Kwanini mambo ya kiibilisi hufanikiwa fasta kuliko ya Mungu?

Mungu hajawahi kushindwa
Kwa hiyo sisi wadau wake ndio tunazingua.

Huwa nasikitika sana, hata kapepo
Kanaweza kumkata mitama mtumishi, kajini kale choka mbaya kabisa kanaweza kuvuruga msikiti au kanisa kumtoa ni kama vile kuwakamata magaidi wa kibiti. Huwa najiuliza sasa akija ibirisi kamanda mwenyewe si anaweza kunyonya damu waumini wote bila kufanywa chochote.

Sijui Mungu huwa anatuonaje
 
Sio kweli ni mitazamo wako hayo mawazo yakufikiri kila aliye fanikiwa ni Freemason hayo ndiyo yanayokufanya usitoboe shetani Hana chake ktk dunia hii ni muongo na mlaghai amewaaminisha uongo wengi wakaamini kua yeye ndiye anaye weza kukupa mafanikio sio kweli ili watu wasimtegemee muumba wao na ndiye aliyeumba vyote vijazavyo dunia ni sehemu gani Ktk vitabu vitakatifu kwa mfano ambapo MUNGU alimkabizi shetani utajiri wa dunia?
 
Ngoja 'wazoefu' Wakinga na Waha waje.
Mkuu mimi mkristo ila huwa naona wivu sana. Nasota na dua alafu kutoboa ni kwa mbinde tena hakuna continuity alafu wadau wa ibirisi wao ni kubonyeza tu mikwanja inatiririka kwa mujibu wa story zao.

Mungu inabidi aingilie kati aisee, hawezi kuacha vijana wake waabike hivi.

Walokole hadi jasho linatoka kufukuza kahoma tu au UTI wakati aYesu alikuwa haongei anaaangalia tu plasmodia wote wanadedi.

Na kasema watakaomuamini watafanya show kali kumzidi yeye
 
Shetani akitaka kumuhonga Yesu najumba mzee.
Au bible husomi. Ila cha ajabu wale wa Mungu wanaungaunga sana, hata kama unasema sio freemason ila wengi uganga au hata huyo Mungu hawana time naye.

Kwa nini ni rahisi Ibirisi kuwapa vitu watu wake kuliko Mungu mwenye uwezo kuwapa watu wake papo hapo baada ya maombi?

Utasikia stori, jini limemwambia mtu aende makaburini atakuta pesa na akazikuta. Ila maombi ukimalizakumuomba Mungu hata buku tu watoto wapate nauli hukuti hata sumni.

Huu ugumu unatoka wapi
 
Lete ushahidi
Hakuna ushahidi kwenye quran mkuu labda hadithi. Sio mimi ila huwa naona nidahalo na waislam wanashindwa kuleta.

Ila tusiende huko sana, kwa nini uweza wa Mungu ktk kutendea watu wake mambo kama umeshuka siku hizi kiasi kwamba ibris anaonekana kujizolea mashabiki kirahisi
 
Yameshapita hayo
 
Barikiwa.
Kuna kitu nimejifunza kiasi
 

Zaburi 90:4​

"Kwako miaka elfu ni kama siku moja tu, ni kama jana ambayo imekwisha pita; kwako ni kama mkesha mmoja wa usiku!"

Mkuu kwa Mungu wanasema miaka elfu ni kama siku moja. Sasa ukiomba utajiri Mungu akachelewesha kwa siku moja maana yake ilibidi ukae miaka elfu ndio uupate.
 
Mkuu uweza wa mungu hauwezi kushuka hata mara au la hauna imani ya kweli juu ya huyo mungu wako
 
kuna mdada mmoja alipata post kapangiw shule ya hapa kijijin kwangu;
ailetwa kuripoti na mamaake akiw kama kichaa na afya imezorota htr kam mgonjwa wa ukimwi.
kifupi wanasema alikuw karogwa au kutupiwa majini,
basi akapew ruhusa ya kutosh kufany matibabu.
watu wa dini waliooomba mpak maneno yote na njia zao zote zikaish; lkn wap.
mwisho aliponea kw wataalam.
mwl yupo kazin na kanisaan anaenda kama kawaid;
 
Kama Mwanga ufifiavyo katika tochi yenye betri afifu,ndivyo na Nguvu ya Mungu ififiavyo kizazi hata kizazi kutokana kufifia kwa imani ya wanadamu kwa Mungu wao alie hai na kupenda giza kuliko Mwanga.

Kwakuwa Mwanadamu amepewa zawadi kuu ya uhuru wa kuchagua jema au baya na kwakuwa Shetani anao uwezo wa kufinyanga kitu kwa nje kikaonekana ni utajiri kumbe ndani ni kama yai bovu,basi mwanadamu anakimbilia mwonekano wa nje.
Biblia inaonyesha halihalisi ya tamaa ya mwanadamu isiyo na subira katika kitabu cha Mwanzo 3:6.
Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.

Hivyo utajiri unaosema au miujiza ya kishetani unayoisema ni kutokana na imani uliyonayo kwa Ibirisi vivyo hivyo ukiwa na imani ya kutosha Kwa Mungu alie hai,utahamisha milima.Barikiwa.
 
Mkuu unamaanisha imani kwa mola inapukutika kwa kasi huku kwa ibirisi inaongezeka kwa kasiii.

Baba tuongezee imani. Waja wako tunawivu tunapoona mchawi anatamba hadi madhabahuni na hakuna mtu wa kumgusa.
 
Mungu ametuumba ili tumjue, tumtumikie ili baadae tuwe pamoja na yeye.
Shetani alikuja ili dhumuni la kujua ni nani anayetenda tofauti na aliyemuumba.
Njia iendeyo Mbinguni ni nyembamba sana, lakini kwa shetani njia ni pana sana kwa kuwa Duniani ndimo ulipo mtihani wa Pepo na Jehanamu ya Moto.
Mara nyingi yote hayo utokea baada ya Binadamu kushindwa kuelewa maisha baada ya kifo.
Ni binadamu wachache sana wenye uelewa wa yajayo baada ya kifo, ingawa wengi wanasema hakuna kitu kama hicho kwani ni lazima kuifurahia Dunia kwa kula raha,starehe za hapa na pale,(Utajiri /Umiliki wa vitu vya thamani, watu n. k)
Hapo ndipo mtego wa Shetani ulipo, kwa kuwa kwake hiyo ndio siraha yake Kuu.
Nitaendelea baadae........... ..Hongera mtoa mada.
 

Ibilisi ni mdanganyifu na mwisho wa mambo yake ni distructions, Mungu is principled, doesnโ€™t force, una hiyari ya kutii ule Mema ya nchi na upate uzima wa Milele au uache!

Watu wengi wanaosema ni wa Mungu hawafanikiwi maana Hakika si wa Mungu ni waongo, na ndo maana wanafanya mambo ya Mungu yazaraulike!
 
aisee inauma sana.
Hadi ibilisi aliyeuweka ugonjwa kaamua kuutoa mwenyewe kwa maslahi yake.

Hii si aibu kwa prayer worriers mkuu.
Hao watu wa Mungu wanajisikiaje wakipata story za mtaalam
 
Kwamba plasmodia wote wanadedi....๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Ulimwengu wote hivi Sasa unatawaliwa na Ibilisi. Hivyo sharti lake kuu kwa mafanikio yako, lazima Uwe upande wake. Short of that, anakuona wewe kizabizabina, na anaweza kukuondoa ukijifamya unataka mafanikio halafu baadaye unamshiti kwa lions masharti yake hayana mashiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ