Ukiangalia na kuchunguza kisa kizima cha kuzaliwa Yesu, unamshangaa yeye, mama yake, baba yake hata Mungu wake. Eti bikra alipata mimba kwa roho mtakatifu! Hii maana yake nini wakati tunaambiwa roho ya Mungu ilimfunika Maria. Kama kweli ilimfunika, nani anajua kilichofanyika wakati amefunikwa? Je hii ndiiyo ilikuwa njia pekee ya 'kufanya miujiza uchwara'? Kwanini kumsumbua binti watu kama ni kweli wakati Yesu angeshuka kama malaika Gabriel au vibwengo vingine? Kama haitoshi, kuna baadhi ya wajinga wanamuita Maria mama wa Mungu kana kwamba Mungu anaweza kutosha kwenye tumbo la mwanamke. Kama kweli mwanae ni Mungu, je alipokuwa na mimba, dunia haikuwa na Mungu? Naomba tuelimishane juu ya hili wnangu.
SOMA ISAYA 9:6
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,Tumepewa mtoto mwanamume;Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;Naye ataitwa jina lake,Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,Baba wa milele, Mfalme wa amani.
SOMA PIA
Isa 53:5
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,Alichubuliwa kwa maovu yetu;Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
SOMA PIA
Yn 1:1-14
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru. Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
SOMA PIA
Kuzaliwa Kwa Yesu Kwatabiriwa
26 Miezi sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alim tuma malaika Gabrieli aende katika mji wa Nazareti, ulioko Gali laya, 27 kwa msichana bikira aliyeitwa Mariamu. Yeye alikuwa ameposwa na mtu mmoja aliyeitwa Yusufu, wa ukoo wa Mfalme Daudi.
28 Malaika Gabrieli alimtokea Mariamu, akamwambia: “Sal aamu, ewe binti uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!”
29 Mariamu alifadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, maana ya salamu hizi ni nini. 30 Ndipo malaika akamwam bia, “Usiogope, Mariamu, Mungu amependezwa nawe. 31 Sikiliza, utapata mimba, nawe utazaa mtoto wa kiume; na utamwita jina lake Yesu. 32 Mtoto huyo atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Mfalme Daudi, baba yake. 33 Atatawala juu ya nyumba ya Yakobo daima; na ufalme wake hau takuwa na mwisho!”
Maneno ya Mungu yanaoonyesha kuwa YESU ni mfalme ,tena mwana wa MUNGU ni mengi. kuwezi kushangaa kwamba alizaliwaje kama unaamini katika uumbaji wa MUNGU
Ebu jiulize ,ADAMU NA EVA wazazi wao ni kina nani?
Isaka alizaliwa na bibi wa miaka 90 ,aliacha kuona siku zake .maana yake mayai yeye kutunga mimba yalishakwisha kitambo
Kuzaliwa kwa Isaka
mwazo 21:1-3
1 BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema. 2Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu. 3Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia.
YESU Kuzaliwa kama mwandamu ulikuwa ni mpango mkakati wa kukomboa mwanadamu ,na ADAMU pia aliyekosea akiwa pale edeni.YESU aliitaji kuvaa mwili ali ajue matatizo ya sisi wanadamu.ndiyo maana naye alijaribiwa kama sisi wanadamu ,aliomba kama sisi wanadamu tunavyotakiwa kuomba.KAMA angeshuka kama malaika bado watu wasiyoamini kama wewe wangesema ni pepo au jini.pia sisi wanadamu ytungekuwa tunajitetea kuwa tunatenda dhambi kwa sbabu tumevaa mwili lakini YESU hakutenda dhambi kwa sababu hakuzaliwa kama sisi binadamu.sasa YESU alivaa mwili ili aelewe shida zetu na kuzipeleka pale msalabani
Yohana 16:33
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Kwa nini alisema duniani mnayo dhiki? ni kwa sababu naye alipata dhiki sana akiwa hapa duniani.Alisingiziwa mengi sana ya uongo,shetani alimjaribu kwa njaa,kupenda madaraka,na kumjaribu MUngu .
MATHAYO 4:6
Akamwambia Yesu, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe mpaka chini! Kwani Maandiko yanasema, ‘Mungu atawaamuru malaika zake wakusaidie, na mikono yao itakupokea, ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.’”
YESU alivaa mwili ya binadamu ili atufundishe kuomba .
Luka 6:12
Ikawa katika siku hizo Yesu alikwenda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.
Alivaa mwili wenye udhaifu mwingi ,ili atuonyeshe namna ya kuushinda mwili
Mk 14:38
Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu.
MWANADAMU unatakiwa ujue kuwa kuna falme mbili ambazo zinapinga.UFALME WA SHETANI ambao mkuu wake ni shetani ,ibilisi ,nyoka wa zamani . ana watu wake ,mawaziri wake na watendaji wakuu wake amabayo ni mapepo na majini.Ana pia wasaidizi wake wanaomsaidi kupiga kapeni ili aendelee kukaa madarakani kama mfalme wa giza.machawa wake ni binadamu ambao matendo yako ni dhahiri nayo ndyo haya :
GALATIA 5:19-21
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: uasherati, uchafu, ufisadi, 20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha waonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama haya, hawataurithi Ufalme wa Mungu.
MACHAWA WA IBILISI ,AMBAO NA WEWE MTOA MAADA UMO ,MSHAHARA WAO SIKU YESU ATAKAPOKUJA KUHUKUMU ULIMWENGU ,NI KUTUPWA KATIKA MOTO WA MILELE
Ufu 22:15
Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
UFALME WA MUNGU ,NI MKUSANJIKO WA MATENDO MEMA.KATIKA UFALME WA MUNGU KULE KUNA RAHA NA UZIMA WA MILELE.MACHAWA WA MUNGU MATENDO YAO NI YA AMANI NA FURAHA SANA.
Sifa na Heri
MATHAYO 5 :1-12
1 Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; 2akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema,
3 Heri walio maskini wa roho;
Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4 Heri wenye huzuni;
Maana hao watafarijika.
5 Heri wenye upole;
Maana hao watairithi nchi.
6 Heri wenye njaa na kiu ya haki;
Maana hao watashibishwa.
7 Heri wenye rehema;
Maana hao watapata rehema.
8 Heri wenye moyo safi;
Maana hao watamwona Mungu.
9 Heri wapatanishi;
Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki;
Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. 12Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Yakobo 1:27
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
Mt 25:35-40
kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
MACHAWA WA MUNGU WAO MSHAHARA WAO NI UZIMA WA MILELE
Ufu 21:4
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Ufu 14:13
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Kama uatitaji kujifunza zaidi juu ya YESU na UFALME WA MBINGUNI ,nitafute nikupe namba yangu ya simu au email kwa mawasiliano zaidi
KARIBU KWA YESU UPONE JEHANAMU YA MILELE