Kwanini Marekani imewazidi Mexico kwa mbali sana tofauti na Ujerumani inavyotaka kulingana na Ufaransa ilhali hizo zote sio nchi za ndani ya Afrika?

Kwanini Marekani imewazidi Mexico kwa mbali sana tofauti na Ujerumani inavyotaka kulingana na Ufaransa ilhali hizo zote sio nchi za ndani ya Afrika?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Kwanini Marekani imewazidi jirani yao Mexico kwa mbali sana tofauti na Ujerumani inavyotaka kulingana na jirani yao Ufaransa ilhali hizi zote ni nchi za wazungu (The Whites)?

View attachment 1605845

Je, ushahidi huu ni udhibitisho mwingine tena wa ule msemo/dhana maarufu ya kwamba kuishi karibu na mahakama sio kujua sheria kwa maana nchi ya Mexico ipo karibia kabisa na mahakama (Marekani) lakini bado sio wabobezi wa sheria (Global Influence) tofauti na Wafaransa wanavyojitahidi kutaka kulingana na Wajerumani.

Kwanini utofauti ni mkubwa hivi na hawa wote ni rangi nyeupe?

Kwa kipindi cha muda mrefu sana kumekuwapo na dhana sijui niseme ni kasumba ya kuamini kwamba ukikaa karibu na mzungu basi wewe ndio umefanikiwa. Tazama maendeleo ya nchi kama South Afrika ukilinganisha na jirani zao wa Msumbiji waliojawa na umasikini wa kutupwa.

Asilimia kubwa ya watu wanaamini ya kwamba maendeleo yale ya vitu yametokana na wao kukumbatia wazungu waliokuwapo nchi ile enzi na enzi pamoja na uamuzi wa mzee Madiba wa kutotaka kuwafukuza punde baada ya kumalizika kwa utawala wa kikaburu (Apatheid Regime)

Tukirudi hapa nyumbani kwetu Tanzania, moja kati ya sera za baba wa taifa Mwalimu Julius Nyarere ambazo baadhi ya wanazuoni wamekuwa wakizikosoa kwa nguvu zote na kudai ya kwamba ndio chanzo kikuu cha Tanzania kutokuwa na uchumi kama wa South Afrika ni ile ya kuwafukuza wazungu nikiwa na maana kwamba aliwafukuza kwa kufuta lugha ya kiingereza kama medium of instruction katika taasisi zetu za elimu ya msingi pamoja na utaifishwaji wa mali zao.

Achilia mbali sera za Mwalimu Nyerere pamoja na Makaburu wa South Afrika, bali turudi huku uswahilini kwetu tunapokaa. Just imagine leo hii umepita ukiongozana na mzungu barabarani huku uswahilini tunapokaa, unafikiri watu watasemaje. Lazima viji maneno vitambae utasikia daaaah yule jamaa si ndio Infantry Soldier.

Yule si ndio hapa juzi alikuwa analialia eti ameangusha pesa yake 300,000/= ya rambirambi ila leo anaongozana na wazungu hakika ametoboa kimaisha. Kwanini hii dhana ya mafanikio huletwa ukaapo na mzungu imekuwa si halisi kwa Mexico?

SWALI LA KIZUSHI: Je, ni mara ngapi uliwahi kukataa kupiga picha na mzungu? (Kuwa Mkweli)

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Mdogo wangu kinachoisibu Mexico ni uhalifu uliokidhiri bangi na madawa ya kulevya
 
They are WHITES and Africans are BLACK...
hapana mexican are not white...South american mexico included ni masalio ya waafrika na mataifa ya hapo kama wa inca,wa aztec..marekani ni zao la watu wa ulaya sana na nchi nyengine ..usiconfuse
 
mexico si wakuwabeza mkuu maana wapo nafasi ya 15 kiuchumi dunia pia wapo kwenye G20.
Mkuu, hizo Gs wala zisikuchanganye sana mara sijui G5 tena G25, mbona hata tukianzisha G120 na sisi Tanzania tutakuwepo.
 
Mkuu, gizo Gs wala zisikuchanganye sana mara sijui G5 tena G25, mbona hata tukianzisha G120 na sisi Tanzania tutakuwepo.
mkuu unadhani kua wa 15 kiuchumi duniani ni kazi ndogo? hawa mabwana wapo vizuri japo wamezidiwa mbali na marekani
 
Mimi ninamaanisha weupe ambao ni opposite na weusi na sio weupe huo wa kung'aa yaaani weupe peeeeee...
Unamaanishaje kitu ambacho hakipo.Unafahamu kuwa Aboriginal na sisi waafrika ni rangi mbili tofauti kabisa.Vipi mwarabu na mchina wawe saw a.Ina maana nadharia ya races haipo. Kwa hio warangi na wanyiramba,wachaga nk utawaweka kundi gani.Watu tupo tofauti hata waafrika tu tupo tofauti sana.M sokhsa was south na mzuru ni ranging mbili tofauti.It seems unaupungufu wa uelewa wa human races.Your hypothesis is very vague!
 
Unamaanishaje kitu ambacho hakipo.Unafahamu kuwa Aboriginal na sisi waafrika ni rangi mbili tofauti kabisa.Vipi mwarabu na mchina wawe saw a.Ina maana nadharia ya races haipo. Kwa hio warangi na wanyiramba,wachaga nk utawaweka kundi gani.Watu tupo tofauti hata waafrika tu tupo tofauti sana.M sokhsa was south na mzuru ni ranging mbili tofauti.It seems unaupungufu wa uelewa wa human races.Your hypothesis is very vague!
Piga kelele zooooote unazozijua wewe lakini duniani kuna rangi mbili tu za binadamu yaaani MWEUPE na MWEUSI.

Labda kama wewe ni binadamu wa njano au blue.
 
Light skin and white people are two different people. Kiswahili hakina misamiati ya kutosha ya kutofautisha watu.Waafrika weupe huko ulaya huitwa black au light skin.Hao Mexico, Wajapan no ni light skin but not white.Hats ulaya yenyewe kuna badhi ya nchi wazungu weupe huwa hawawatambui kama white.Mfano Ureno, Italy, Spain,greece sion White people.White are Arien people ambao in UK,Germany France nk
 
Unamaanishaje kitu ambacho hakipo.Unafahamu kuwa Aboriginal na sisi waafrika ni rangi mbili tofauti kabisa.Vipi mwarabu na mchina wawe saw a.Ina maana nadharia ya races haipo. Kwa hio warangi na wanyiramba,wachaga nk utawaweka kundi gani.
Kujifanya mjuaji sana hakukupeleki popote mkuu. Sasa wewe chukua hao Latino kisha nenda nao Mbagala alafu kawaambie watu kuwa hawa sio watu weupe kama haujapigwa mawe...
 
Piga kelele zooooote unazozijua wewe lakini duniani kuna rangi mbili tu za binadamu yaaani MWEUPE na MWEUSI.

Labda kama wewe ni binadamu wa njano au blue.
Kwa uelewa wako but not books(facts).Usilazimishe uelewa wako ukawa uelewa wa jumla/Ukweli.Uelewa wako ni common sense na uelewa unaokubalika ni facts.Kuwa layman ktk jambo sio vibaya vibaya ni kuukataa ukweli unaokubalika.Fanya andiko ili upinge nadharia zilizopo zinazobainisha watu. Unaoneka huwezi kujenga hoja bali kulazimisha tu bila evidence.Hata babu zetu wenyewe waliwatofautisha watu weupe kwa majina tofauti ; Wazungu,wahindi,wabaniani,singasinga nk wewe unakuja na utopia.Napoteza mda bure sikujibu tena.
 
Kwa uelewa wako but not books(facts).Usilazimishe uelewa wako ukawa uelewa wa jumla/Ukweli.Uelewa wako ni common sense na uelewa unaokubalika ni facts.Kuwa layman ktk jambo sio vibaya vibaya ni kuukataa ukweli unaokubalika.Fanya andiko ili upinge nadharia zilizopo zinazobainisha watu. Unaoneka huwezi kujenga hoja bali kulazimisha tu bila evidence.
Sasa wewe chukua hao Latino kisha nenda nao Mbagala alafu kawaambie watu kuwa hawa sio watu weupe kama haujapigwa mawe...
 
Back
Top Bottom