Kwanini Mkuu wa Majeshi(JWTZ)anatokea Kamandi Moja tu, wakati tuna Kamandi Sita?

Kwanini Mkuu wa Majeshi(JWTZ)anatokea Kamandi Moja tu, wakati tuna Kamandi Sita?

Kila nchi ina mifumo yake ya kijeshi kulingana na geography ya nchi yao ilivyo kwaiyo jeshi linaundwa kulingana na udhaifu na uimara wa mazingira yao yalivyoo sisi TZ askari wengi lazima wapate mafunzo ya infantry na ndiyo msingi wa jeshi letu ulivyo kulingana na geografia ya nchi ilivyoo then navy mwisho anga na kamand zote zinafanya majukumu yao makao makuuu hii yote ni kuzuia mapinduzi kama ambayo yalitakaga kutokea nyuma ila kwa sasa naona ni wakati sahihi kwa nchi kulisuka upya jeshi la anga hasa kulingana na vita vya ukrein na mashambulizi ya Irani drone zimekuwa ndyo msingi mpya wa kuanzishwa mashambulizi kwa adui
 
Kwanza kwa Tanzania, ni vigezo gani hutumika ktk kumteua mtu Mwanajeshi kuwa Mkuu wa Majeshi(CDF)?? Je, uchawa haupo kabisa kwenye vigezo vya kuweza kuteuliwa kuwa CDF hapa Tz?

Jaribu tu kufikiria, kama Paul Makonda na umbumbumbu wake pamoja na uhalifu wake alionao ameweza kuteuliwa kushika nyadhifa kubwa kubwa hapa Tanzania Huku wakiachwa watu wengine wengi ambao ni Wasomi, waadilifu na weledi, Je, inashindikana nini kumteua CDF kwa kufuata utaratibu kama huo ambao unaulalamikia????
Mkuu Makonda kaingiaje kwenye Uzi wetu wa Jeshi 😀
 
Kwanza kwa Tanzania, ni vigezo gani hutumika ktk kumteua mtu Mwanajeshi kuwa Mkuu wa Majeshi(CDF)?? Je, uchawa haupo kabisa kwenye vigezo vya kuweza kuteuliwa kuwa CDF hapa Tz?

Jaribu tu kufikiria, kama Paul Makonda na umbumbumbu wake pamoja na uhalifu wake alionao ameweza kuteuliwa kushika nyadhifa kubwa kubwa hapa Tanzania Huku wakiachwa watu wengine wengi ambao ni Wasomi, waadilifu na weledi, Je, inashindikana nini kumteua CDF kwa kufuata utaratibu kama huo ambao unaulalamikia????
Hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa nimecheka sana , maanina na juzi akaharisha mbele ya Rais kule Arusha eti kuna mawaziri wanamhujumu Rais.
 
Mkuu! Kwani Makao Makuu si ndiyo kuna Wakuu wa Kamandi zote au?
Lakini ngoja waje wataalamu wa mambo ya kijeshi waseme vizuri.
asante kwa kumsaidia kabla ya kusoma comment nilitaka kumjibu ila nashukuru umemaliza.
Yaani ni kama haielewi kuwa wizara zote zinapatikana makao makuu DODOMA
 
Vigezo sio kupokezana tu kama mnapokezana jeneza kwenye msafara viko vingi.Kenya nako Kuna shida.Kuna generali siku za karibuni tu alipelekwa Kongo kwenda kuongoza operation ya Majeshi ya Kenya kupambana na M23 akakimbia vita analalamika kuwa wanataka M23 kumuua akarudi Kenya .Sasa alivyoenda vitani alifikiria Nini kule anaenda kucheza mziki au?

Mkuu wa Majeshi huchaguliwa pia Kwa kuangalia uwezo wake kivita je alishawahi ongoza operation ngapi za kivita na zikafanikiwa? Kwenye eneo lake? Kuna vyeo aweza panda Kwa kikawaida tu kuwa umefanya kazi miaka hii na kuhudhuria Kozi au elimu shika.Cheo .Mkuu wa majeshi CV yake kivita lazima ionyeshe mafanikio ndani na nje ya nchi anayaweza ? Umetumwa kupambana na M23 ,operation za Jeshi sijui Dafur Nk .Historia Yako kivita ikoje eneo lako la ubobezi liwe anga,ardhini,military intelligence,baharini nk kivita ukoje? Mfano nilisoma mahali Kuna makamanda wa kamandi walishawahi twangana ngumi na mwenzie wa kamandi ya anga na majini baada ya kikosi Cha majini kufanya vibaya vita ya Uganda na Tanzania kikosi kilazamishwa na majeshi ya Idd Amin Cha majini sababu ya utendaji mbovu vitani wa kamandi ya majini ziwa Victoria walipokuwa wakivuka kukabili majeshi ya Uganda yaliyovamis Tanzania na kumpa kazi ngumu ya ziada kamanda wa Anga kufanya kazi extra kuokoa jahazi

Yule kamanda wa kamandi ya majini ilibidi aondolewe vitani arudishwe kambini.Suala Sio tu ukuu wa kamandi

Pia Kuna swala la umri Unakuta mkuu mwingine wa kamandi umri unemtupa mkono anafikia ku kustaafu

Wengine Kwa kuona uzito wa hiyo kazi hugoma.Mkuu wa Majeshi Hana muda wa kulala akiwa mdogo mno sababu ni mkuu wa Majeshi yote yawe polisi,JWtZ,Usalama wa Taifa nk na wote hueakilisha ripoti kwake Kila siku na muda wowote kukiwa na swala lazima atafute Kwa maamuzi na maelekezo yake
Ndiko.maana sio rahisi Kumkuta mkuu wa Majeshi wa Tanzania mnene ila wale wa chini yake waweza Kuta wako wanene wengi tu
Duuu unamaanisha DG wa tiss Kila siku anaripoti kwa mkuu wa majeshi?
 
Tofauti ya Kamandi ni majukumu tu.
Mfano:
Kamandi ya MMJ ni Utawala wa Jeshi
Kamandi ya Anga ni Ulinzi wa Anga
Kamandi ya Nchi Kavu ni Ulinzi wa Ardhini
Kamandi ya Majini ni Ulinzi wa Majini
Kamandi ya JKT ni Ujenzi wa Taifa
Kamandi ya Mgambo ni Askari wa Akiba
Umetisha sana, Ila Sasa mi huwa nawazaga mbali kwa Sisi tusiojua lolote, Maana mi hata mgambo Sijawai kwenda, Kwenda mstarini Shule ya msingi nilikua nao usumbufu mtupu.
Haya Mambo ya Jeshi ndo sijui Chochote. Naona Yuniform za Jeshi, na sign/ wanazovaa mabegani sijui Hata maana yake... Hilo neno CDF nililisikia kwa Mara ya kwanza alipokufa Magufuli...
 
JKT ni JWTZ, kitu ambacho hujajua JKT ni chuo cha mafunzo (maandalizi) tu, wale ma kuruta na private ndio jkt, akishaajiriwa ni JWTZ au TPDF,mengine ni vitengob tu. Mavazi, vitambulisho na kila kitubni TPDF. jkt ina baki kama kituo cha mafunzo na uzalishaji tu
Nimesoma nimepata Elimu kumbe ndo hivyooooo
 
Haya Mambo ya Jeshi ndo sijui Chochote. Naona Yuniform za Jeshi, na sign/ wanazovaa mabegani sijui Hata maana yake... Hilo neno CDF nililisikia kwa Mara ya kwanza alipokufa Magufuli
Pata muda ujielimishe hapa
👇
Screenshot_20250120-122637_Facebook.jpg

Screenshot_20250120-122652_Facebook.jpg
 
Habari, kwanza kabisa nitoe salam zangu za pole kwa majirani zetu Kenya kwa msiba wa CDF na wafuasi wake katika ajali ya ndege ya kivita iliyotokea tarehe 19/04/2024 wakiwa katika ziara za kikazi.

Baada ya kifo cha Mkuu wa Majeshi wao (CDF) nimetokea kuvutiwa sana na utaratibu wa majirani zetu baada ya uteuzi wa CDF mpya kuteuliwa kutoka kamandi ya majini (Navy).

Swala hili likanivutia sana nikaamua kuwafuatilia kidogo, nikagundua kumbe wao wana utaratibu wa kupokezana kwa kila kamandi kutoa CDF.

Swali langu, Je mbona huku kwetu asilimia kubwa kama si zote tunatoa Mkuu wa majeshi (CDF) kutoka Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi (MMJ) pekee?

Ina maana hizi Kamandi nyingine kama Kamandi ya Nchi Kavu, Kamandi ya Anga, Kamandi ya Majini, Kamandi ya JKT na Kamandi ya Mgambo Mkuu wa Majeshi hawezi kutokea huko?

Naomba kuwasilisha.
mgambo watoe CDF? lazima umevuta SKANKA!!
 
Back
Top Bottom