Kwanini Mbezi beach imepoteza umaarufu wake iliyokuwa nao miaka ya nyuma?

Tangi Bovu tumelikuta bovu hivyo hivyo lina kutu.

Pale kulikuwa na mashamba, shamba la bibi yangu lilikuwa upande wa pili hapo palipokuwa na Tangi Bovu.

Hivyo inaonekana lilitumika katika kuhudumia nyumba ya shambani.
Kwa komba??? Wale mateja pale nyuma hiv serikali huwa haiwaoni au ni vipi etiiii
 
Ndiyo mitaa hiyo, hao mateja sijawaona niliondoka bado pana heshima, ila kwa Mbezi Beach ya sasa siwezi kushangaa stories za mateja.
Kuna yale mabanda pale karibia na efm kwa majizzo, hivi ni mradi wa mtu ule ama nini??? Mana pembeni ni mijengo ya maana ila yale mabanda duuuh, tena yamejengwa kwa mabati kabisaaa full kuanzia ukuta mbka paa...mbezi beach kuna sehemu znachekesha sana
 
Ila mbweni kuna mijengo, jaman watu wana helaa.
Nliwahi enda nyumba 1 hiv kwenye rehearsal ya dance ili kutumbuiza siku ya harusi, sio kwa jumba lile japo nliishia uani tyuuh ila nilichanganyikiwa kabisaa.
 
Mbweni kuna balaa aisee unaweza omba unywe sumu ufe maana unaweza jiona wewe si binadamu😀 ,kuna watu wana hela nyieee🙌
 
Sio halali aisee zile hela lazima zitakuwa za upigaji hakuna public servant mwenye mshahara wa kujenga mijengo kama ile Hakuna!
Kuna yule alimtaja ndugu yake mwenye gorofa moja alafu kaweka lifti....hata yy anashangaa kwa mshahara upiii, sema tuache utani wapigaji wenye miradi yao wameula aseee....nilikua pori huko mji unaposogea ni balaaa.....unaambiwa huuu ukuta wote kuanzia hapa mbka mwisho ntakuonesha wa mama flani kitengoni....ukuta wenyew nusu saa au zaidi hauiishii tuu....huko mbeleni tutakosa hata pa kuweka mbavu zetu muwahi jamnii ni hatariiiii....mamia kwa maelfu ya ekari ana miliki mtu mmoja
 
Wazazi waliojenga hiyo mijengo kwenye miji mipya wakianza kustaafu miji inaanza kuoza sababu pesa zinakata. Kama ni eneo zuri kama Masaki na Mikocheni watu wananunua na kujenga majengo ya maofisi. Miaka kadhaa huko Mbweni baada ya wapiga dili kustaafu nako kutaanza kuchakaa na kuoza. Nchi za wenzetu unakuta eneo ni la kishua miaka nenda miaka rudi.
 
Nilisoma sehemu yule mzee warren buffet anaishi nyumba ambayo alinunua zamani mnooo....lakini ni usphuani sahv wamemkuta msee katuliaa tu anawazoom.....mndengereko mimi sasa weee
 
Una mpango wa kurudi moja kwa moja siku za baadae sana? Binafsi japo nafsi inasitasita ila nina mpango wa kuhamia Ujerumani mazima mwakani mwezi wa 6.
 
Mbezi ya kimara nayo kubwa mkuu.. Luis, makabe, msakuzi, hadi tegeta A. Mchawi ni barabara tu,ila zikijengwa utashangaa siku ukipita watu wameshusha madude sio poa
Dar kunatakiwa kuwe na ring road kuanzia Tegeta, Madale, Kimara, Kinyerezi, ipite mpaka Gezaulole huko.

Yani unatoka Tegeta mpaka airport au Gezaulole kwa hii barabara huhitaji Bagamoyo Road, huhitaji Kawawa Road, huhitaji Mandela Road wala Nyerere Road.

Ingeupanua mji vizuri sana na kupunguza traffic hapa kati.
 

Unaiacha vipi Salasala Mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…