SIna shida na hii, i just want understand about Samael kama jina la malaika ibilisi. Maana iliyo bayana ni kwamba ibilisi hapo kabla aliitwa Lucifer
Hii siwezi kubaliana na wewe. Labda uniwekee refferences
Hili pia sijui ulipolitoa labda uniwekee source ili nielewe
Niliwahi kuandika Hichi kitu hapa hapa Jf muda kidogo ngoja nikiandike tena..
Lucifer=Nyota ya Asubuhi=Venus=Light Bringer
Yesu =Nyota ya Asubuhi =Venus = light bringer
Archangel (Baadhi ya malaika wakuu) =Nyota za Asubuhi...
Lucifer kama Samael au Shetani mnavyoita..
Hapa hasa ndo Walipoanzia kujikita kwenye hilo jina...
Na maneno hayo yalianza kuonekana mwaka 405 AD kwenye Tafsiri ya Biblia ya Lugha ya latin au Latin vulgate baada ya Papa Damasus wa 1 ,Kumwambia Jorome atafsiri na ndiyo ilikuwa Tafsiri ya kwanza Standard ya kilatin...
Isaya 14:12
Latin vulgate origins..
"quomodo cecidisti de caelo Lucifer qui mane oriebaris corruisti in terram qui vulnerabas gentes."
Kwa kiswahili chetu cha mama samia
"
Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni,
Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!"
Kwa Kingereza cha Anko Charles
"
How art thou fallen from heaven, O Lucifer, son of the morning! how art thou cut down to the ground, which didst weaken the nations!"
Najua Wengi mnafahamu kuhusu huu upande wa Isaya naomba niwaletee upande mwingine wa Lucifer..
Yesu mwenyewe Na Confirm kwamba yeye ni Nyota ya asubuhi..
Ufunuo wa Yohana 22:16
"
Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.
"I Jesus have sent mine angel to testify unto you these things in the churches. I am the root and the offspring of David, and the bright and morning star"
Hold on bado Pia ameahidi kwamba kwa wale watakaofata anachoamuru na wao watapewa uwezo wa kuwa Nyota ya asubuhi (Lucifer- Kwa kilatin)
Ufunuo wa Yohana 2:28
"
Nami nitampa ile nyota ya asubuhi."
"And I will give him the morning star"
Tight up your seat belt ,PopCorn and Buckle up bado naendelea..
Unakumbuka mwanzoni nilisema pia kuna group la malaika au viumbe walioko mbinguni ndo linaitwa morning stars (Lucifers)
Ayubu 38:7
"
Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?"
"
When the morning stars sang together, and all the sons of God shouted for joy?"
Sasa ilikuaje zikaacha kuimba pamoja Sasa hapo ndo nakusihi urejee kwenye Isaya 14:12 kwamba kuna Mmoja aliasi Ndo huyo mnamuita.. shetani..
Sasa Yesu aliahidi kwenye ufunuo 2:28 kutoa nyota ya Asubuhi (Lucifer) kwa watu watakaomwamini Je mtume petro kipenzi Cha pili cha Yesu akitoka Yohana na Maria magdalena anasemaje kuhusu hilo..
Na nitaweka na Vulagate kabisa ili maana halisi ionekane
2 Petro 1:19
"
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu."
"
We have also a more sure word of prophecy; whereunto ye do well that ye take heed, as unto a light that shineth in a dark place, until the day dawn, and the Morning star arise in your hearts:"
In Latin Vulgate..405 AD bible..
2 petro 1:19
"
Et habemus firmiorem propheticum sermonem cui bene facitis adtendentes quasi lucernae lucenti in caliginoso loco donec dies inlucescat et lucifer oriatur in cordibus vestris."...
umenielewa????