Kwanini mbwa hugongwa sana na magari barabarani?

Kwanini mbwa hugongwa sana na magari barabarani?

Juzi nimesafiri kutoka mkoa wa Dar es Salaam kwenda mkoa wa Shinyanga. Kijiografia, ni umbali mrefu, ambapo magari ya abiria hutumia si chini ya masaa 16 kufika mwisho wa safari.

Sasa kuna jambo moja nimeliona katika safari hii ndilo nataka wajuvi wa mambo ya wanyama watueleze, kwani ni jambo la kufikirisha kidogo!

Mnyama mbwa, ni miongoni mwa wanyama wanaotumiwa na binadamu katika shughuli mbalimbali za kijamii, kama ulinzi, kunusa, nk. Lakini pia, mnyama huyu anaweza kufundishwa michezo mbalimbali na akamudu kuicheza sawia.

Kwa muktadha huo, inaonyesha kuwa, mbwa ana akili pengine kuliko wanyama wengine, na ndiyo maana ni rahisi kwake kufundishika, tofauti na wanyama wengineo (most).

Sasa juzi katika safari yangu hiyo, nimeshuhudia si chini ya mbwa 6, mahala tofauti tofauti, wamegongwa na magari. Hapo ndio najiuliza, inakuwaje mnyama mwenye akili kuliko wengine; kama mbuzi, punda, paka, kuku, nguruwe, kondoo, ng'ombe, nk, anagongwa na magari wakati hawa wenye akili kidogo hawagongwi?!

Wakati tunajibu swali hili, majibu yetu tuhusianishe na ubongo wa mbwa, na sio factor nyingine kama uwingi wao, kukosa matunzo, kichaa cha mbwa, nk; kwani hizi ni hoja nyepesi. Mbwa wanaoongelewa hapa ni wakamilifu kwa mitazamo yote.

Mtu anaweza kuona nimeuliza jambo la kijinga, lakini wataalamu wa wanyama najuwa watakuja na sababu za msingi kuhusiana na jambo hili! Au wenzangu hamjawahi kijiuliza kwanini mbwa anagongwa kirahisi sana na magari kuliko wanyama wengine?
mi nachoonaga mbwa wanakuwaga na ujasiri fulani, yaani siyo waoga km mbuzi. Kutokujali.
 
Wanyama wengi huwa na mtu wa kuwalinda sio mbwa na paka
Wakivuka hawaangalii magari ko lazma walimwe tu,
 
Hasa nyakati za usiku hua wanashindwa kutathimini umbali wa gari na hapo alipo sababu ya taa
 
Mbwa wengi wanagongwa wakati wa usiku na sio mchana na wakati wa usiku mbwa ndio anaona vizuri sana,wakati wa giza macho ya mbwa rods (scotopic vision)zake huwa active sana kuliko cones(photopic vision),hivyo humchukua muda mrefu kubadilishana mawasiliano ,hivyo ikitokea mbwa anavuka katika giza na gari ikatokea maana yake macho yake yatashindwa kuona hivyo mara nyingi wanalazimika kusimama ama kuendelea na safari kitu ambacho ni hatari kwao
Naona kama inamake sense
 
Vyovyote iwavyo, wakigongwa au wamegongwa, swali ni je walipofikwa na kitendo cha kugongwa wote hao walikuwa wamekufa au walikuwa wazima ??
Nadhani wengine watakua walikimbia.
 
Dogs can be vulnerable to getting hit by moving vehicles for several reasons:

Size and visibility: Dogs are generally smaller than vehicles and can be difficult for drivers to spot, especially if they are crossing the road in low-light conditions or in areas with poor visibility. Their size makes them more prone to being overlooked by drivers, particularly if they are moving quickly or unexpectedly.

Speed and unpredictability: Dogs can move swiftly and erratically, making it challenging for drivers to anticipate their movements. They may dart across the road suddenly or run in unpredictable patterns, increasing the likelihood of a collision.

Lack of road sense: Unlike humans, dogs do not have an innate understanding of road safety. They may not comprehend the dangers posed by moving vehicles or the concept of traffic rules. Consequently, dogs might attempt to cross roads without properly assessing the oncoming traffic.

Leash or containment failure: Sometimes, dogs may escape from their leashes or enclosures, leading to unexpected encounters with vehicles. If a dog is not properly restrained or supervised, they may wander onto roads and increase the risk of being struck by a vehicle.

Distractions: Dogs can be easily distracted by various stimuli, such as other animals, unfamiliar sounds, or enticing scents. These distractions can divert their attention away from potential dangers on the road, making them more susceptible to accidents.

It is crucial for dog owners to take appropriate measures to keep their pets safe, such as keeping them on a leash or within a fenced area, providing proper training and supervision, and avoiding allowing them to roam freely near busy roads. Additionally, drivers should remain vigilant and cautious, especially in areas where dogs are likely to be present, such as residential neighborhoods or parks.
Tutafsirie KWA kiswwhili mkuu
 
Hilo la binadamu kugongwa nililijibu (unaweza kurejea). Halafu unasema sio kweli kuwa mbwa ana akili kuliko wanyama wengine, ni wanyama wepi hao wenye akili kuliko mbwa? Na je, wanafundishika?
 
KKwahiyo mkuu kigezo chako cha wewe mbwa kuwa na akili kuliko wanyama wengine ni KWA sababu anafunidishika
Hilo la binadamu kugongwa nililijibu (unaweza kurejea). Halafu unasema sio kweli kuwa mbwa ana akili kuliko wanyama wengine, ni wanyama wepi hao wenye akili kuliko mbwa? Na je, wanafundishika?
 
Ehhh, eti mbwa kugongwa na magari [emoji849][emoji849] hell my foot
 
Back
Top Bottom