Kwanini matukio ya Ngono za Kuagana kabla ya Harusi yanashika kasi Tanzania?

Tatizo kubwa ni umasikini,ukikutana na binti anatoka familia ya kipato cha juu kwa asilimia kubwa unaounguza huo ujinga.
Masikini ana tamaa vibaya sana,masikini hana dhamana.
Ongezea na kigezo cha kukosa akili. Mwanamke smart hawezi hata kufanya mawasiliano na ex huku akiwa ktk mchakato wa kuolewa na mwanaume mwingine.
 
Mama huwa anasema madhaifu ya baba ila baba kamwe hasemi madhaifu ya mama ndio maana tunawaona mama zetu ni malaika..

Kilichoongezeka ni kiwango tu ila hakuna jipya
 
Inasikitisha sana ,sasa kama alikuwa anampenda huyo ex wake kwanini alitaka kufunga ndoa na mtu mwingine? Hapo kama mimi ndiyo huyo mwanamme ndiyo basi hakuna ndoa hapo ni kurudi nyumbani na kuanza safari upya kila mtu na 50 zake.
 
Dah itamchukua miezi jamaa kuwa sawa kiakili,na itamchukua zaidi ya miaka tena huyo jamaa kuja kuoa.
Ukisikia maumivu ndio hayo sasa,unaweza kuua.
Yote mawili,kuumia au kuua ni uzembe!. Badala ya kumshukuru Mungu umejua uliyopaswa kuyajua mapema sasa uumie nini?. Tujifunze kuwa positive minded😀
 
Ukute ndo ametumika pande zote, harafu ukumbini njemba lipo na linakuchora TU unavyokwenda kunenpesha mbuzi WA wake nayeye aendelee kukamua TU.
 
Wanaume wote ni masimp kwa wanawake wanaowapenda ni vile kelele nyingi jukwaani lakini kwa ground vinalia kama vitoto vya ndege..!! 😹😹
Ukweli mchungu, kwenye wimbo wa diamond wa holiday kuna mstari anasema "we unagharamikia na kuna baharia anakula bure" mimi naongezea hata huyo baharia anaemla bure demu wako unaemuhonga, na yeye kuna sehemu anagharamikia na kuhonga balaa..

Mwanaume ukiwa mjanja kwa demu huyu, utakua boya kwa demu mwingine, haya mambo hayana mbabe Lamomy
 
Kwanini sasa
Anaamini wanaume wengi wana trauma ya bad relationship kama ambayo mwanaume anayetajwa kwenye huu uuzi huenda ameipata kupitia tukio alilopigwa na mke wake mtarajiwa. Mimi naamini ni wanaume wachache wana trauma ya kweli inayotokana na mapenzi. Matukio ya mwanamke kumpiga event mwanaume si mengi kama yalivyo matukio ya mwanaume kumpiga matukio mwanamke. Na hii inachangiwa na advantages nyingi zaidi za kibaiolojia, kiuchumi, na za kimila na desturi alizonazo mwanaume ukilinganisha na mwanamke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…