Hao wazungu wachache ndio wanamiliki ardhi na nafasi za ajira. Uliwahi ona Waafrika Kusini wanakimbia nchi yao kuja kuzamia Tanzania kutafuta ajira ambapo ardhi inamilikiwa na sisi wazawa tunaomiliki majaruba 20 kwenye kakipande huku tunatifua kwa jembe la mkono?
Wabongo ndio wanakimbilia Afrika Kusini kufanya umachinga, wizi, madawa na kuwa vinyozi. Afrika Kusini inabeba wahamiaji wa Zimbabwe, Zambia, Tanzania, Malawi, Mozambique na bado inaishi.
Hao wazungu unaolalamikia ndio mfano wakulima wadogo wa matunda waliungana kuunda kampuni ya Ceres, unaziona juisi zao kwenye supermarkets zetu
View attachment 2964951
Wakati sisi wabongo wanaungana kutengeneza matawi ya Simba na Yanga almost kila kata jijini Dar na maeneo nchi nzima
View attachment 2964952
Hutokaa usikie wakulima wadogo wa mawese Kigoma waungana kujenga kinu kidogo cha kukamua mazao yao. Utasikia kila siku wanaomba serikali, Samia, Makonda. Na Afrika Kusini husikii wazungu wanalialia juu ya serikali, hizo ni kazi za wacheza amapiano ambao ndio hupiga kura. Mzungu anabaguliwa baadhi ya vitu kama nafasi za kisiasa na amekubali, vitu vingi anajifanyia yeye.
View attachment 2964951View attachment 2964952View attachment 2964951View attachment 2964952