Nje ya main biblical scriptures. Hiz ni doctrine ambazo hazithibitishwi na maandiko ya kikristo. Ni kama mambo ya imani zilizozaliwa kutokana na tamaduni tu wa watu, sio ukristo kwa jinsi navyofikiri mimi. Hazipo katika vitabu 67 vya kibiblia
Unafahamu kuwa hivyo vitabu vya kwenye biblia vilitolewa kwenye Tanakh ya kiyahudi na kupangwa upya? Waka ondoa vingine wasivyovitaka?
Lugha asilia ilikuwa ni Kiebrania na Kiaramu kwa Agano la Kale (Tanakh ya Kiyahudi) na Kigiriki Agano Jipya. Biblia ilitafsiriwa katika Kilatini ili Wakristo katika Milki ya Roma waweze kuielewa. Tafsiri maarufu ya Kilatini ni Versio Vulgata ya St. Jerome.
Jerome alitafsiri Biblia katika Kilatini kati ya A.D. 383 na 404. Hapo awali aliitafsiri yote kutoka Kigiriki, lakini alipoendelea alirekebisha Agano la Kale dhidi ya asili ya Kiebrania.
Biblia unayoisoma, ilitafsiriwa na Jerome ambae ni mroma,
Je Jerome alitumia chanzo kipi kuitafsiri?
Kumbuka Mitume walikuwa Wayahudi, maana yake hao wayahudi ndio walihusika kutunza maandiko hayo, na kitabu Chao ni Tanakh. (hiki ndicho chanzo cha biblia)
Kumbuka Yesu alisoma kifungu kutoka chuo cha nabii Isaya.
Luka 4 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
¹⁵ Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote.
¹⁶ Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
¹⁷ Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,
¹⁸ Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
¹⁹ Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
²⁰ Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
Akasema hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza
Mathayo 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁷ Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
¹⁸ Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.
Je biblia ya vitabu 66 haina kitabu cha nabii Isaya?
Je wakati Yesu anakisoma hicho kitabu biblia ilikuwepo?
Jibu ni kitabu kilikuwepo na biblia haikuwepo.
Je waliokiingiza kwenye biblia walikitoa wapi?