Kwanini mtaani kuna dhana mbaya kuhusu ndugu?

Kwanini mtaani kuna dhana mbaya kuhusu ndugu?

Utasikia;

1. Usikae na ndugu yako ni shida
2. Usiajiri ndugu utakuja kulia
3. Ndugu ni wa kukaa nao mbali na nyingine nyingi

Nafikiri umoja kwa familia na undugu wa damu ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya jamii zetu. Tusitegemee kupata maendeleo kama taifa endapo jamii hasa ndugu hawawezi kushirikiana kwenye uzalishaji mali na kazi, hili ni tatizo kubwa sana.

Hebu tutoe maoni huku tukiangalia mifano ya biblia; Kaini na Abeli, Yacobo na Esao, Daudi na ndugu zake, Yusuph na ndugu zake, Isaka na Ishmail, Israel na Palestine.
Kwa hiyo
Unajifanya hujui,?
 
Ndugu wanazingua sana hata umuitie kazi kaa ukijua uwezekano wa kukuangusha ni zaidi ya 75%.

Mwaka flani sio zamani, nilikuwa na kikazi changu mahala nikamuita ndugu yangu apate rizki yeye ni fundi wa kuweka tiles (assume hivyo).

Tukaongea bei akaizidisha mara mbili ya bei ya soko nikamtazama nikasema sio shida acha apate ni jamaa yangu haina neno.

Shida ilianza nje ya malipo yetu hata pesa alichukua ya kununua vifaa alinipiga parefu, kwenda site anataka nilipe nauli, ikifika muda wa msosi anataka nilipie chakula, akienda lodge anataka nilipe mimi lodge.

Kifupi anataka siku anamaliza kazi ela zake ziwe kama zilivyo, kumbuka kabla ya kuanza kazi nilimpa advance payment.

Alifanya robo kazi, alipoondoka nikamwambia sikilizia nitaongeza vifaa kisha nitakucheki uje.

Hiyo ikawa jumla nikampotezea akawa anapiga simu sipokei. Ile kazi ilikamilishwa na mtu baki tena kwa nusu ya ile bei aliyotaka ndugu yangu.

Mifano ya ndugu iko mingi sana, nilishajaribu kuishi na ndugu kutoka kwetu kijijini ili niwasaidie ndio kwanza niliharibu kabisa nikajuta.
 
Napenda sana kuishi na ndugu na toka mwanzo nilikuwa nasema hivyo kabla sijaoa
Ila ajabu hao ndugu/watoto wa ndugu ambao naishi nao wamekuwa kiburi na hata akielekezwa kazi na wife wanakuwa na dharau za wazi nimeshuhudia akimjibu hovyo wakati huo hakujua kama nipo mpaka unakuta mke analia.

Tofauti na nilivyotarajia ndugu wakati mwingine changamoto kuishi nao japo sio wote

NB: Naishi na watoto wa ndugu watatu ila mmoja namtimua muda sio mrefu na najua ndugu wataongea sana maana nimemuonya mara kadhaa ila amekataa kubadilika
 
Shida ya ndugu ni kuwa kuna ambao walishuhudia unazaliwa so muda wote wanahisi we ni mtoto. Na kuna ambao waliteseka wote na wewe Wakat wa ukuaji so wanachukulia chochote unachofanya cha maendeleo uwafanyie na wao so kuna ile wewe ni kijana umefanikiwa kuna wakubwa kwenye familia walichemka so wanahic unajiona kwasababu amefanikiwa so the better way ni kukaa kimya na mbali na watu ulitumikie kusudi Mungu aliloweka ndani yako.
 
Napenda sana kuishi na ndugu na toka mwanzo nilikuwa nasema hivyo kabla sijaoa
Ila ajabu hao ndugu/watoto wa ndugu ambao naishi nao wamekuwa kiburi na hata akielekezwa kazi na wife wanakuwa na dharau za wazi nimeshuhudia akimjibu hovyo wakati huo hakujua kama nipo mpaka unakuta mke analia.

Tofauti na nilivyotarajia ndugu wakati mwingine changamoto kuishi nao japo sio wote

NB: Naishi na watoto wa ndugu watatu ila mmoja namtimua muda sio mrefu na najua ndugu wataongea sana maana nimemuonya mara kadhaa ila amekataa kubadilika
Timua hakuna namna
 
Hilo nalo ni tatizo sana maana kuna uwezekano mkubwa wa uaminifu huo kupotea kwa muda mfupi tu....Nina experience na Hilo jambo yupo jamaa amekosa nyumba kabisa kumwamini mtu baki bila ndugu kujua
sina tamaa kabisa bro huu mwaka wa saba sasa nasimamia mali zake nilishakaa na milioni 150 zake miezi sita sikuchukua hata senti, narudia tena waafrica wengi uaminifu 0%
 
Habari Wakuu!
Naomba kuchangi mada kama ifuatavyo;
1. Usikae na ndugu yako ni shida
Hili lipo wazi kwani ndugu wengi hawana kabsa mshipa wa shukrani haswa pale ambapo anaona msaada wako kwake ni lazma na sio ombi. Ndugu zetu wengi ni matatizo matupu mkuu, katika ndugu zako 10 ukitazama vyema utaona kuna ndugu 6 au 7 ambao ni chenga za vitumbua kabsa.
2. Usiajiri ndugu utakuja kulia
Ukitaka kula short na hasara kubwa basi ajiri ndugu yako! Tena mwafrika ambaye ni mbinafsi na anataka kuendelea kwa kupitia mgongo wako. Ni hatari kubwa sana.
3. Ndugu ni wa kukaa nao mbali
Ukitaka maendeleo basi kaa mbali na ndugu, waache mita mia kabsa, kwa sababu ukipata nafasi ya kimaendeleo basi watajazana kwa wingi kuja kukuomba msaada ila ukifulia na kuchoka hutoona hata mmoja akiwa machoni mwako.
Take Home yangu!
Tafuta ndugu wachache ambao wapo timamu kabsa na fanya kuwageuza marafiki zako hapo utapiga bingo!
 
Kaka angu aliajiti bdugu upande wa mke wamsaidie magari kilichotokea had hata gari moja zima
 
Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake...

Ikiwa na maana ndugu yako ndio adui yako maana anakujua sana.

Mtu asiyekujua hawezi kukudhuru.
 
Utasikia;

1. Usikae na ndugu yako ni shida
2. Usiajiri ndugu utakuja kulia
3. Ndugu ni wa kukaa nao mbali na nyingine nyingi

Nafikiri umoja kwa familia na undugu wa damu ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya jamii zetu. Tusitegemee kupata maendeleo kama taifa endapo jamii hasa ndugu hawawezi kushirikiana kwenye uzalishaji mali na kazi, hili ni tatizo kubwa sana.

Hebu tutoe maoni huku tukiangalia mifano ya biblia; Kaini na Abeli, Yacobo na Esao, Daudi na ndugu zake, Yusuph na ndugu zake, Isaka na Ishmail, Israel na Palestine.

Uko sahihi.

Mcheza kwao ‘hutunzwa’.
 
Back
Top Bottom