Kwanini malaika wana majina ya Kizungu na majini (mapepo) yana majina ya Kiarabu?

Kwanini malaika wana majina ya Kizungu na majini (mapepo) yana majina ya Kiarabu?

Nahisi Sijakuelewa Dada angu Faiza?
Hakuna Wazungu Wayahudi ulikuwa unamaanisha nini?
safi sana, nimekujibu ulichoandika wewe fata uzi ukajisome ulivyoandika. Ikiwa utajielewa basi nami utanielewa, kama hautajielewa ulichokiandika, hata nami hautanielewa nilichokijibu.
 
Mbona hata neno "malaika" ulilolitumia ni la Kiarabu?

Hapa wote mnachanya, naonesha wazi hamuelewi maana ya w-wayahudi wala wahebrania wala Waarabu".

Mkielewa maana ya hayo hamtajichanganya.

Someni.
Malaika Ni neno la Kiebrania au Kiyahudi na Kiarabu pia Huwa Ni neno moja...

Kwa mfano Kiebrania/Kiyahudi malaika huandikwa "מַלְאָךְ" (mal'akh) ambayo humaanisha Mjumbe "messenger." na wingi wake huwa "מַלְאָכִים" (mal'akhim).

Hivyo hivyo na kwa kiarabu malaika huitwa "malak" (مَلَك)..Kwahyo Kiebrania "מַלְאָךְ" (mal'akh) na Kiarabu "مَلَك" (malak) zote zinafanana kisemitic na zote Zina maana Moja ya Mjumbe au Messenger."

Sema kuna kitu kimoja ambacho ndo kilinifanya niseme kuwa Malaika ni Kutoka kwa wayahudi na Djin ni kutoka kwa Waarabu..

Kwa sababu neno Malak/Malaika Lilianza kutumika Zaidi kipindi cha Ujio wa Quran ila PreQuranic Era lilikuwa Halitumiki sana walikuwa wakitumia neno Harb (حرب) huyu ni kama Mjumbe wa Kutahadharisha kuhusu Vita..
Nadhir (نذير), Muonyaji wa matukio na Rasul (رسول) kama Mpeleka ujumbe...
 
safi sana, nimekujibu ulichoandika wewe fata uzi ukajisome ulivyoandika. Ikiwa utajielewa basi nami utanielewa, kama hautajielewa ulichokiandika, hata nami hautanielewa nilichokijibu.
Dada Faiza!
Muebrania/Myahudi sio Mzungu..
Myahudi ni Taifa Jingine Rather than a race..
Na ndo maana Waethiopia Ni wayahudi/Waebrania Ila wako Africa..
 
Mbona hata neno "malaika" ulilolitumia ni la Kiarabu?

Hapa wote mnachanya, naonesha wazi hamuelewi maana ya w-wayahudi wala wahebrania wala Waarabu".

Mkielewa maana ya hayo hamtajichanganya.

Someni.
Wayahudi ni wafuasi wa dini ya Kiyahudi.
Waebrania ni Waisrael
na Waarabu ni wale ndugu zetu wa kutoka Mashariki ya Kati
 
Kabla ya Kuendelea Soma majibu ya Post 345..

Pili Tuelewe kwanza nini maana ya Mzungu na Nini maana Ya Muebrania au Myahudi
Nimeshayasoma, hizo maana zilielezee wewe kwa ufahamu wako, mimi naelewa mtu wa nchi za Ulaya na marekani akiwa mweupe ni mzungu.

Wahebrania ni watu walioitwa " mtoto/watoto wa Mungu, kwa maana kuwa wanaamini Mungu mmoja na si lazima wawe ni wayahudi.

Naamini Yesu alikuwa ni Mhebrania lakini hakuwa Myahudi.
 
Nimeshayasoma, hizo maana zilielezee wewe kwa ufahamu wako, mimi naelewa mtu wa nchi za Ulaya na marekani akiwa mweupe ni mzungu.

Wahebrania ni watu walioitwa " mtoto/watoto wa Mungu, kwa maana kuwa wanaamini Mungu mmoja na si lazima wawe ni wayahudi.

Naamini Yesu alikuwa ni Mhebrania lakini hakuwa Myahudi.
Vilaza kweli nyie.
 
UMMY SUBIAN
ummy subian ni jini wa kike ni malkia wa jide chini ya bahari mavazi yake mekundu Pete zake nyekundu ni moja kati ya majini wakorofi akiwa kwako harafu hujatafuta Pete yake atakuadabisha huyu ummy subian yupo chini ya utawala wa sharif sultan bin daud subian ni miongoni mwa maruhaniyat wa kisharifu apa nazungumzia subian mwema kwanza jini huyu ummy subian ukiwa nae huwez kosa jini kama ruhan hizi ni koo kubwa za kijini zinazoelewana sana ummy subian ni miongoni mwa majini wenye cheo ujinini na Wana Mali sana wakikutunuku kitu shida utakisikia Kwa jirani tu na kama yupo Kwa mwanaume basi mwanaume huyo atakua na mvuto mkali sana Kwa wanawake ila jini uyu anapenda uwe msafi ujipende apo mtaendana arafu ukiwa wapenda nguo nyekundu utamfurahisha ummy subian ana uwezo wa kubadilika zaidi ya mara Tano mtu MWENYE jini huyu ukimkorofisha kimbia subian hapend mtu wake aonewe ni jini mwenye Mali ila mkorofi Mali zake zikitumiwa vibaya ukiwa nae huwez kosa jini kama ruhan ila ruhan yeye Mpore mara nyingi utakuta yeye anakutawala sana kuliko ruhani japo ruhani ni mkubwa Kwa subiani ruhan yeye anatoa tu amri subian anatekeleza ruhan ni kiongoz wake subian yupo Kwa ulinzi ila ruhan ni bosi mtoa amri labda itokee jambo zito apo ruhan ataingilia kutetea ila mara nyingi utakuta yeye ametulia tu anampa amli subian ukienda nao sana Kila kitu kwako kitakua mtelemko ukiona wateseka ujue wamefungwa au wanadai Pete yao ili wakutumikie na sio Kila mtu anao Kuna baadhi ya wanadamu Wana nyota Kali kiasi Cha kuwavutia Hawa viumbe mara nyingi wanakuja kwako Kwa kuvutiwa na nyota yako ili wakupe kile walichojaaliwa na muumba wao na kukuwekea ulinzi ili wanadam na majini wabaya wasikudhuru hiyo ni Pete ya ummy subian
View attachment 2978858
Hayo ni mambo ya akina Faiza na dini yao
 
Uislamu unaamini kuna majini walisilimu baada ya kusoma quran na ukisilimu lazima upewe jina la Kiarabu hii ndiyo maana majini wana majina ya kiarabu waliyoyachagua baada ya kusilimu
Kwa hiyo ukiliita jini kwa jina John haliwezi kuja kufanya kazi yako ngo

Majina na lugha ya kiarabu Yana impact katika tasnia ya majini

Ili uweze kuyatawala majini lazima u some kuran kwanza
 
Ningeshtuka ingekuwa ni mashetani.

Shetani aliyemkumba "Mungu" yesu kwa siku 40 alikuwa anaitwa nani?
Screenshot_2024-07-02-23-30-33-444_com.android.chrome~2.jpg
 
Back
Top Bottom