Kwanini mgeni akiulizwa "unaondoka lini" inakuwa nongwa?

haya ndio maneno sasa
 
Kuna dada angu nilimuuliza anakuja kufanya nini, ukawa ugomvi mkubwa sana.
Miafrika ndivyo tulivyo.
Ifike mahali tuambizane ukweli.
Akija aseme alichofuata na atakuwepo kwa muda gani.
Lazima tuende kwa utaratibu.
Kwa mfano huko alikotoka ametenda uhalifu. Kitendo kumhifadhi mhalifu ni kosa la jinai na unaweza ukabananishwa nalo.
 
Ifike mahali tuambizane ukweli.
Akija aseme alichofuata na atakuwepo kwa muda gani.
Lazima tuende kwa utaratibu.
Kwa mfano huko alikotoka ametenda uhalifu. Kitendo kumhifadhi mhalifu ni kosa la jinai na unaweza ukabananishwa nalo.
umenikumbusha jambo mkuu. Kuna dogo mmoja wa kijijini tulikuwa naye alikuwa safarini kwenda machimboni akanipigia simu afikie home kesho aendelee na safari. Bila hata kufuatilia historia yake nikachukulia poa,nikapiga simu home wakampokea. Kumbe ni kibaka mno hata kwa muonekano tu. Ili asionekane mbaya wife akaficha huo ukweli. Bahati nzuri alilala mabanda ya nje,akaiba baiskeli na vyombo vya ndani akasepa usiku kwa usiku. Nakuja kutoa taarifa kijijini wakaniambia alishakuwa kibaka
 
Ila mkienda kijijini kwa huyo mliyemuuliza nini ndo mnakomba mazao yake yote kila kitu mnasema nifungie tu, mahindi, maharage rangi zote, karanga, njugu, mikungu ya ndizi, mihogo, parachichi mpaka passo inachuchumaa kama mbuzi anakojoa. Wakati wewe unakasirika mgeni amekaa sana yeye anafurahi kwamba amekufungia mazagazaga kwake ni baraka.
Tukubali tu kwamba maisha ya mjini ni ya kimaskini, ya bush ni raha bila presha
 
Hi Ndio sababu kwanini sipendi kula au kutembelea watu.ile hari yakuhisi mtu ananifikiliaje sipend Hata kidogo
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Huu uzi ni wa kibongo hasa yaani !
 
kwa nini umefikiria wa mjini tu,kwani wa kijijini hawezi kuuliza unaondoka lini ili atafututie mbuzi mnono
 
Bado hatujafikia huko kuwa wachoyo na wabinafsi bongo hii chakula Hadi Cha buku unapata Tena ni huko huko dar vyakula kibao
 
Wageni wa kulala siwapi nafasi nyumbani kwangu kama una shida nitakusaidia huko huko ulipo. Kama ni lazima uje lodge itakuhusu japo kwa gharama zangu.
 
Waafrika tunapenda sana kitonga. Kuna kijana mmoja fundi kujenga hapo Dar-Chamanzi kaoa Mnyamwezi, wamepanga vyumba viwili hali ngumu ila mama mkwe na kaka wawili wa dada/mke wapo hapo mwaka wa pili unaisha. Sijui wanalalaje.

Kijana alijaribu kumuuliza mke wake mama na kaka zake wanaondoka lini palikuwa hapatoshi. Walimchangia wote wanne kuwa ni mbinafsi na mchoyo.
 

Wazungu huwa kawaida tu kuulizana hivyo ahha
 
Mgeni anayekuja kwangu kutembea na kuondoka Sina shida naye,shida Ni kwa yule anayetoka kijijini Kuja kukaa kwangu tu,hajulikani kaja kufanya nini na ,atakaa kwa muda gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…