Kwanini Mo Anapata Hasara Simba, Yanga wanapata Faida?

Nakubaliana nawe hapo kwenye ripoti ikaguliwe kabla kufikishwa mkutanoni kama ilikuwa bado haijakaguliwa.
Hapo kwenye riba umejuaje kama haikujumuishwa kwenye kufikia hiyo FAIDA iliyoripotiwa au ripoti umeiona mwenzetu?
Mkeka mzima uliwekwa pale na nimeuona, wameweka mapato na matumizi, hakuna "item" ya matumizi ambayo unaweza kusema riba ya mkopo ilikuwa imeingizwa humo, labda mkopo waliuchukulia msikitini na cha kushangaza zaidi riba ndiyo ilitakiwa ionyeshwe katika ule mkeka na siyo mkopo wenyewe.
 
Mbona nimekupostia BS inayoonyesha accrue expenses? Au hujui hizo accrue zilishatambuliwa kwenye Income statement ndo zikawepo hapo. Soma hiyo BS hapo kulipowekwa yellow ni accrue expenses. Inaweza kuwa mishahara pia. View attachment 2668117

Income statement utaona kama gharama za mwaka husika na sio mkopo. Inaenda kwenye BS sheet siku unalipa uta Dr Accrue, na uta Cr Cash bila kuitambua kama gharama kwa mara nyingine.

Kuhusu ualimu Mimi sijui hata ualimu unafananaje, uhasibu nimeujua kutoka kwenye biashara zangu nikiwa na wahasibu wanaoniandalia hesabu na wakati wa discussion na TRA kila mwaka baada ya examination zao. Pia katika ujana nilibahatika kufanya kazi kwa ukaribu na accounts departments za baadhi ya kampuni.
Kwa hiyo wewe kwa ufahamu wako Balance Sheet ndiyo inatumika kuangalia kama kampuni imepata faida au hasara? Na sijui kwa nini unazungumzia mishahara, mimi wapi nimegusia mishahara?

Ukiwa tayari kujishusha, niambie nikuelekeze utanishukuru baadae.
 
Kwa hiyo wewe kwa ufahamu wako Balance Sheet ndiyo inatumika kuangalia kama kampuni imepata faida au hasara?
Balance sheet inatumika kuonyesha mali na madeni ya chama ila madeni ya chama yanayotokana na matumizi mfano mishahara yanatambuliwa katika mwaka husika yanapotokea sio siku fedha inalipwa. Hivyo, yanapotokea yanaathiri moja kwa moja mapato na matumizi kama hayajalipwa yanakuwa accruel kwenye balance sheet na yataondoka yatakapolipwa.
 
Umekalia tu kuongelea accrual (na siyo accruel). Nadhani unacopy na kupaste maelezo uliyotumiwa zamani ndiyo maana hayaendani na mada inayozungumzwa.
 
Kwa hiyo wewe kwa ufahamu wako Balance Sheet ndiyo inatumika kuangalia kama kampuni imepata faida au hasara? Na sijui kwa nini unazungumzia mishahara, mimi wapi nimegusia mishahara?

Ukiwa tayari kujishusha, niambie nikuelekeze utanishukuru baadae.
Naomba nikupe mfano mwepesi sana halafu naachana na wewe iwapo hutoelewa.

OFISI NDOGO MPYA INA MTAJI WA TSH 1000. BIASHARA IMEANZA MWAKA 2022 JANUARY.

MAPATO YAO NI TSH 500. MATUMIZI YAO NI TSH 200, KATIKA HIYO 200 MISHAHARA NI TSH 100 AMBAYO MPAKA KUFIKIA MWISHO WA MWAKA HAIJALIPWA. HESABU ZAO ZITAKUAJE?

INCOME STATEMENT:
MAPATO TSH 500
TOA:
MATUMIZI TSH 200
FAIDA TSH 300.
KODI TSH 90

BALANCE SHEET:
ASSET / CASH TSH 1210

CAPITAL TSH 1000
RESERVE TSH 110
LIABILITIES:
MISHAHARA TSH 100
TOTAL TSH 1210

Hapo utaona kuwa Tsh 100 ya mishahara ambayo haijalipwa imetambuliwa kama matumizi kwa mwaka 2022 lakini pia imeenda kuwa deni/Accrue kwenye balance sheet.

Huu mfumo ndio unaotumika ili uweze kulipa kodi halisi ya mapato ya mwaka husika kwa sababu unakusaidia kuitambua faida yako halisi kwa mwaka husika bila kujali umeshafanya malipo ya gharama zako au la. Hujalipa mishahara ya Tsh 100 ila umeiweka kwenye matumizi yako na faida kubaki Tsh 300 hivyo 30% ya 300 ni kodi stahili. Usipoitambua tsh 100 utakuwa na faida ya Tsh 400 isiyo halisi halafu kodi itaongezeka.

Natumai tumeelewana.
 
Ninacho wakubali Kolo FC kwenye mambo ya Yanga huwaga wanajua kila kitu ,kwenye sheria wapo kwenye uhasibu wapo.

Ila inawezekana kweli kwenye uhasibu wapo vizuri na ndio maana kila wakipigwa wanaulizia bil 20 zao.
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Umekalia tu kuongelea accrual (na siyo accruel). Nadhani unacopy na kupaste maelezo uliyotumiwa zamani ndiyo maana hayaendani na mada inayozungumzwa.
Sasa unaanza kunifundisha lugha tena boss? Ndo maana nilikupa angalizo kuwa kuwa mpole ili ninachofahamu nikuambie ukifahamu. Sasa nimeshakuelewa unataka kushinda majibizano.
 
Kuna vitu vya kishabiki na vitu vya taaluma sasa mtu ana changanya mambo
Unajua Ukipika pika hesabu kukwepa gharama za wahasibu CPA bila kujali halafu ukapigwa kodi ya maana na TRA lazima kichwa kikuume halafu next time utataka kujua what happened? Hesabu za miaka ya mbele utazidisha umakini, baada ya miaka kadhaa ya biashara unajikuta uhasibu unaujua kwa kiwango fulani.

Sasa tatizo ni pale unapojaribu kumueleza mwenzako uzoefu wako halafu anakudharau kabisa.
 
Mkeka mzima uliwekwa pale na nimeuona, wameweka mapato na matumizi, hakuna "item" ya matumizi ambayo unaweza kusema riba ya mkopo ilikuwa imeingizwa humo, labda mkopo waliuchukulia msikitini na cha kushangaza zaidi riba ndiyo ilitakiwa ionyeshwe katika ule mkeka na siyo mkopo wenyewe.
Kama usemayo ni kweli basi tupo pamoja.
 
Ninacho wakubali Kolo FC kwenye mambo ya Yanga huwaga wanajua kila kitu ,kwenye sheria wapo kwenye uhasibu wapo.

Ila inawezekana kweli kwenye uhasibu wapo vizuri na ndio maana kila wakipigwa wanaulizia bil 20 zao.
Alafu mudy ametoa billion 20 kununua hisa za simba ambazo anauhuru wa kudumu nazo hata milele

Yanga kwa mwaka wanaingiza billion 17 ukifanya comparison utaona mambo mengine yanakera sana hata kama sio mshabiki wa simba sababu anawafanya watu kama watoto wadogo
 
Naomba nikupe mfano mwepesi sana halafu naachana na wewe iwapo hutoelewa.

OFISI NDOGO MPYA INA MTAJI WA TSH 1000. BIASHARA IMEANZA MWAKA 2022 JANUARY.

MAPATO YAO NI TSH 500. MATUMIZI YAO NI TSH 200, KATIKA HIYO 200 MISHAHARA NI TSH 100 AMBAYO MPAKA KUFIKIA MWISHO WA MWAKA HAIJALIPWA. HESABU ZAO ZITAKUAJE?

INCOME STATEMENT:
MAPATO TSH 500
TOA:
MATUMIZI TSH 200
FAIDA TSH 300.
KODI TSH 90

BALANCE SHEET:
ASSET / CASH TSH 1210

CAPITAL TSH 1000
RESERVE TSH 110
LIABILITIES:
MISHAHARA TSH 100
TOTAL TSH 1210

Hapo utaona kuwa Tsh 100 ya mishahara ambayo haijalipwa imetambuliwa kama matumizi kwa mwaka 2022 lakini pia imeenda kuwa deni/Accrue kwenye balance sheet.

Huu mfumo ndio unaotumika ili uweze kulipa kodi halisi ya mapato ya mwaka husika kwa sababu unakusaidia kuitambua faida yako halisi kwa mwaka husika bila kujali umeshafanya malipo ya gharama zako au la. Hujalipa mishahara ya Tsh 100 ila umeiweka kwenye matumizi yako na faida kubaki Tsh 300 hivyo 30% ya 300 ni kodi stahili. Usipoitambua tsh 100 utakuwa na faida ya Tsh 400 isiyo halisi halafu kodi itaongezeka.

Natumai tumeelewana.
Wewe bwana, utakuwa comedian. Mbona jambo rahisi unataka kulifanya gumu kwa maelezo na mifano mingi isiyoendana na tunachozungumza hapa?

Kama umeweza kupata Balance Sheet ya Starbucks, haushindwi kupata Income Statement ya Starbucks au ya kampuni nyingine yoyote ile duniani ambayo inaonyesha kuwa Mkopo umewekwa kwnye list ya Mapato kama walivyofanya Yanga. Nimekwambia ukiweza kuipata hiyo statement tunafunga mjadala.

Hakuna anayezungumzia mshahara hapa, usikariri mambo ndugu yangu.
 
Sasa unaanza kunifundisha lugha tena boss? Ndo maana nilikupa angalizo kuwa kuwa mpole ili ninachofahamu nikuambie ukifahamu. Sasa nimeshakuelewa unataka kushinda majibizano.
Ukishaona mtu anaanza kukimbilia kwenye typing error ujue hapo hamna kitu sababu hoja dhaifu wakati mnaongea mambo muhimu
 
Mbona jambo rahisi unataka kulifanya gumu kwa maelezo na mifano mingi isiyoendana na tunachozungumza hapa?

Kama umeweza kupata Balance Sheet ya Starbucks, haushindwi kupata Income Statement ya Starbucks au ya kampuni nyingine yoyote ile duniani ambayo inaonyesha kuwa Mkopo umewekwa kwnye list ya Mapato kama walivyofanya Yanga. Nimekwambia ukiweza kuipata hiyo statement tunafunga mjadala.

Hakuna anayezungumzia mshahara hapa, usikariri mambo ndugu yangu.
We endelea kubisha ukweli ni kwamba wenzenu wanapata faida, nyie tajiri wenu analalamika kila siku anapata hasara mpaka aliita waandishi wa habari
 
Mwezi uliopita mliambiwa zawadi walizovuna Yanga msimu huu ni 11B, baadhi tukabisha ila tukajibiwa hivi hivi "tuache ubishi na ujuaji". Leo wanakuja kuambiwa zawadi zote ni 1B.

Kwani Dewji aliposema anapata hasara alikuwa anaongelea taasisi gani?
 
Mwezi uliopita mliambiwa zawadi walizovuna Yanga mwaka huu ni 11B, baadhi tukabisha ila tukajibiwa hivi hivi "tuache ubishi na ujuaji". Leo wanakuja kuambiwa zawadi ni 1B.

Kwani Dewji aliposema anapata hasara alikuwa anaongelea taasisi gani?
Onyesha hio taarifa rasmi ya Yanga inayosema zawadi ni billion 11 waliosema mwezi uliopita nimekaa pale nasubiria
 
Nikikupa hiyo taarifa rasmi itabadili nini? Mbona hapa tunajadili taarifa rasmi lakini bado mnasema "tuache ubishi". Wewe unaamini Yanga inastahili kupata mapato ya 300M kwa mauzo ya jezi ya msimu mzima? Hiyo ni taarifa rasmi.
 
Back
Top Bottom