku ya tukio watu wako bize na mambo yao, ndio maana nasema kama hayo maandamano yangefanyika mitandaoni basi ingekuwa balaa maana kulionyesha hawaogopi jeshi la polisi.
 
Acha uongo wewe.

Unataka kutuaminisha ujinga, kwanini wasingegombea Urais Sasa kama walikuwa na nguvu kama unavyotaka kutuaminisha hapa.

Najua unachuki na Hayati Magufuli huna lolote wewe!!
 
Mbona hamsemi Magufuli kama dikteta aliyekuwa anauwa watu aliwaogopea kitu gani akina Nape?
 
Mbona hamsemi Magufuli kama dikteta aliyekuwa anauwa watu aliwaogopea kitu gani akina Nape?

Unadhani ukiwa dictator ndio huogopi? Kumbuka udictator wake alikuwa anafanya kwa kutegemea state apparatus, ambazo pia hao aliokuwa hawapendi walikuwa na ukaribu nazo.
 
Unadhani ukiwa dictator ndio huogopi? Kumbuka udictator wake alikuwa anafanya kwa kutegemea state apparatus, ambazo pia hao aliokuwa hawapendi walikuwa na ukaribu nazo.
Wao walifanya nini? Maana Magufuli alimtumia Musiba kuwachafua na hawakuweza kumgusa Musiba, wakaandika waraka jamaa akawarekodi mazungumzo yao na kuvujisha wengine wakaenda kuomba msamaha.
 
Wao walifanya nini? Maana Magufuli alimtumia Musiba kuwachafua na hawakuweza kumgusa Musiba, wakaandika waraka jamaa akawarekodi mazungumzo yao na kuvujisha wengine wakaenda kuomba msamaha.

Kwa katiba hii rais ni mungu, hivyo walienda kuomba msamaha ili wawe salama maana walikuwa wanapambana na aliyeshika mpini. Lakini hawakuomba msamaha kwa kukosa bali ndio unafiki wenyewe ili wabaki kwenye mlo. Leo hii Magu hayuko madarakani ama hai, wanaonyesha fika hawakuomba msamaha wa dhati.
 
Hivi kile chuma ni cha kuogopa hawa wadudu kweli jamani!
Nape alikwenda ikulu kwa magoti ambayo ni ishara ya woga uliopindukia!
Makamba wote 2 walitafuta hadi mashimo ya kuingia kumkimbia 🗝️🔑🤣
Aah, wapi, makamba alikua cool tu, akiendelea na ishu zake,, wala hakuhangaika kuomba msamaha,,
Nape naye aliomba msamaha kiuongo uongo tu, just for show..
 
Kwahiyo pamoja na hayo majina hakuogopa kuwarekodi na kuvujisha sauti zao?
Kwanini avujishe kwa Siri?, Kwanini hakudeal nao kimya kimya, akaamua kuwatafutia sababu in public?
 
Hivi kile chuma ni cha kuogopa hawa wadudu kweli jamani!
Nape alikwenda ikulu kwa magoti ambayo ni ishara ya woga uliopindukia!
Makamba wote 2 walitafuta hadi mashimo ya kuingia kumkimbia [emoji2785][emoji360][emoji1787]
[emoji16] Makamba power 2 walibatizwa kwa moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…