Kwanini mfalme Zumaridi anasumbuliwa sana na dola? Uhuru wa kidini uko wapi!?

Kwanini mfalme Zumaridi anasumbuliwa sana na dola? Uhuru wa kidini uko wapi!?

Kama si chawachawa wa ccm na ana mrengo wa kipinzani lazima waruke naye tu. Kama mnabisha ajitokeze mchungaji wa kanisa fulani aunge mkono upinzani hadharani mtaona watakavyomshughulikia fasta bila kujali ni mwanamke
Sio kuunga mkono
Yaani wachungaji wanaosema ukweli wanatekwa, Kuna yule alitekwa jana , kapatikana Leo msitu Gani sijui kamsikikize na Hana chama
 
Nimesoma taarifa ya polisi kuhusu kukamatwa kwa mfalme Zumaridi imenishangaza sana.

Lini polisi badala ya NEMC wameanza kushughulikia uchafuzi wa mazingira kwa kelele?

Lini katika nchi hii imekuwa kosa kisheria mtu kujisema yeye ni mungu?

Kwa muda mrefu sana polisi wamekuwa wakijishughulisha na Zumaridi inashangaza madai ya kwamba hajasajili kanisa lake, kama ni kweli kwa nini wasimasaidie kusajili kanisa lake ? Au anakwamishwa kwa makusudi??

Dola mwacheni mfalme Zumaridi afanye mambo yake kwa amani na uhuru bila usumbufu, mpeni uhuru wote wa kidini mnaowapa waumini wa dini nyingine zote.

tatizo la huyu mungu ana sura mbili moja ya makeup na nyingine ni ya mahakamani ila huyu mungu nikimkuta na makeup naruka ae ndombolo vizuri tu🤣🤣🤣🤣
 
Yaani anavyopinga hivi mwanao ndiyo anarudi kanisani anawambia mungu zuma alitununulia na ice-cream unajisikia vipi! Huyo mbishi kweli
Wazuie watoto wako kwenda huko, sio kumkamata Zumaridi kwa sababu hampendi mafundisho yako, Zumaridi hujafanya kosa lolote kujiita mungu.
 
Wazuie watoto wako kwenda huko, sio kumkamata Zumaridi kwa sababu hampendi mafundisho yako, Zumaridi hujafanya kosa lolote kujiita mungu.
Wakafanye nini huko wewe mtoto wa mungu zuma?
 
Back
Top Bottom