Kwanini Mbezi beach imepoteza umaarufu wake iliyokuwa nao miaka ya nyuma?

Kwanini Mbezi beach imepoteza umaarufu wake iliyokuwa nao miaka ya nyuma?

Dar kunatakiwa kuwe na ring road kuanzia Tegeta, Madale, Kimara, Kinyerezi, ipite mpaka Gezaulole huko.

Yani unatoka Tegeta mpaka airport au Gezaulole kwa hii barabara huhitaji Bagamoyo Road, huhitaji Kawawa Road, huhitaji Mandela Road wala Nyerere Road.

Ingeupanua mji vizuri sana na kupunguza traffic hapa kati.
Ndo wameng'ang'ana kubomoa na kujenga mwendokasi....
 
Mbezi kimara ni sababu ya stendi ya Magufuli...pamoja na sekeseke la kubomolewa watu nyumba kipindi cha Magu..
Ni kama vile ilivyokuwa ubungo stendi kipindi hicho....Tanzania nzima walipajua sababu ndo lango la kuingilia Daslam kipindi hicho...
Tatu nafikiri unachanga maeneo yanayotajwa sana na ovyo na maeneo ya watu wanaojiweza kiasi fulani...huko mbezi kimara kuko midomoni mwa watu na kumekua mashuhuri sababu ndo lango la kuingia Daslam kwa watu wa kipato cha kati mpaka mwisho huko ambao ndo wengi mjini hapa...mfano maeneo kama Airport kule kukitajwa ovyo ovyo...sababu only the few ambao hawana kelele ndo wanapita kule....
Angalia maeneo kama Mbweni...huwezi iskia inatajwa ovyo ovyo...lkn kule kuna watu wamejishindilia sio mchezo..
 
Mbezi beach ina portion zake ziko vizuri na watu wenye uwezo. Mfano kule mtaa wa Ally sykes unaotokea Tangibovu kuanzia JK nyerere shule kwenda chini mpaka kule kwa rayvanny na zuchu mpaka efm watu wako vizuri sana.

Kule chini ukivuka Bot flats kwa kina marehemu mzee Kikenya, Bob Makani, kwa Lowasa, mpaka upepo garden kule watu wanajiweza,

Portion ya kidimbwi kwa kina Mzee Nyange, Temu wa swissport na kitilya mpaka anapoishi diamond ni pa kishua haswa,

Portion ingine watu wako na mzigo wa hatari inaitwa Kilongawima, salasala nayo kuna portion ya kuanzia feza schools mpaka kwa Baraka shelukindo, imani kajura kule watu wana mzigo wa kutosha.

Ipo swekeni ya maskiji pia kuna wanaysa na wamakonde kama pale uwanja wa mama maria nyerere panaitwa Rungwe opposite na madofe aliyekuwa mkuu wa chuo cha ifm.

Kuna sehemu inaitwa Bahari beach kwa kina mwakyembe, Mzee wa Akuzamu, kwa majizo, kwa bilionea msack mwenye kibo complex hatari sana nako watu wako na pesa ya hatari. Ununio huko kwa kina marley dollarz, bilionea mwamasika mzee wa kokoto huko watu wako na mzigo wa kutosha,

na kuna boko watu mpaka wamejitengenezea uwanja wa mpira mzuri na majani ya ulaya kwa kina engineer kakwezi, mzee rubinga etc.

Goba pia kuko na ma patron akina Kibatala na mentor wake wakili msomi Fungamtama watu wako vizuri sana

Bunju beach hiyo iko na moga schools na Nbaa apc hotel kwa kina Papa amos makala, makonda, semu, late Mugwasa , kuna shule ya DIS,

Ila mbweni ndio inaongoza kwa madon ikiwa namba moko mwenyewe ana nyumba huko, mbweni jkt na kwingineko. Ila wanaharibu kuruhusu fremu ziwe nyingi kama mbezi kwa zena sasa hivi kunavyoenda kuwa fremu, liquor store, duka za nguo zimekuwa za kutosha. Mipango miji inakuwa duni sana
 
Thread ya watoto wa mjini sio sisi tulioingia dar kikwete anaingia madarakani

Either ways, Ila Dar kuna sehemu unapita hadi unajiuliza hivi hawa waliojenga ni watanzania hawa hawa naopishana nao kuna wale watu wa nje ndio wanashusha haya matusi
 
Nimeshindwa kuelewa kwanini Avic Town kumetelekezwa...
Nilipita kushangaa sio mchezo...
Sijui wabongo hawapendi vitu vikipangiliwa?
Miradi yote hiyo ilikuwa inflated kwanza kipindi ambacho Avic inajengwa, siamini Kigamboni ilikuwa occupied kiasi cha kwenda kujenga mbali hivyo na hata ule mradi mwingine wa dege
 
Miradi yote hiyo ilikuwa inflated kwanza kipindi ambacho Avic inajengwa, siamini Kigamboni ilikuwa occupied kiasi cha kwenda kujenga mbali hivyo na hata ule mradi mwingine wa dege
Majengo yamepelekwa mbali na mji kuna muda nafikiri kwann hata wasinge nunua baadhi ya mitaa magomeni mwanzoni huku wakaweka mradi wao mbona ingekuwa poa tu
 
Landlover zilikuwa mbili Moja inapaki bwawani pale mwembe madole nyingine inabaki mbez beach huku ....hiz gari Moja ilikuwa rangi ya blue nyingine silver gar ya tesha na bongo man
Asante,watoto wadogo hawawezi kuelewa maana unaweza kuelezea kitu humu watu wakafikiri unapiga fix

Alafu huko root ya kwenda mbezi kimara ilikuwa hakuna

Ova
 
Landlover zilikuwa mbili Moja inapaki bwawani pale mwembe madole nyingine inabaki mbez beach huku ....hiz gari Moja ilikuwa rangi ya blue nyingine silver gar ya tesha na bongo man
Miaka hiyo huko mashuwa wengi walikuwa na mashamba
Miaka hiyo bado madogo nakumbuka
Tulipakiwaga na yule p.bomani kwenye ule mrange wake akatupeleka
Shambani kwake lilikuwa bonge la eneo mifugo,mabwawa ya samaki nk

Ova
 
Majengo yamepelekwa mbali na mji kuna muda nafikiri kwann hata wasinge nunua baadhi ya mitaa magomeni mwanzoni huku wakaweka mradi wao mbona ingekuwa poa tu
Nadhani hizo zilikuwa ni plan za ule mji mkubwa wa kigamboni ndio maana apartments nyingi ziliibuka kigamboni.

Lakini hata hivyo, bado apartments nyingi kama Avic, watumishi na Dege zilijengewa mbali na ferry. Hiyo nadhani ndio sababu watu hawakai huko
 
Miaka hiyo huko mashuwa wengi walikuwa na mashamba
Miaka hiyo bado madogo nakumbuka
Tulipakiwaga na yule p.bomani kwenye ule mrange wake akatupeleka
Shambani kwake lilikuwa bonge la eneo mifugo,mabwawa ya samaki nk

Ova
We jamaa ningekuwa na pesa, ningenunua story yako kwa ajili ya production ya kitabu na movie series maana lazma itauza tu 😁👏🏾👏🏾
 
Nadhani hizo zilikuwa ni plan za ule mji mkubwa wa kigamboni ndio maana apartments nyingi ziliibuka kigamboni.

Lakini hata hivyo, bado apartments nyingi kama Avic, watumishi na Dege zilijengewa mbali na ferry. Hiyo nadhani ndio sababu watu hawaai huko
Hata hivyo hizi nyumba kwa kiasi kikubwa ukiangalia muundo zilivyo jengwa kama hosteli za wanafunzi 😄 inahitaji moyo sana aisee
Kuna yale magofu kama unaenda kigamboni kutokea kijichi aisee
 
Hata hivyo hizi nyumba kwa kiasi kikubwa ukiangalia muundo zilivyo jengwa kama hosteli za wanafunzi 😄 inahitaji moyo sana aisee
Kuna yale magofu kama unaenda kigamboni kutokea kijichi aisee
Yale ya watumishi 😁😁😁 , anko magu alivyoingia aliyapiga stop kuendelea.

Halafu kama ulivyosema , wabongo wengi mfumo wa apartments hizo huwa wanaona kama hostel au kota 😁
 
Back
Top Bottom