Kwanini mapepo, majini, wachawi na roho wabaya wote humwogopa YESU KRISTO

Vipi kuhusu waasi wa kongo wao hawamwogopi yesu?

Vipi magonjwa kama ukimwi,makaria,covid,nk hayamwogopi yesu?

Acha ujinga na badilika huu siyo wakati wa kukumbatia upumbavu wa hadithi za kijinga,huyo yesu amalize vita na magongwa kote duniani basi?
Tatizo linalo waangamiza wanadamu ni kudharau elimu.
 
Yanawapata wakristo tu au yapo kwa ajili ya wakristo tu?
Mara nyingi ukiwa upande wa dhambi hayawezi kukusumbua kwasababu upo ndani ya ufalme wao. Tusome kila elimu tatizo vijana wakisoma biology wakishiba wanadhani wamemaliza kila kitu na wanaelewa kila kitu.
 
Yesu sawa!

Ila pia yanawaogopa matajiri. Ni makabwela tu ndo upatwa na mapepo na kutoa shuhuda majukwaani
Asilimia kubwa ya matajiri wapo upande wa ibirisi hayawezi kuwasumbua. Embu mchukue tajiri alafu mpeleke kanisani waanze kumwombea ili abadili ufalme, uone kama hayataanza kuruka mapepo.
 
Asilimia kubwa ya matajiri wapo upande wa ibirisi hayawezi kuwasumbua. Embu mchukue tajiri alafu mpeleke kanisani waanze kumwombea ili abadili ufalme, uone kama hayataanza kuruka mapepo.
We umejuaje wapo upande wa ibirisi? Na huyo ibirisi ni nani kwani?
 
We umejuaje wapo upande wa ibirisi? Na huyo ibirisi ni nani kwani?
Elimu ni chanzo cha maarifa. Hapa duniani unadhani unaishi peke yako. Kuna viumbe wengi sana wanaishi hapa duniani. Kama vile ambavyo huwezi kumwona bacteria, au kirusi anaye leta magonjwa basi ndio hivyo hivyo huwezi kuwaona viumbe wengine wanao ishi duniani.
 
Jesus Christ my warrior💪
 
Kwanini huwa makanisa ya kiroho hayafunguliwi karibu na mahospitali? Waweke maspika watu wapone.
Unalijua kanisa la EAGT pale mwanza Bugando? Alikolala askofu Moses Kulola?
 
Unalijua kanisa la EAGT pale mwanza Bugando? Alikolala askofu Moses Kulola?
Wana maspika nje yanayoimba usiku mzima kufukuza mapepo kama hawa wa mitaani?
 
Wana maspika nje yanayoimba usiku mzima kufukuza mapepo kama hawa wa mitaani?
Kwanini huwa makanisa ya kiroho hayafunguliwi karibu na mahospitali?

Hilo ndilo swali lako na nimekujibu vyema
 
Reactions: Tsh
Kwanini huwa makanisa ya kiroho hayafunguliwi karibu na mahospitali?

Hilo ndilo swali lako na nimekujibu vyema

Kwa kuongezea:

Injili haihubiriwa kwa ajili ya wagonjwa pekee bali kwa ajili ya watu wote ili kuwaleta kwenye nuru ya Kristo na kuwaondoa kutoka kwenye giza la dhambi, mateso ya kiroho, na vifungo vya maisha bila Mungu.

Yesu alisema:
"Roho ya Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema; amenituma kuponya waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru walioteswa." (Luka 4:18)

Kwa hiyo kazi za msingi za kanisa ni pamoja na:

1. Kuweka amani ndani ya mioyo ya watu

2. Kufundisha uvumilivu, upendo, ustahimilivu

3. Kuongoza watu kufuata sheria na maadili ya Mungu

4. Kuhimiza kusameheana na kujenga mshikamano

5. Kuwa kituo cha faraja kwa waliovunjika moyo

6. Kuleta uzima wa milele, siyo tu uponyaji wa mwili

Hospitali hutoa huduma ya mwili. Madaktari na wauguzi hutumia elimu na vifaa tiba kuponya magonjwa ya mwilini. Lakini kanisa linashughulika na huduma ya roho, akili, na maadili huduma inayogusa ndani kabisa ya mwanadamu. Hivyo, kanisa linaweza kujengwa mahali popote, si lazima liwe karibu na hospitali, kwa sababu huduma yake ni ya kipekee na pana zaidi: linafundisha watu kutubu dhambi, kuishi kwa amani, kusameheana, na kumtafuta Mungu kwa moyo wote.

Wagonjwa huombewa si kwa sababu hospitali hazitoshi, bali kwa sababu afya ya kweli huanzia rohoni. Maombi ni ishara ya kumtegemea Mungu, ambaye ndiye mponyaji wa mwisho wa mwili na roho. Kuna magonjwa ambayo tiba za dunia hushindwa, lakini nguvu ya maombi na imani huweza kuleta uponyaji wa miujiza, faraja kwa waliovunjika moyo, na tumaini la maisha mapya hata kama mwili haufanyi kazi. Hili ndilo linalofanya huduma ya kiroho kuwa muhimu zaidi, si mbadala wa hospitali bali kiungo cha ukamilifu wa uzima.
 
Roho mbaya ninazoziona kila siku Tz, ni wizi, uchawi, ubabe kwa maisha WaTz, kutesana, kutekana kuuana! Wanaofanya uovu huu wanajazana kanisani!
 
Roho mbaya ninazoziona kila siku Tz, ni wizi, uchawi, ubabe kwa maisha WaTz, kutesana, kutekana kuuana! Wanaofanya uovu huu wanajazana kanisani!
Ukiona wapo kanisani basi ujue hilo kanisa halifundishi habari za Yesu.
 
Kwanini huwa makanisa ya kiroho hayafunguliwi karibu na mahospitali?

Hilo ndilo swali lako na nimekujibu vyema
Ooh, upo sahihi, nilipaswa kuuliza kwanini hayafunguliwi karibu na mahospitali wakaweka maspika wagonjwa wapone.
 
Ooh, upo sahihi, nilipaswa kuuliza kwanini hayafunguliwi karibu na mahospitali wakaweka maspika wagonjwa wapone.
Kwann hao wagonjwa wao wasiende kufata hayo maspekear wapone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…