Kwanini Mishahara ya Watumishi wa Taasisi za Umma inapishana?

Kwanini Mishahara ya Watumishi wa Taasisi za Umma inapishana?

Mkuu, lazima tupime kwa unachokizalisha. Pengine panahitahi motisha ili kuleta uwajibikaji wa kiwango cha juu..

Mfano, afisa wa TRA anapaswa kulipwa kiwango kikubwa kulingana na unyeti wake na kumtoa katika hati hati za kula rushwa. Sawa, bado wanakula lakini hali ingekuwa mbaya zaidi kama mambo yangekuwa sivyo.

Unyeti wa kazi husika pamoja ni muhimu.

Unataka Mwalimu alipwe sawa na sisi Madaktari kwa kuzingatia kiwango sawa cha elimu? Kufanya hivyo utaharibu kabisa umuhimu wa sekta mbalimbali.

Hiyo kamwe haitowezekana. Si Tanzania tu, dunia nzima.
Daktari gani ana mshahara mzuri wewe?

Usome miaka yote hiyo halafu mshahara 1.5 m si ujinga huo.

Mlinzi wa getini f4 wa TPA TPDC anamzidi dr aliesoma miaka 7
 
Huko halmashauri mambo hayaendi, miradi imekwama na upigaji juu kwa sababu watu hawana pesa.

Kuna jamaa yupo halmashauri muhasibu analipwa TGS D halafu mwenzake NSSF analipwa 1.5M+ sasa huo MOYO wa kufanya kazi atautoa wapi.

KAMA NCHI TUMEKWAMA KWA KWELI.
Na posho pia kamzidi huyo wa TGS D.
Sasa hapo kilichobaki ni kuandaa madokezo ya kununua machupa ya chai na sabuni za chooni ili abane tusenti
 
Kama ipi ww ambae ni daktar mbona unapitwa mshaara na watu liofel form four wapo kwenye kakitengo kadogo tu kwa ubaharia bandarin na ni certificate tu tena inasomewa wiki nne hiyo certificate wanaanza kaz na mshaara wa 1.6 kwahyo hao ni muhimu kuliko daktar kama kwel ww ni daktar najua unajua ugumu wake kuanzia kaz mpka kuupata huo udakitar sasa inakuaje unaanza na 1.4 unazidiwa na baharia wa bandarin ?au fundi umeme tu wa bandarin umgusi kwa mshaara kwahyo ww auna umuhimu kuliko hao niliokutajia?
Kwani daktari ana umuhimu kuliko hao uliowataja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daktari gani ana mshahara mzuri wewe?

Usome miaka yote hiyo halafu mshahara 1.5 m si ujinga huo.

Mlinzi wa getini f4 wa TPA TPDC anamzidi dr aliesoma miaka 7
Umeona eeee hili sio sawa hii mishahara imekuwa kimichongo michongo na sababu za upishano huu hata azielewek serikal ilipitie tena lasivyo watu wataiba sana
 
Mtakusanya nini kama amna afya ya kueleweka kila mkiumwa mnakufa tu wake zenu wakibeba mimba awajifungui wanakufa wao na watoto wao kuna nini hapo acheni ujanja ujanja bhna
Kwani bila madaktari hakuna afya inayoeleweka, tukiumwa tunakufa tu..tangu zamani watu walikua wanajifunguaje tangu enzi na enzi mpaka ukazaliwa wewe leo na kupata muda wa kutype hapa jf?

Shida watu wa afya mnajipaga umuhimu mkubwa sana, yaani mnajikutaga wadogo zake Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania kuna tatizo moja ambalo mimi silielewi kabisa, inawezekanaje watu mna elimu sawa mmoja alipwe pesa nyingiiiiii kuliko mwingine kwa sababu ambazo azieleweki?

Kwa mfano Mhasibu wa cheti wa bandarini anakuwa na mshahara mkubwaaa kuliko hata mhasibu wa diploma wa taasisi kama hospital au mashuleni. Hili linawezekanaje?

Inakuaje mlinzi wa getini bandarini analipwa pesa kubwa kuliko CO au Muuguzi au mwalimu wakati yeye ni ngazi ya cheti tu?

Kwanini mshahara upangwe kutokana na uzalishaji na sio mpangilio mzuri? Kwanini mishaara isifanane kutokana na elimu?

Hii habari ya huyu anazalisha kingi kuliko huyu ni dharau kwahyo mwalimu hana maana kwenye jamii?
Kwa kuwa umemtaja mwalimu acha nikuitie mwanaharakati wa mchongo ndungu Mpwayungu Village
 
Umeona eeee hili sio sawa hii mishahara imekuwa kimichongo michongo na sababu za upishano huu hata azielewek serikal ilipitie tena lasivyo watu wataiba sana
Sasa daktari ataiba nini, wenzako wana fursa za kuiba makontena na tozo wakishikwa wanamalizana na DPP we ukichukua elf 50 ya mgonjwa ukikamatwa unaishia kudhalilishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani bila madaktari hakuna afya inayoeleweka, tukiumwa tunakufa tu..tangu zamani watu walikua wanajifunguaje tangu enzi na enzi mpaka ukazaliwa wewe leo na kupata muda wa kutype hapa jf?

Shida watu wa afya mnajipaga umuhimu mkubwa sana, yaani mnajikutaga wadogo zake Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahyo leo hii ww unasema doctor hana umuhimu tena ?????
 
Kushindwa kuelewa equation rahisi kama hii, its either we sio daktari au daktari kilaza sana mwenye ego kuliko content, ukiwakilisha wenzako wengi wa kaliba yako ya kujipa umuhimu uliopitiliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa hicho kingereza chako kimekuja vipi hapo humu sio wote tunaojua mfano mm sjasoma kabisa ila kama elimu ndo inamfanya mtu kuwa hivyo ulivyo bas akuna umuhimu wa kusoma tunajadil hapa unaanza kuleta vingereza vyako vya shule ya msingi kuzingua watu
 
Sasa daktari ataiba nini, wenzako wana fursa za kuiba makontena na tozo wakishikwa wanamalizana na DPP we ukichukua elf 50 ya mgonjwa ukikamatwa unaishia kudhalilishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa atuongelei wiz wa mtu hiyo ni juu yake tunaongelea mshahara uliopangwa na serikal sio wiz au posho hayo ayatuhusu sisi kama wiz pia unajumuishwa kwenye mishahara yao hapo sawa ila kama wanaiba kwa siri kama waiz wengine hilo ni juu yao sisi tupo hapa katika mpishano wa mishahara
 
Zinztofautiana kwa umuhimu kwenye uchumi na uzalishaji.
 
Sasa hicho kingereza chako kimekuja vipi hapo humu sio wote tunaojua mfano mm sjasoma kabisa ila kama elimu ndo inamfanya mtu kuwa hivyo ulivyo bas akuna umuhimu wa kusoma tunajadil hapa unaanza kuleta vingereza vyako vya shule ya msingi kuzingua watu

Kumbe kuna vingereza vya shule ya msingi?!

Kumbe vingereza vinazingua watu?!

Wonder shall never end

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom