Kwanini Mbilikimo wengi wanapatikana kwenye Misitu ya DRC

Bado Nategemea Muendelezo Wa Thread Hii Kwa Kupata Hoja Zenye Kutuelimisha Wote Kila Iitwapo Leo
 
Have the evolutionists now found the missing link between ape and man?
 
Kwa nini mbilikimo wa Kongo wasiwe weupe maana hawapigwi na jua?
 
Ni kweli hawa Pygmy wa Congo huuwawa na kuliwa ni baadhi ya jamii za huko?
 
Kwann mbilikimo wa Kongo wasiwe weupe maana hawapigwi na juwa?
Utashangaa kuwa mionzi ya ultra-violet zinazoleta vitamin D ni low frequency wakati zile zinazosababisha tan kwenye ngozi ni high frequency, halaf tana hutegemea na intensity ambayo pamoja na mambo mengine hutegemea na incident angle ya mionzi. Mionzi inayopiga moja kwa moja (digrii tisini ) huchoma ngozi sana kuliko mionzi inayopiga kutokea pembeni. vile vile high frequencies hupenya sana kuliko low frequencies, ndiyo maan X-ray hupenya ndani ya mwili kwa sababu hii ni frequency ja juu sana kuliko visible light. Hebu google "electromagnetic spectrum."
 
Biology naisomaga ila siiaminigi sana
 
Organism Adaptation and survival na Organism mutation changes hapo ndipo kwenye majibu yenu somo pana mno
kwenye Organism adaptation and survival hapo viumbe vinakua vya asili ya maeneo au mazingira husika ili waweze kuishi,kufanya shughuli nyingine na kuzaana, hao ni Pygmy, Aidha kwenye Organism Mutation changes hapo viumbe sio lazima viwe na asili ya eneo husika bali ni mabadiliko yao ya kimwili yanatokana na mabadiliko ya genes hata seli hai kubadilika kutokana na sababu za mfumo wa maisha wa vinasaba kukosa muelekeo wa kimuundo na uzalishaji, mabadiliko ya kubadilika kwa hali ya mwili yanatokana na mazingira mapya, vyakula, madawa,vipodozi na misongo, Kumbuka mazingira ndio hubadili maisha na muundo wa mwili, kwa mazingira mapya na mabadiliko ya kimaumbile yanayotokana na vinasaba zalishi ndio hubadili muonekano wa mwili wa kiumbe bila kujali mazingira yake.

Hivyo basi wale wenye asili ya kuishi katika misitu mikubwa miili yao inatakiwa iendane na mazingira ya pale, kumbuka ukuaji wa mwili wa binaadamu unaletwa na ongezeko na ukuaji wa mifupa, aidha mifupa inakuzwa na madini ya calcium ,madini hayo hupata kasi ya kukua kutoka kwenye vyakula na mwanga wa jua, mwanga wa jua hutoa vitamini D inaingia mwilini na kuboresha uimarikaji wa mifupa, mfano mimea yote midogo inayozunguukwa na msitu minene huwa na maumbile madogo kwasababu miti refu ndio inayopata mwanga wa kutosha kuliko hiyo mimea, geuza mimea ndio hao mbilikimo na mazingira ndio msitu mnene.

Vilevile aina ya organism mutation changes hapa sio lazima mzazi wa mbilikimo awe mbilikimo maana mabadiliko hayo hayaendani na mzaingira bali yameletwa na mabadiliko ya mfumo wa mwili. ni hayo machache wakuu jazieni minofu nilipokosea
 
Kwann mbilikimo wa Kongo wasiwe weupe maana hawapigwi na juwa?
Kinacho fanya weusi wa ngozi utokee siyo mwanga mweupe wa jua (visible light) bali ni UV rays (utra violet) zinazokuja pamoja na mwanga wa jua. Japo kuwa kuna misitu na vivuli vingi upande ule wa kongo lakini bado eneo husika lipo upande wa ikweta ambao una kiasi kikubwa cha mionzi hiyo (UV) kuliko kwenye poles.
 
biblia inatuambia kulikuwa na Goliath hilo ni jitu refu tena limeshiba na pia kulikuwa na zakayo kalikuwa kafupi huko middle east
Haya bana mimi nilikuwa naongelea ya kaisari.
 
ule msitu ni mkubwa, hawapati jua la kutosha ndiyo maana hawakui warerefu
 
Shukran kaka,

Umenikumbusha mbali sana ulipogusia hzo theories, nilizikariri sana wakati tuko chuo..

Unachozungumza umefafanua vzur ila tokana na mitazamo tofauti, usishangae wakapinga kutumia misimamo ya dini na n.k.
ila uko sawa kabisa ukisimamia theories hizo.

thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…