Kwanini malaika wana majina ya Kizungu na majini (mapepo) yana majina ya Kiarabu?

Kwanini malaika wana majina ya Kizungu na majini (mapepo) yana majina ya Kiarabu?

Samahani, hapa ulimaanisha nini??

Ukinipa ufupisho wa hayo mambo itapendeza! Inaonekana umeiva kwenye elimu ya dini, umeelewa na siyo kukariri! Huna papara, hasira, hisia, mhemko ,jazba na chuki!
Wabongo wameshindikana, Andrew Nyerere yeye yuko Buddha na ndio anatafsiri vitabu vyake kuja kwenye kiswahili.

Kuna siku down town nilimuona mswahili amevaa kama masingasinga nilishindwa kushangaa, maana mshangao ulipitiliza.
 
Kwa sasa Dini yangu Kubwa ni Upendo, Kujali wengine na Kusaidia Watu Wanaohitaji msaada wangu..

Ubaya ni kwamba Judaism haina Ufupisho wa maelezo Ya Kitheolojia..
Hapana Kuiva ni vigumu sana Ila Nilichonacho huwa napenda kukitoa..

Kwa kifupi Dini ya Judaism Ina Tofauti na Dini ya Kikristo na Uislamu Kwa 85% kwa mafundisho yao..

Yaani Ukristo na Uislamu unafanana kwa 70% lakini uko tofauti na Uyahudi kwa 90% yaani unafanana kwa only 10% tu..

Nilijifunza mengi sana.. Kupitia Halakha,Gemera , Mishnah zinakufanya Ujue Sheria na Torah kwa ukaribu sana
Bado BUDHISM mkuu
 
Dah Hongera sana....
Kwahyo Sasa Hivi naweza kukuita Rabbi..?
Bado mkuu. Kuwa rabbi sio mchezo
Unatumia miaka mingi kusoma maandishi ya kale ya Kiyahudi - Tanakh, Mishnah, Talmud, ili kupata ustadi wa kusoma, kuelewa, kuchambua, na kufikia hitimisho sawia la kitheolojia na kivitendo kuhusu kuishi kulingana na sheria ya Kiyahudi, ambayo inaelezea kwa undani jinsi Myahudi anavyopaswa kuishi kulingana na Agano kati ya Mungu na watu wa Kiyahudi.

Kuna hatua tano za kufata hadi uidhinishwe kuwa Rabbi.

1- Lazima uwe Myahudi. (kiimani)

2 - Ujue vizuri Tanakh, Mishnah, Talmud. Hapa wanataka uwe na ujuzi wa kusoma, kuelewa, kuchambua na kuishi kwa mujibu wa sheria ya Kiyahudi, kulingana na Agano kati ya Mungu na wayahudi.

3 - Ufaulu mitihani inayoonyesha ustadi wako na ujuzi wako maalum katika maeneo fulani ya sheria ya Kiyahudi kivitendo. Mamlaka, na Rabbi Mkuu wa Israeli, watachunguza kuhusu elimu yako na ujuzi uliopata.

4 - Lazima ujifunze chini ya ulezi wa rabbi mwenye uzoefu jinsi ya kutumia ujuzi wako katika hali halisi ya maisha.

5 - Lazima wajiridhishe unaonyesha tabia na utu mzuri wa kimaadili, wa kumcha Mungu, na kukubali kwa unyenyekevu kujitolea, kibinafsi kwa sheria na mila za watu wa Kiyahudi.

Ukifaulu hayo yoye, unaidhinishwa kuwa Rabbi.
 
Bado mkuu. Kuwa rabbi sio mchezo
Unatumia miaka mingi kusoma maandishi ya kale ya Kiyahudi - Tanakh, Mishnah, Talmud, ili kupata ustadi wa kusoma, kuelewa, kuchambua, na kufikia hitimisho sawia la kitheolojia na kivitendo kuhusu kuishi kulingana na sheria ya Kiyahudi, ambayo inaelezea kwa undani jinsi Myahudi anavyopaswa kuishi kulingana na Agano kati ya Mungu na watu wa Kiyahudi.

Kuna hatua tano za kufata hadi uidhinishwe kuwa Rabbi.

1- Lazima uwe Myahudi. (kiimani)

2 - Ujue vizuri Tanakh, Mishnah, Talmud. Hapa wanataka uwe na ujuzi wa kusoma, kuelewa, kuchambua na kuishi kwa mujibu wa sheria ya Kiyahudi, kulingana na Agano kati ya Mungu na wayahudi.

3 - Ufaulu mitihani inayoonyesha ustadi wako na ujuzi wako maalum katika maeneo fulani ya sheria ya Kiyahudi kivitendo. Mamlaka, na Rabbi Mkuu wa Israeli, watachunguza kuhusu elimu yako na ujuzi uliopata.

4 - Lazima ujifunze chini ya ulezi wa rabbi mwenye uzoefu jinsi ya kutumia ujuzi wako katika hali halisi ya maisha.

5 - Lazima wajiridhishe unaonyesha tabia na utu mzuri wa kimaadili, wa kumcha Mungu, na kukubali kwa unyenyekevu kujitolea, kibinafsi kwa sheria na mila za watu wa Kiyahudi.

Ukifaulu hayo yoye, unaidhinishwa kuwa Rabbi.
Nayaelewa Mkuu hayo..
Me nilidhani Tayri Umeshamaliza Maana Mimi niliacha niliporudi Tz nikaamua Kuacha Uyahudi kabisa
 
Nayaelewa Mkuu hayo..
Me nilidhani Tayri Umeshamaliza Maana Mimi niliacha niliporudi Tz nikaamua Kuacha Uyahudi kabisa
Niko namba 3 mkuu.
Ulikutana na changamoto gani mpaka ukaamua kuacha.
 
Habari Tena Mkuu!
Ukisoma kwenye Isaya 40:22 inayozungumziwa Sio Dunia as Whole but inayozungumziwa ni Dome-Shaped Structure ambayo Huitwa Firmament..

Unajua maana ya firmaments??

Nakurejesha Genesis/Mwanzo 1:6-8

"And God said, Let there be a firmament in the midst of the waters, and let it divide the waters from the waters.
And God made the firmament, and divided the waters which were under the firmament from the waters which were above the firmament: and it was so.
And God called the firmament Heaven. And the evening and the morning were the second day."

so lets Discuss Ulichoandika Isaya 40:22
Na kilichopo kwe he Mwanzo 1:6-8..

Firmament ni duara ya Anga Ambayo huitwa Mbingu ndo hiyo ambayo Mungu hukaa kwa mujibu wa Biblia na Ndo hiyo huitwa Mbingu Ni kama Dome hivi..

Hii ndo Dunia According to Bible Mkuu Yenye Firmament..
View attachment 2979150

View attachment 2979152


So Mkuu Pitia na Hizi verse..

1 Chronicles 16:30: “He has fixed the earth firm, immovable.”

Psalm 93:1: “Thou hast fixed the earth immovable and firm …”

Psalm 96:10: “He has fixed the earth firm, immovable …”

Psalm 104:5: “Thou didst fix the earth on its foundation so that it never can be shaken.”

Isaiah 45:18: “… who made the earth and fashioned it, and himself fixed it fast …”
Kuna shidah hapa sema ni ngumu sana kunielewa, hayo maneni ni ya realm gani?? Hiyo kuzimu yako ulio weka hapo chini physical kama utaikuta
 
Hata malaika Israel mtoa roho ni jina baya lkn kwa shobo zenu na wazungu linaonekana zuri,, iweje nchi iitwe Israel (malaika mtoa roho) alafu ndo liwe taifa teule la Mungu,, hali kama hii ingekuwa nchi moja kati ya za kiislam ndo ina jina la malaika mtoa roho (Israel) nadhani ungeanzisha nyuzi Mia kwa siku na chuki zako za wazi kabisa,, tofauti yako ktk hili wewe na MK254 ni jamaa ni wendawazimu, ila wewe mzima unafanya kusudi
 
Neno took, and make them wives ni tofauti,
Ok sasa Nifatilize hapa Chini..
Andiko Hilo Limetoka kwenye Genesis/Mwanzo au Bere'shit 6 : 2..

In Hebrew inaandikwa Hivi..

וַיִּרְאוּ בְנֵי־הָאֱלֹהִים אֶת־בְּנוֹת הָאָדָם כִּי טֹבֹת הֵנָּה וַיִּקְחוּ לָהֶם נָשִׁים מִכֹּל אֲשֶׁר בָּחָרוּ׃

inasomeka hivi..

Wayyir'u v'nei haElohim et-B'not haAdam Ki tovot hena vayik'chu lahem nashim mikol asher bacharu..
Kwa Lugha ya Mfalme charles..

That the sons of God saw the daughters of men that they were fair; and they took them wives of all which they chose.


Sasa kwenye Tafsiri ambayo imekuchanganya ni hiyo niliyowekea Rangi nyekundu..

Yaani:-

וַיִּקְחוּ לָהֶם נָשִׁים מִכֹּל אֲשֶׁר בָּחָרוּ
(vayik'chu lahem nashim mikol asher bacharu
)

Neno וַיִּקְחוּ (vayik'chu) - ni Nafsi ya Tatu Wingi Kama kingereza wangesema "They took" na hapo ni Katika wakati uliopita ambayo imetokana na verb "לקח" (lakach), ambayo inamaanisha kujichukulia ,Kuchukua,Kutwaa "to take."

Neno לָהֶם (lahem) -linamaanisha kwa ajili yao wenyewe yaaani "to them" au "for themselves."

Neno נָשִׁים (nashim) - Ni wingi wa Neno "אישה" (isha), Ambayo Linamaanisha "mwanamke(Woman)" au "Mke."

Neno מִכֹּל (mikol) - linamaanisha kutoka kwa wote au kwa wote ("of all" or "from all.")

Neno אֲשֶׁר (asher) -Ni relative pronoun inamaanisha "that" au "which."

Neno בָּחָרוּ (bacharu) - Hii ni Mafsi ya Tatu wingi iliyotokana na verb "לבחור" (libokhar), ambayo humaanisha Kuchagua ( "to choose.")..


Sasa baada ya kukuchambulia Hiyi nafikiri Umenielewa Kiasi..

Sasa tujikite kwnye neno vayik'chu..
Nataka nikurudishe Nyuma Nikupe mfano mmoja tu kwenye mwanzo hapo hapo sitaki kwenda mbali

Neno Hilo Vayik'Chu limetumika Sana kwenye Biblia likimaanisha kuchukua au kutwaa/Kujitwalia

Kwenye Mwanzo/Geneis 4:19..

Lameck anajitwalia Wake wawili..inasomeka hivi..

Mwanzo 4:19

"Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila."

'And Lamech took unto him two wives: the name of the one was Adah, and the name of the other Zillah."


Nakupeleka kwa Lugha ya Kiebrania..


וַיִּקַּח־לוֹ לְמֶךְ שְׁתֵּי נָשִׁים שֵׁם הָֽאַחַת עָדָה וְשֵׁם הַשֵּׁנִית צִלָּה׃

vayikach-lo Lemech shtey nashim shem ha'achat Adah ve-shem ha'shenit Tzillah..

Umenielewa sasa?

Kwahyo kwa Mujibu Wa Tafsiri Hizo umeelewa Maana ya They Took uliyokuwa unataka??
 
Kuna shidah hapa sema ni ngumu sana kunielewa, hayo maneni ni ya realm gani?? Hiyo kuzimu yako ulio weka hapo chini physical kama utaikuta
Najua Unazungumzia Nini so Realm ya Kuzimu Ni 5th Dimension Anticlockwise au Ni 5th dimension Kushuka Chini...
Sefirat?
 
  • Thanks
Reactions: 511
Nje ya main biblical scriptures. Hiz ni doctrine ambazo hazithibitishwi na maandiko ya kikristo. Ni kama mambo ya imani zilizozaliwa kutokana na tamaduni tu wa watu, sio ukristo kwa jinsi navyofikiri mimi. Hazipo katika vitabu 67 vya kibiblia
Unafahamu kuwa hivyo vitabu vya kwenye biblia vilitolewa kwenye Tanakh ya kiyahudi na kupangwa upya? Waka ondoa vingine wasivyovitaka?

Lugha asilia ilikuwa ni Kiebrania na Kiaramu kwa Agano la Kale (Tanakh ya Kiyahudi) na Kigiriki Agano Jipya. Biblia ilitafsiriwa katika Kilatini ili Wakristo katika Milki ya Roma waweze kuielewa. Tafsiri maarufu ya Kilatini ni Versio Vulgata ya St. Jerome.

Jerome alitafsiri Biblia katika Kilatini kati ya A.D. 383 na 404. Hapo awali aliitafsiri yote kutoka Kigiriki, lakini alipoendelea alirekebisha Agano la Kale dhidi ya asili ya Kiebrania.

Biblia unayoisoma, ilitafsiriwa na Jerome ambae ni mroma,

Je Jerome alitumia chanzo kipi kuitafsiri?
Kumbuka Mitume walikuwa Wayahudi, maana yake hao wayahudi ndio walihusika kutunza maandiko hayo, na kitabu Chao ni Tanakh. (hiki ndicho chanzo cha biblia)

Kumbuka Yesu alisoma kifungu kutoka chuo cha nabii Isaya.
Luka 4 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
¹⁵ Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote.
¹⁶ Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
¹⁷ Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,
¹⁸ Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
¹⁹ Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
²⁰ Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.


Akasema hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza
Mathayo 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁷ Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
¹⁸ Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.

Je biblia ya vitabu 66 haina kitabu cha nabii Isaya?
Je wakati Yesu anakisoma hicho kitabu biblia ilikuwepo?


Jibu ni kitabu kilikuwepo na biblia haikuwepo.
Je waliokiingiza kwenye biblia walikitoa wapi?
Screenshot_20240503-093954~2.png
 
Kuna sehemu wanasema ametajwa kwenye kitabu Cha Ayubu ndio Niko hapa nimetulia nachimbua Hadi nimpate,
Jerome alitaja sifa aliyokuwa nayo Shetani, hakutaja jina lake. Tafuta maana ya Lucifer. Maana yake kwa Kiswahili ni nyota ya asubuhi. Halafu msome Isaya

Isaya 14:12 “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa”
Hapa Isaya anamuongelea Shetani

Kisha msome Yesu
Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi”.
Hapa Yohana anamuongelea Yesu

Utagundua inayoongelewa ni sifa sio jina
 
Back
Top Bottom