Kwanini mambo ya kiibilisi hufanikiwa fasta kuliko ya Mungu?

Hakuna kitu kama hicho ila kinachofanyika mambo ya shetani yanajulikana na yanafanyika kwa vitendo na Jambo lolote Ili lifanikiwe lazima ujue kanuni zake na vitendo vyake ufanye ndo unapata matokeo, kama unavyotengeneza kitu alafu utapata matokeo yake huku ukikilinda, sasa kwanini kwa Mungu hatupati matokeo? Kwa vile wale tunaowategemea watuongoze na wao wanatutegemea sisi na hawafanyi kabisa chochote kinachomuhusu Mungu Ili tupate matokeo kama kujitoa kwaajili ya Mungu muda wote na kutogusa dhambi na ilitakiwa tangu utoto wawe hawajagusa dhambi pia wawe na sehemu za kufanya matendo yanayoleta uwepo wa Mungu kwa hatua zake na Mungu angeonekana kama waganga wanavyotengeneza vilinge na kufanya mambo yao na Kwa Mungu hivyo hivyo, na pia kwa mambo ya utajiri Sheria ya Mungu ni moja mtoto ataurithi kwa babaye na yeye atarishisha watoto wake basi utajua kwanini mwanaume kazi kwake ni muhimu sana na ibada njia hiyo ikitumika watu watamtafuta Mungu kwa mambo ya kiroho na siyo kwenda kutafuta mali maana mali anazo baba wa kila mtoto.
 
Mada yako ni ya kufikirisha sana!! yaani ukiyachunguza haya mambo, unaweza hisi Kama vile Mungu ameenda likizo!! yaani mambo ya kishetani ndio yanayolipa! ee Mungu utusaidi tusipotee wanao!! maana mambo yamekuwa magumu sana kwa watu waadilifu!!
 
Nimeguswa na hili andiko saana.

Ila kwakuchangia kulingana na spirital experience yangu,

Mungu bado anafanya vile alikua anafanya zamani tatizo ni pale tunapojaribu kufanya kwa maslai yetu (utukufu)
Na hicho kitu hapendi...

Mfano binafsi ndani ya moyo wangu nataka utajiri ili na Mimi nitambeee niwasomeshe namba... sasa hi si ni Shida??

Nnapojaribu kuponya mtu au kumuombea mtu abarikiwe moyoni natafuta sifa.. ndo mana wenzetu wanakuambia "Mungu was flani" pia ni tatizo.

Ila mara chache nilipotia imani kikamilifu vile vilivyo mbele yangu bila kutegemea palifanyika muujiza kwa kadri nilivyomuomba Mungu.

Hivyo Mungu anaitaji moyo usio na tamaa ya ulimwengu zaidi ya kuwajibika ipasavyo kwa asili na mazingira unayokumbana nayo ktk maisha.
Maana hata shetani alimwambia Yesu amsujudi amkabidhi utajiri was dunia ndo mana kwake kupata ni rahisi maana "chema cha jiuza kibaya chajitembeza"
 

Hilo SoMo la math:4:9-10 limekua likifafanuliwa kwa maana nyingine kabisa shetani anaposema kua hivi vyote Mimi humpa nimtakaye limewapotosha wengi lakini sishangai kwani ndiyo kazi yake kupotosha ili wapotee shetani ni muongo kujalibu kusema kua alisema kweli ni kusema amepoteza sifa ya shetani sifa yake kuu ni uongo ndiyo maana ktk bibilia anaitwa baba wa uongo hakuna kweli itakayo kwake hivyo alipomjalibu yesu na mauongo yake yesu alimpinga kwakua alidanganya kua yeye ndiye hugawia watu Mali kwani bibilia ilidanganya kua Mali zote za dunia ni Mali ya bwana na kua alimpa Mali zote za dunia binamu aliyeumba kwa mfano wake mw:1na 2 avitawale na kuvitiisha kwake binadamu hata Hapo huelewi kua binadamu Alisha kabidhiwa kitambo ? Hebu tupe andiko ambalo shetani naye alikabidhiwa vya duniani ukienda kumomba ambaye hamiliki hicho umuombacho atakulaghai kwa masharti ya uongo hata kufanya Jambo baya shetani alipigwa Chenga kubwa kwani hakumjua yesu kua ndiye Kristi utaona anahoji Kama wewe ni hoja hiyo inaonesha Hana uhakika anajalibu na anakomea kufukuzwa yeye ambaye unatakakusema ni Mali yake vyote viijazayo dunia ni uongo kwani hakuna kweli itakayo kwake
 
Ndugu yangu iko hivi, Mtumishi wa Mungu ni kama mtu tu anayewasha Swichi ya Umeme ukutani. Umeme ukishapata action ya muwashaji upita kwenye nyaya na kwenda kwenye balbu na kuifanya Balbu kuwaka.Kama Nyaya zina shida hutaona Balbu ikitoa mwanga hata ukiwasha mara elfu.

Vivyo hivyo,Mtumishi wa Mungu anapoombea mgonjwa Umeme au Nguvu ya uponyaji lazima ipite kwenye Nyaya zinazoitwa IMANI.Kama Mgonjwa alijengewa au alikulia katika Imani nyingine ,nyaya zake haziwezi kupitisha nguvu ya Nuru .Lakini kama hajiwezi Familia yake inaweza kuomba toba (kumtengenezea System ya nyaya mpya) kwanza kwa ajili yake huku na wao wakiwa na uhakika wana nyaya ambazo hazijachubuliwa au kuliwa na panya.

Vivyo hivyo kwa Mtumishi wa Mungu kabla ya kuomba sharti aangalie system ya wiring yake kama hakuna sehemu itakayozuia Nguvu ya uponyaji kumfikia mgonjwa.Vinginevyo aanze na toba na kujisafisha kwanza ndipo Roho Mtakatifu atashuka kwa neno atakalo litamka kwa IMANI.

Mfano ,huwezi kumwombea Mgonjwa huku nyuma una chuki,husuda,choyo,tamaa,kisasi,kutosamehe n.k. ukategemea Nguvu imfikie Mgonjwa.Hayo ni Mapanya yatakuwa yametafuna nyaya za Imani.Vivyo hivyo kwa Mgonjwa.
 
Hapa unamsema marehemu magufuli pamoja na wateule wake kina sabaya au 😄😄
 
Jibu lipo pale nabii Issa alipopandishwa mlimani na shetani na kuonyeshwa ufalme wote wa dunia. Kwa ufupi mwenye dunia ni shetani, wewe endelea kupasua sala tu ila mwisho wa siku utajikuta unasindikiza wajanja wa hii dunia.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
WE jamaa ni mkali aisee.
Yaani ungekuwa member wa SCOAN ungepewa viatu vya hayati TB.

Nimeelewa hadi raha
 
WE jamaa ni mkali aisee.
Yaani ungekuwa member wa SCOAN ungepewa viatu vya hayati TB.

Nimeelewa hadi raha
 
Ivi mnaposema Mungu humpa mtu mtihani ivi kwamba Mungu muweza wa yote anakuwa ajui huyu mtu ata mtii.
 
WE jamaa ni mkali aisee.
Yaani ungekuwa member wa SCOAN ungepewa viatu vya hayati TB.

Nimeelewa hadi raha
[emoji2][emoji2] Mimi ni mtoto mdogo sana kwa yule Mtumishi wa Mungu Sistahili hata kulinganishwa na watumishi wake.Hekima yake na ufahamu wake kwa maswala ya kiroho ni wa juu sana kwa mtu aliekuwa anamfuatilia atajua nilisemalo.
 
Sema uzuri wa Mungu akikupa amekupa mazima japo lazima usali mpaka goti liote sugu...ila siku akikupa, ni anakupa kitu kizuri mara 100 ya ulichokuwa unaomba

Ishu msoto[emoji848]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Sema uzuri wa Mungu akikupa amekupa mazima japo lazima usali mpaka goti liote sugu...ila siku akikupa, ni anakupa kitu kizuri mara 100 ya ulichokuwa unaomba

Ishu msoto[emoji848]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Akikupa Mungu mkuu ndio ushatoka.ila vya Mungu unakula na raha na amani kama bonus wakati unasherehekea utajiri.

Ila hao jamaa wa ibris nasikia huwa cha moto wanakiona. Akimalizana na watoto wako na mke na mama mkwe mwisho wa siku atataka damu yako kama exchange ya ulivyokula.

Yaani kula uliwe hahaha
 
Jibu lipo pale nabii Issa alipopandishwa mlimani na shetani na kuonyeshwa ufalme wote wa dunia. Kwa ufupi mwenye dunia ni shetani, wewe endelea kupasua sala tu ila mwisho wa siku utajikuta unasindikiza wajanja wa hii dunia.
Unataka kusema MUNGU na mwanadamu wameporwa dunia na shetani amejimilikisha amewazidi nguvu au ujanja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…