Kwanini mapepo, majini, wachawi na roho wabaya wote humwogopa YESU KRISTO

Kwanini huwa makanisa ya kiroho hayafunguliwi karibu na mahospitali? Waweke maspika watu wapone.
Injili haihubiriwa kwa ajili ya wagonjwa pekee bali kwa ajili ya watu wote ili kuwaleta kwenye nuru ya Kristo na kuwaondoa kutoka kwenye giza la dhambi, mateso ya kiroho, na vifungo vya maisha bila Mungu.

Yesu alisema:
"Roho ya Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema; amenituma kuponya waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru walioteswa." (Luka 4:18)

Kwa hiyo kazi za msingi za kanisa ni pamoja na:

1. Kuweka amani ndani ya mioyo ya watu

2. Kufundisha uvumilivu, upendo, ustahimilivu

3. Kuongoza watu kufuata sheria na maadili ya Mungu

4. Kuhimiza kusameheana na kujenga mshikamano

5. Kuwa kituo cha faraja kwa waliovunjika moyo

6. Kuleta uzima wa milele, siyo tu uponyaji wa mwili

Hospitali hutoa huduma ya mwili. Madaktari na wauguzi hutumia elimu na vifaa tiba kuponya magonjwa ya mwilini. Lakini kanisa linashughulika na huduma ya roho, akili, na maadili huduma inayogusa ndani kabisa ya mwanadamu. Hivyo, kanisa linaweza kujengwa mahali popote, si lazima liwe karibu na hospitali, kwa sababu huduma yake ni ya kipekee na pana zaidi: linafundisha watu kutubu dhambi, kuishi kwa amani, kusameheana, na kumtafuta Mungu kwa moyo wote.

Wagonjwa huombewa si kwa sababu hospitali hazitoshi, bali kwa sababu afya ya kweli huanzia rohoni. Maombi ni ishara ya kumtegemea Mungu, ambaye ndiye mponyaji wa mwisho wa mwili na roho. Kuna magonjwa ambayo tiba za dunia hushindwa, lakini nguvu ya maombi na imani huweza kuleta uponyaji wa miujiza, faraja kwa waliovunjika moyo, na tumaini la maisha mapya hata kama mwili haufanyi kazi. Hili ndilo linalofanya huduma ya kiroho kuwa muhimu zaidi, si mbadala wa hospitali bali kiungo cha ukamilifu wa uzima.
 
Kwa mujibu wa kipimo cha nguvu za kiroho kinaitwa ACDs.
Mwanadamu ana nguvu za kiroho kipimo cha 1.5
Jini ana 2.5
Makamanda au majemedari watano wa shetani Wana 3.5
Shetani ana 4.
Jesus ana 💯 %
Kumshinda mchawi,pepo,jini,au shetani inategemea na wewe ulivyojiconnect na Jesus power kwa asilimia ngapi.
Mchawi yeyeto hawezi kukudhuru bila kupima kwanza nguvu zako za kiroho kwa kutumia testa maana nao Wana Roho uogopa kufa wakiingia vibaya
 
Mara nyingi ukiwa upande wa dhambi hayawezi kukusumbua kwasababu upo ndani ya ufalme wao. Tusome kila elimu tatizo vijana wakisoma biology wakishiba wanadhani wamemaliza kila kitu na wanaelewa kila kitu.
Huwa mna ujinga wa kufarijiana mambo ya kipumbavu hasa kwenye kukwepa ukweli yaani ukiwa upande wa dhambi mapepo haywezi kukusumbua,kweli una akili wewe mpimbavu nini??unalazimisha uongo kusimama kweli?
 
Tembelea hospitali mara moja moja kuwajulia hali wagonjwa na utajua kwanini hawaendi boss.
Uponyaji ni ishu ya imani imani ni kuruhusu nguvu za uponyaji zitende miujiza ndani mwako
 
Injili haihubiriwa kwa ajili ya wagonjwa pekee bali kwa ajili ya watu wote ili kuwaleta kwenye nuru ya Kristo na kuwaondoa kutoka kwenye giza la dhambi, mateso ya kiroho, na vifungo vya maisha bila Mungu.

Yesu alisema:
"Roho ya Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema; amenituma kuponya waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru walioteswa." (Luka 4:18)

Kwa hiyo kazi za msingi za kanisa ni pamoja na:

1. Kuweka amani ndani ya mioyo ya watu

2. Kufundisha uvumilivu, upendo, ustahimilivu

3. Kuongoza watu kufuata sheria na maadili ya Mungu

4. Kuhimiza kusameheana na kujenga mshikamano

5. Kuwa kituo cha faraja kwa waliovunjika moyo

6. Kuleta uzima wa milele, siyo tu uponyaji wa mwili

Hospitali hutoa huduma ya mwili. Madaktari na wauguzi hutumia elimu na vifaa tiba kuponya magonjwa ya mwilini. Lakini kanisa linashughulika na huduma ya roho, akili, na maadili huduma inayogusa ndani kabisa ya mwanadamu. Hivyo, kanisa linaweza kujengwa mahali popote, si lazima liwe karibu na hospitali, kwa sababu huduma yake ni ya kipekee na pana zaidi: linafundisha watu kutubu dhambi, kuishi kwa amani, kusameheana, na kumtafuta Mungu kwa moyo wote.

Wagonjwa huombewa si kwa sababu hospitali hazitoshi, bali kwa sababu afya ya kweli huanzia rohoni. Maombi ni ishara ya kumtegemea Mungu, ambaye ndiye mponyaji wa mwisho wa mwili na roho. Kuna magonjwa ambayo tiba za dunia hushindwa, lakini nguvu ya maombi na imani huweza kuleta uponyaji wa miujiza, faraja kwa waliovunjika moyo, na tumaini la maisha mapya hata kama mwili haufanyi kazi. Hili ndilo linalofanya huduma ya kiroho kuwa muhimu zaidi, si mbadala wa hospitali bali kiungo cha ukamilifu wa uzima.
Wagonjwa wanahitaji uponyaji. Wazima tunaweza tembelea makanisani kuipata injili. Si normal logic hii?
 
Huwa mna ujinga wa kufarijiana mambo ya kipumbavu hasa kwenye kukwepa ukweli yaani ukiwa upande wa dhambi mapepo haywezi kukusumbua,kweli una akili wewe mpimbavu nini??unalazimisha uongo kusimama kweli?

Ni kweli kabisa ukiwa upande wa dhambi, unakuwa kwenye uwanja wa mapepo yanakua yanakutesa hata kama huoni au huhisi na huwezi kuhisi kama huna akili za kiroho. Wanadamu wengi wanatumia akili za ubongo na moyoni. Lakini nakwambia kuna akili za ubongo, rohoni na moyoni. Biblia inasema:

“Yeye atendaye dhambi ni wa Ibilisi, kwa kuwa Ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo.” (1 Yohana 3:8)

Hii ina maana kwamba mtu anapoendelea kuishi katika dhambi, anajifungulia milango kwa nguvu za giza. Hata kama mapepo hayaonekani kwa macho, yanaweza kusababisha mateso ya kiakili, kiroho, na hata kimwili.

Lakini pia, lengo la Yesu halikuwa la kumshutumu tu mwenye dhambi, bali kumpa njia ya kutubu na kuponywa.

“Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.” (Luka 5:32)

Kwa hiyo, hakuna sababu ya kufarijiana kwa uongo na wala si sahihi kuhalalisha dhambi. Lakini pia hatupaswi kukatisha tamaa wale wanaohitaji huruma ya Mungu. Kweli inapaswa kusemwa, kwa nguvu na kwa upendo, kama Yesu alivyoifanya.
 
Uponyaji ni ishu ya imani imani ni kuruhusu nguvu za uponyaji zitende miujiza ndani mwako
Wachungaji wanapougua wanapoteza imani? Kwanini wanaacha maspika ya uponyaji kwa kelele za juu na kukimbilia hospitali pasipo na maspika ya injili?

Tuelimishane mkuu, haya ni maswali watu wa injili wanakutana nayo field. Ukijibu vyema utamsaidia mwinjilisti atakayesoma na kukutana nalo field.
 
Wagonjwa wanahitaji uponyaji. Wazima tunaweza tembelea makanisani kuipata injili. Si normal logic hii?
Ni kweli wagonjwa wanahitaji uponyaji, lakini je, unadhani mwili pekee ndio unaweza kuugua? Kuna watu wanaonekana wazima lakini wamejaa majeraha ya roho: huzuni, chuki, dhambi, msamaha wa ndani, upweke, na mateso ya kiakili. Injili ni tiba kwa haya yote. Ndiyo maana makanisa hayapo tu kwa ajili ya wagonjwa wa mwili, bali kwa ajili ya kila mtu mzima au mgonjwa anayeihitaji kweli ya Mungu. Kwa hiyo, siyo ‘wagonjwa hospitali na wazima kanisani’, bali wote wanahitaji Injili popote walipo.
 
Wachungaji wanapougua wanapoteza imani? Kwanini wanaacha maspika ya uponyaji kwa kelele za juu na kukimbilia hospitali pasipo na maspika ya injili?

Tuelimishane mkuu, haya ni maswali watu wa injili wanakutana nayo field. Ukijibu vyema utamsaidia mwinjilisti atakayesoma na kukutana nalo field.
Kuna aina mbili za magonjwa ya kiroho na ya kimwili ya kimwili utibika hospitalini ya kiroho hayatibiki hospital
 
Ni kweli wagonjwa wanahitaji uponyaji, lakini je, unadhani mwili pekee ndio unaweza kuugua?
Maombi hayana msaada kwenye kuugua mwili?
Kuna watu wanaonekana wazima lakini wamejaa majeraha ya roho: huzuni, chuki, dhambi, msamaha wa ndani, upweke, na mateso ya kiakili. Injili ni tiba kwa haya yote. Ndiyo maana makanisa hayapo tu kwa ajili ya wagonjwa wa mwili, bali kwa ajili ya kila mtu mzima au mgonjwa anayeihitaji kweli ya Mungu. Kwa hiyo, siyo ‘wagonjwa hospitali na wazima kanisani’, bali wote wanahitaji Injili popote walipo.
Swali langu limejikita kwenye uponyaji wa kimwili si wa kiroho, tumeshuhudia vilema wakitembea kwenye TV, watu wakipona HIV, Kansa.
 
Kuna aina mbili za magonjwa ya kiroho na ya kimwili ya kimwili utibika hospitalini ya kiroho hayatibiki hospital
Hawa tunaowashuhudia wakipona HIV huwa ni HIV ya kiroho?
 
Ni kweli wagonjwa wanahitaji uponyaji, lakini je, unadhani mwili pekee ndio unaweza kuugua? Kuna watu wanaonekana wazima lakini wamejaa majeraha ya roho: huzuni, chuki, dhambi, msamaha wa ndani, upweke, na mateso ya kiakili. Injili ni tiba kwa haya yote. Ndiyo maana makanisa hayapo tu kwa ajili ya wagonjwa wa mwili, bali kwa ajili ya kila mtu mzima au mgonjwa anayeihitaji kweli ya Mungu. Kwa hiyo, siyo ‘wagonjwa hospitali na wazima kanisani’, bali wote wanahitaji Injili popote walipo.
Wachungaji huwa hawapotezi imani wanapougua wala hawakimbii injili wanapokwenda hospitali. Wanatumia hekima ya kiroho na ya kawaida kwa wakati mmoja. Maandiko yanasema:

“Hekima ni ulinzi kama vile fedha ilivyo ulinzi; lakini faida ya maarifa ni hii, kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.” (Mhubiri 7:12)

Hospitali si kinyume cha imani, bali ni sehemu ya maarifa ambayo Mungu mwenyewe ameruhusu binadamu awe nayo ili kusaidia miili yetu. Daktari mzuri, dawa, au upasuaji ni chombo tu lakini mponyaji wa kweli ni Mungu. Biblia haisemi “usitumie daktari”, bali hata Luka mwenyewe alikuwa daktari (Wakolosai 4:14).

Maspika ya uponyaji ni kwa ajili ya kuhubiri kweli ya Injili kwa watu wote si kwa ajili ya kuwazuia wachungaji kwenda hospitali. Kuwa na imani hakumaanishi kupuuzia njia ambazo Mungu ameziruhusu kwa uponyaji wa mwili.

Yesu mwenyewe alisema:

“Wagonjwa ndio wanaohitaji tabibu.” (Marko 2:17)

Na Paulo alimwacha Trofimo akiwa mgonjwa huko Mileto (2 Timotheo 4:20), hakumlazimisha abaki tu kwa maombi. Hii inaonesha kuwa hata mitume walitambua kuwa uponyaji unaweza kuwa wa kiroho au wa kawaida au vyote kwa pamoja.

Kwa hiyo;

1. Imani haipingani na tiba, bali imani huweka msingi wa tumaini katika mponyaji halisi wa Mungu.

2. Hospitali ni sehemu ya rehema ya Mungu kwa wanadamu, na imani haimaanishi kudharau tiba.

3. Mhubiri au mchungaji anayekwenda hospitali hajakimbia imani anaonyesha kuwa Mungu hutenda kazi kwa njia nyingi.

4. Maspika ni chombo cha uinjilisti si ishara ya kudharau hospitali.
 
Ni kweli kabisa ukiwa upande wa dhambi, unakuwa kwenye uwanja wa mapepo yanakua yanakutesa hata kama huoni au huhisi na huwezi kuhisi kama huna akili za kiroho. Wanadamu wengi wanatumia akili za ubongo na moyoni. Lakini nakwambia kuna akili za ubongo, rohoni na moyoni. Biblia inasema:

“Yeye atendaye dhambi ni wa Ibilisi, kwa kuwa Ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo.” (1 Yohana 3:8)

Hii ina maana kwamba mtu anapoendelea kuishi katika dhambi, anajifungulia milango kwa nguvu za giza. Hata kama mapepo hayaonekani kwa macho, yanaweza kusababisha mateso ya kiakili, kiroho, na hata kimwili.

Lakini pia, lengo la Yesu halikuwa la kumshutumu tu mwenye dhambi, bali kumpa njia ya kutubu na kuponywa.

“Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.” (Luka 5:32)

Kwa hiyo, hakuna sababu ya kufarijiana kwa uongo na wala si sahihi kuhalalisha dhambi. Lakini pia hatupaswi kukatisha tamaa wale wanaohitaji huruma ya Mungu. Kweli inapaswa kusemwa, kwa nguvu na kwa upendo, kama Yesu alivyoifanya.
Biblia haiwezi kusema hata siku moja bali biblia imeandikwa kuwasemea wajanja ili kuwakamata wajinga kama wewe ni sawa na sungura akasema,wapumbavu ndiyo mnaoamini kuwa biblia inasema kwa mistari
 
Kimwili na kiroho hiv ipo
Tukae kwenye kimwili, halafu baadae kiroho.

Rejea swali la awali, kwanini huu mfumo hautumiki mahospitalini? Yafungwe maspika usiku mzima kwa sauti ya juu uponyaji umwagike hadi ICU.
 
Kwan wagonjwa wote Wana nguvu ya Imani sawa.
 
Maombi hayana msaada kwenye kuugua mwili?

Swali langu limejikita kwenye uponyaji wa kimwili si wa kiroho, tumeshuhudia vilema wakitembea kwenye TV, watu wakipona HIV, Kansa.

Maombi yana msaada mkubwa sana kwenye kuugua mwili. Mungu anaponya.

Katika Biblia na hadi leo, maombi yamekuwa njia halali ya kupokea uponyaji wa kimwili. Mungu hajasema kwamba uponyaji wa kimwili ni wa madaktari pekee. Hata madaktari wanaweza kushindwa, lakini maombi hayashindwi kufika kwa Mungu.

1. Biblia Inathibitisha Uponyaji kwa Maombi:

Yakobo 5:14-15:

"Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa, na waombe juu yake, wakimtia mafuta kwa jina la Bwana. Na maombi ya imani yatamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana atamwinua."

Yesu mwenyewe aliponya magonjwa ya mwili bila dawa:

Kipofu, bubu, wenye ukoma, mama aliyekuwa anatokwa na damu miaka 12, mwana wa mlinzi wa kifalme, na wengine wengi.

2. Ushuhuda wa Kisasa Unathibitisha:

Tumeshuhudia watu wakipona:

Kansa, bila chemotherapy

HIV, bila ARVs

Kulemaa, na sasa wanatembea

Shinikizo la damu, kisukari, kifafa, na mengine kwa njia ya maombi ya imani na si dawa peke yake

Hii si hadithi. Kuna rekodi za hospitali zilizoshuhudia kwamba mtu aliyeonekana hana tumaini, alirudi na vipimo vipya vilivyoonyesha kwamba amepona baada ya maombi.

3. Kwanini Wengine Hawaponi Hata Wakisali?

Hii haimaanishi kwamba kila mtu atapona mara moja. Sababu zinaweza kuwa:

Mapenzi ya Mungu: Mungu anaweza kutumia ugonjwa kama sehemu ya kumtengeneza mtu kiroho au kuwafundisha wengine

Imani isiyo kamili au maombi yasiyo na bidii

Ugonjwa wa kifo au adhabu ya kiroho (kama kwa Herode – Matendo 12:23)

Lakini ukweli unabaki palepale: Mungu anaponya, na maombi yana nguvu katika uponyaji wa mwili.

Hivyo maombi si ya kiroho tu, bali ni silaha ya uponyaji wa kimwili pia.
Kama Yesu aliwaponya walio lemewa kimwili, basi na leo anaweza na bado anaponya.

Maombi ni dawa ya mbinguni ambayo haiwezi kununuliwa na haina madhara ya pembeni. Na wakati mwingine, ni maombi ndiyo dawa ya mwisho unapofika mwisho wa hospitali.
 
Back
Top Bottom