Kwanini mgeni akiulizwa "unaondoka lini" inakuwa nongwa?

Kwanini mgeni akiulizwa "unaondoka lini" inakuwa nongwa?

hiyo let say ni sababu tosha,na inajulikana mazingira yaliyomuweka ndugu na unajipanga namna ya kumsadia. Na unajua shida ikiisha ataondoka
Mbona ukienda kijijini uwe na shida usiwe na hawakuuliza wala kukuwazia utakaa siku ngapi??
 
Mambo mengine S ya kuyaiga tubak na u Africa wetu na u Tanzania wetu
 
Kama akihitaji kuwa kwako utafanyaje??
Mgeni anayekuja kwangu kunisalimia siku moja,mbili hata wiki namkaribisha.Lakini anayekuja hajui kaja kufanya nini,how long will he/she stay,which means he/she is there to stay,huyo ipo siku nitamuuliza utaondoka lini?.
 
Lazima umuulize.

Mwingine nauli tu ya kuondokea anakutegemea wewe mwenyeji

Lazima ujipange kula kunywa matibabu nauli nk nk
 
Ila kusema ukweli kila mtu akae kwao tu [emoji23][emoji23][emoji23],
Kuna dada mmoja alikuwa anapata wageni kila mtu anakuja kujifungulia kwake akitoka huyu anaingia mwingine
Alikuwa akiniamsha usiku kwenda hospital ilifikia hatua nikachoka kusindikiza wenye mimba hospital
 
Swali linajieleza kabisa. Hili lipo sana kwenye familia za Kiafrika.

Nimepokea mgeni, kutokana na mipangilio ya kifamilia na kibajeti nalazimika kumuuliza atakaa hapa ugenini kwa muda gani.

Mara mgeni anaanza kusambaza taarifa mimi ni mbinafsi, sitaki kutembelewa 😂😂😂😂😂
Mkuu wavumilie tu hao wa mikoani, yeye raha yake ashinde tu sebuleni akiangalia TV......baadaye atoke akazurure kariakoo ashangae magorofa..
 
Lazima umuulize.

Mwingine nauli tu ya kuondokea anakutegemea wewe mwenyeji

Lazima ujipange kula kunywa matibabu nauli nk nk
Kuna aliyenipigia simu wiki iliyopita eti nimtumie nauli anataka Kuja kunisalimia,nilimwambia sipo nimesafiri.
 
Kuna aliyenipigia simu wiki iliyopita eti nimtumie nauli anataka Kuja kunisalimia,nilimwambia sipo nimesafiri.
Asalimie yeye

Nauli utoe wewe!!!!!!

Wawe na huruma jamani Mjini pagumu!!!

Yaani hana hata shughuli ya kufanya huyo kajisikia tu kuja mjini!!!
 
Lazima umuulize.

Mwingine nauli tu ya kuondokea anakutegemea wewe mwenyeji

Lazima ujipange kula kunywa matibabu nauli nk nk
Kama huyo mgeni wako uchumi wake ni mkubwa kuliko wako je utamuuliza??
 
Huu uzalendo wa kuvumilia wageni ni mgumu sana hasa life la mjini.

Vijijini ni kawaida, gharama za maisha huko ni simple, watu wanajilia ugali wa mazao waliyolima sio kama huku mjini tunaotegemea kilo kadhaa za unga kwa mangi, bado makorokocho ya mboga yanahitaji vijisenti.

Tujitahidi kuzidisha ukarimu ili tuweze kuhimili mambo kama haya kwenye jamii zetu
Dah nina mdogo wangu anakaa na rafiki wa kaka yake ambaye walikuwa wanafanya kazi sehemu moja. Jamaa aliomba aje afuatilie issue yake sasa ana miezi mi 4 hajaondoka. Kijana anapambana jamaa anakula tu halafu anashindwa kumuondoa. Yaan ni hatari sana
 
Kama ugali upo wa kutosha asimfukeze, amwache akichoka kukaa ataondoka
 
Swali linajieleza kabisa. Hili lipo sana kwenye familia za Kiafrika.

Nimepokea mgeni, kutokana na mipangilio ya kifamilia na kibajeti nalazimika kumuuliza atakaa hapa ugenini kwa muda gani.

Mara mgeni anaanza kusambaza taarifa mimi ni mbinafsi, sitaki kutembelewa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yamenikuta hayo alikuja jamaa kwangu bila taarifa bas mm nikampokea tu kishkaji alikaha Kama mwez coni dalili za yey kusepa na mgeni mwenyew ana kiburi ..nilikomaa mpk sas HV cna hamu na mgen especially hapa dsm mnk anakuwa tegemezi kwa Kila kitu..
 
Ila kusema ukweli kila mtu akae kwao tu [emoji23][emoji23][emoji23],
Kuna dada mmoja alikuwa anapata wageni kila mtu anakuja kujifungulia kwake akitoka huyu anaingia mwingine
Alikuwa akiniamsha usiku kwenda hospital ilifikia hatua nikachoka kusindikiza wenye mimba hospital
...... huwa wanaambizana. Kwa fulani bwana, Hana shida. Utapokeaga Wageni hata usio na ukaribu nao, watafululizana hapo, bandika bandua.
 
Swali linajieleza kabisa. Hili lipo sana kwenye familia za Kiafrika.

Nimepokea mgeni, kutokana na mipangilio ya kifamilia na kibajeti nalazimika kumuuliza atakaa hapa ugenini kwa muda gani.

Mara mgeni anaanza kusambaza taarifa mimi ni mbinafsi, sitaki kutembelewa 😂😂😂😂😂
Matatuzi mengine tunajipa sie wenyewe waafrika, siku hizi karibia ya kila mtu ana simu.....mgeni anakujaje kwangu bila taarifa? Mimi sikaribishi kabisa mgeni, njoo kunitembele asubuhi, mchana ama jioni ondoka. Sipendi mazoea ya kijinga namna hii.
 
Back
Top Bottom