Ukiangalia na kuchunguza kisa kizima cha kuzaliwa Yesu, unamshangaa yeye, mama yake, baba yake hata Mungu wake. Eti bikra alipata mimba kwa roho mtakatifu! Hii maana yake nini wakati tunaambiwa roho ya Mungu ilimfunika Maria. Kama kweli ilimfunika, nani anajua kilichofanyika wakati amefunikwa? Je hii ndiiyo ilikuwa njia pekee ya 'kufanya miujiza uchwara'? Kwanini kumsumbua binti watu kama ni kweli wakati Yesu angeshuka kama malaika Gabriel au vibwengo vingine? Kama haitoshi, kuna baadhi ya wajinga wanamuita Maria mama wa Mungu kana kwamba Mungu anaweza kutosha kwenye tumbo la mwanamke. Kama kweli mwanae ni Mungu, je alipokuwa na mimba, dunia haikuwa na Mungu? Naomba tuelimishane juu ya hili wnangu.
Warumi na Wayunani walitunga uongo kuwa Yesu alizaliwa bila ya baba bali ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Ktk kitabu chao Biblia +Injili hawakutaka kuandika kwa kirefu kuhusu ukoo wa Mariamu na wa Yusufu. Pia, hawakupenda kuelezea kwa undani zaidi kuhusu uhusiano wao (Yusufu na Mariamu). Yaani hapa waliamua kufukia-fukia kwa lengo la kutimiza mpango wao.
Kama ukibahatika kukutana na Mapadri, Maaskofu, Wachungaji au Wainjilisti wasomi na walioamua kuasi... Watakueleza ukweli kuwa, Mariamu alipewa mimba na Yusufu kabla ya ndoa. Wazazi wa Mariamu (mzee Yoakimu na bibi Anna), waliamua kumfukuza binti yao (Mariamu) nyumbani, kwaajili ya kutimiza Sheria na taratibu za Kiyahudi.
Alifukuzwa na aliondoka kusikojulikana yeye pamoja na mume wake 'mtarajiwa' Yusufu, huko walipofikia (kwakuwa walikuwa ni wageni) waliamua kuhangaika kutafuta nyumba za kulala wageni... Wazee wa Kiyahudi, (walioitwa 'mamajusi') kwa lengo la kutimiza Sheria na Taratibu za Kiyahudi, waliamua kumtafuta Mariamu ili wamuue kutokana na kuasi Sheria za Torati.
Waliamua kutokomea mpaka nchini Misri, kwaajili ya kujihifadhi-kuepukana na fedheha! Kwa muda wa miaka 13. Huko pia, (Yusufu na Mariamu) walizaa watoto wengine wanne (Yakobo, Yuda, binti Yoana na binti Yose). Mzee Yusufu baba yake aliitwa mzee Yakobo, hivyo aliamua kutumia herufi 'Y' kwaajili ya majina ya watoto wake (Yesu, Yakobo, Yuda, Yoana na Yose).