Kwanini Mbilikimo wengi wanapatikana kwenye Misitu ya DRC

Kwanini Mbilikimo wengi wanapatikana kwenye Misitu ya DRC

Bado Nategemea Muendelezo Wa Thread Hii Kwa Kupata Hoja Zenye Kutuelimisha Wote Kila Iitwapo Leo
 
Have the evolutionists now found the missing link between ape and man?
 
Swaali zuri sana;

Kwanza fahamu kuwa kuna mbilikimo wa aina mbili: mbilikimo wa asili (pygmy) na mbilikimo wa ugonjwa (dwarf). Wale wa kongo ni mbilikiko wa asili kwa maana ya kuwa maumbile yao ni asili yao na yanatokana na mazingira yao ya asili. Umbilikimo wa aina hii ni hereditary kwa maana ya kuwa huzaliwa na mbilikimo pia. Ni kama ambavyo maumbile ya asili ya waachina yalivyo tofauti na maumbile ya asili ya wazungu, na pia wachina huzaliwa na wachina tu.

Kuna mbilikimo wa aina nyingine ambao wanapata matatizo ya mwili kushindwa kutengeneza hormones zinazohitajika mwili kukua, na hivyo kubaki na umbo la kitoto maisha yao yote; hawa wanajulikana kama drwafs. Mbilikimo wa aina hii huweza kutokea katika familia yoyote ile, wazazi wawili warefu wanaweza kuzaa mbilikimo wa aina ya dwarf.

Theories zinazonyesha kuwa evolutionary process iliyosababisha waafrika wakawa na ngozi nyeusi kutokana na mazingira ya joto la tropical, ndiyo pia iliyosababisha watu waliokuwa wakiishi kwenye misitu mizito kama vile Kongo kuwa wafupi kwa vile miili yao ilikuwa inakosa mwanga wa jua kutengeneza vitamin D; kwa hiyo miili yao ikawa haiwezi ku-absrob calcium ya kutosha, jambo liliosababisha wawe na mifupa midogo na hivyo kuwa na miili midogo. Misitu ya Kongo ndiyo yenye mbilikimo wengi wa aina hiyo ikifuatiwa na misitu ya Amazon huko Brazili. Kuna sehemu nyingine za dunia kama Papua New Guinea na Australia ambako pia kuna mbilikimo waliotokana na misitu mikubwa iliyokuweko maeneo hayo.
Kwa nini mbilikimo wa Kongo wasiwe weupe maana hawapigwi na jua?
 
Ni kweli hawa Pygmy wa Congo huuwawa na kuliwa ni baadhi ya jamii za huko?
 
Kwann mbilikimo wa Kongo wasiwe weupe maana hawapigwi na juwa?
Utashangaa kuwa mionzi ya ultra-violet zinazoleta vitamin D ni low frequency wakati zile zinazosababisha tan kwenye ngozi ni high frequency, halaf tana hutegemea na intensity ambayo pamoja na mambo mengine hutegemea na incident angle ya mionzi. Mionzi inayopiga moja kwa moja (digrii tisini ) huchoma ngozi sana kuliko mionzi inayopiga kutokea pembeni. vile vile high frequencies hupenya sana kuliko low frequencies, ndiyo maan X-ray hupenya ndani ya mwili kwa sababu hii ni frequency ja juu sana kuliko visible light. Hebu google "electromagnetic spectrum."
 
Swaali zuri sana;

Kwanza fahamu kuwa kuna mbilikimo wa aina mbili: mbilikimo wa asili (pygmy) na mbilikimo wa ugonjwa (dwarf). Wale wa kongo ni mbilikiko wa asili kwa maana ya kuwa maumbile yao ni asili yao na yanatokana na mazingira yao ya asili. Umbilikimo wa aina hii ni hereditary kwa maana ya kuwa huzaliwa na mbilikimo pia. Ni kama ambavyo maumbile ya asili ya waachina yalivyo tofauti na maumbile ya asili ya wazungu, na pia wachina huzaliwa na wachina tu.

Kuna mbilikimo wa aina nyingine ambao wanapata matatizo ya mwili kushindwa kutengeneza hormones zinazohitajika mwili kukua, na hivyo kubaki na umbo la kitoto maisha yao yote; hawa wanajulikana kama drwafs. Mbilikimo wa aina hii huweza kutokea katika familia yoyote ile, wazazi wawili warefu wanaweza kuzaa mbilikimo wa aina ya dwarf.

Theories zinazonyesha kuwa evolutionary process iliyosababisha waafrika wakawa na ngozi nyeusi kutokana na mazingira ya joto la tropical, ndiyo pia iliyosababisha watu waliokuwa wakiishi kwenye misitu mizito kama vile Kongo kuwa wafupi kwa vile miili yao ilikuwa inakosa mwanga wa jua kutengeneza vitamin D; kwa hiyo miili yao ikawa haiwezi ku-absrob calcium ya kutosha, jambo liliosababisha wawe na mifupa midogo na hivyo kuwa na miili midogo. Misitu ya Kongo ndiyo yenye mbilikimo wengi wa aina hiyo ikifuatiwa na misitu ya Amazon huko Brazili. Kuna sehemu nyingine za dunia kama Papua New Guinea na Australia ambako pia kuna mbilikimo waliotokana na misitu mikubwa iliyokuweko maeneo hayo.
Biology naisomaga ila siiaminigi sana
 
Organism Adaptation and survival na Organism mutation changes hapo ndipo kwenye majibu yenu somo pana mno
kwenye Organism adaptation and survival hapo viumbe vinakua vya asili ya maeneo au mazingira husika ili waweze kuishi,kufanya shughuli nyingine na kuzaana, hao ni Pygmy, Aidha kwenye Organism Mutation changes hapo viumbe sio lazima viwe na asili ya eneo husika bali ni mabadiliko yao ya kimwili yanatokana na mabadiliko ya genes hata seli hai kubadilika kutokana na sababu za mfumo wa maisha wa vinasaba kukosa muelekeo wa kimuundo na uzalishaji, mabadiliko ya kubadilika kwa hali ya mwili yanatokana na mazingira mapya, vyakula, madawa,vipodozi na misongo, Kumbuka mazingira ndio hubadili maisha na muundo wa mwili, kwa mazingira mapya na mabadiliko ya kimaumbile yanayotokana na vinasaba zalishi ndio hubadili muonekano wa mwili wa kiumbe bila kujali mazingira yake.

Hivyo basi wale wenye asili ya kuishi katika misitu mikubwa miili yao inatakiwa iendane na mazingira ya pale, kumbuka ukuaji wa mwili wa binaadamu unaletwa na ongezeko na ukuaji wa mifupa, aidha mifupa inakuzwa na madini ya calcium ,madini hayo hupata kasi ya kukua kutoka kwenye vyakula na mwanga wa jua, mwanga wa jua hutoa vitamini D inaingia mwilini na kuboresha uimarikaji wa mifupa, mfano mimea yote midogo inayozunguukwa na msitu minene huwa na maumbile madogo kwasababu miti refu ndio inayopata mwanga wa kutosha kuliko hiyo mimea, geuza mimea ndio hao mbilikimo na mazingira ndio msitu mnene.

Vilevile aina ya organism mutation changes hapa sio lazima mzazi wa mbilikimo awe mbilikimo maana mabadiliko hayo hayaendani na mzaingira bali yameletwa na mabadiliko ya mfumo wa mwili. ni hayo machache wakuu jazieni minofu nilipokosea
 
Kwann mbilikimo wa Kongo wasiwe weupe maana hawapigwi na juwa?
Kinacho fanya weusi wa ngozi utokee siyo mwanga mweupe wa jua (visible light) bali ni UV rays (utra violet) zinazokuja pamoja na mwanga wa jua. Japo kuwa kuna misitu na vivuli vingi upande ule wa kongo lakini bado eneo husika lipo upande wa ikweta ambao una kiasi kikubwa cha mionzi hiyo (UV) kuliko kwenye poles.
 
biblia inatuambia kulikuwa na Goliath hilo ni jitu refu tena limeshiba na pia kulikuwa na zakayo kalikuwa kafupi huko middle east
Haya bana mimi nilikuwa naongelea ya kaisari.
 
ule msitu ni mkubwa, hawapati jua la kutosha ndiyo maana hawakui warerefu
 
Sielewi iwapo unakataa maelezo niliyotoa hapo juu au unapinga theory ya evolution. Maelezo niliyotoa hapo juu yana ushahidi wa kutosha kuwa watu wa sehemu zote zenye asili ya mistu mikubwa (rainforests) kama vile Congo, Amazon, Quuensland, na papua new Guinea ni mbilikimo. Sababu yake halisi ni hiyo, mifupa hujengwa kwa calcium ambayo mwili wako utaiabsorb tu iwapo una Vitamin D ya kutosha. Na vitamin D hutokana na mwanga wa kutosha. Process hii inajijenga pole pole kwa muda mrefu san (evolution).

Kuhusu Theory ya evolution sijui nikueleze vipi iwapo huiamini. Kumbuka kuwa theory hiyo inatumia muda wa mamilioni ya miaka siyo miaka elfu moja tu. Kama umepiga shule ya kutosha kuhusu mabadiliko ya muudo wa dunia, utajua kuwa Africa, South America, Australasia na India zilikuwa ni bara moja kwenye maeneo ya tropical. Kwa hiyo watu weusi unaowaona huko wote wana asili ya tropical. Soma theory ya Pangaea kwa makini halafu ufuatilie theories za Plate Tectonics, baadaye uchunguze tena namna matetemeko ya dunia yanavyotokea leo ndipo uangalie tena ukaribu wa sehemu zote unazoona leo zina asili ya watu weusi. Uhamiaji uliotokea baada ya ugunduzi wa vyombo vya kusafuiria ndio uliosababisha watu hawa kuchanganyikana; hakukuwa na mtu mweupe kusini ya ikweta. Uhamiaji huo umetokea miaka isyozidi 2000 zilizopita, kipindi ambacho si kifupi sana katika process ya evolution.
Shukran kaka,

Umenikumbusha mbali sana ulipogusia hzo theories, nilizikariri sana wakati tuko chuo..

Unachozungumza umefafanua vzur ila tokana na mitazamo tofauti, usishangae wakapinga kutumia misimamo ya dini na n.k.
ila uko sawa kabisa ukisimamia theories hizo.

thanks
 
Back
Top Bottom