Kwanini Mungu alimuumba Yesu kiharamu kama kweli alifanya hivyo badala ya kumshusha kama malaika?

Haya Kuhusu
 
Una mawazo ya kishetani, mambo ya Mungu hayachunguziki kwa akili za kibinadamu
 
Alitaka kudhihirisha ukuu wake!Mungu hachunguziki Wala kazi zake hazina kipimo,Huenda atakavyo!
 
Cha msingi endelea kuamini unachoamini wewe. Imani sio sayansi. Na njia za Mungu sio za kama za Wanadamu.
 
mode do the needful, hili ni jukwaa la siasa
P
 
Mungu alitumia manabii kuongea na mwanadamu lakini ilifikia wakati manabii hawa walipata wakati mgumu mno kufikisha ujumbe kwa wanadamu na ukakubalika.

Mungu akaona njia pekee ya wokovu ya uhakika wa milele ni yeye mweyewe kuja duniani kwa kutumia nafsi ya uungu ili azaliwe kama mwanadamu wa kawaida, aishi, akue ili watu wamuone na wahakikishe yeye ni Mungu kweli.

Kwa hiyo Yesu ni yeye Mungu!!
 
Ni ngumu sana kujificha kwenye kichaka cha Utatu au Divinity of Jesus, kichaka ni chepesi kukinga mashambulizi ya questioning and reasoning.
Sijui waliokijenga hiki walituonaje, labda kwa sababu enzi hizo kulikuwa na nguvu ya dola hivyo watu hawakupewa uhuru wa kuhoji!
 
Mnatuchanganya ashuke Mungu mwenyewe yupi Tena!
Si Mungu alishakuja kwa kiwiliwili au Yesu sio Mungu?
Huyo kwenye picha siyo Yesu ni muigizaji wa Yesu, isipokuwa ni kweli Yesu halisi alishakuja duniani kwa njia ya kuzaliwa na wengi walimkataa kama wanavyomkataa mpaka sasa kwa kuwa wana hiari ya kumkataa au kumkubali na wataendelea kuchanganyikiwa kama walivyochanganyikiwa watu wa kwanza,mpaka watakaposhukiwa na neema ya Mungu ndipo watamuelewa Yesu na hawatachanganyikiwa tena.
 
Yesu hana chanzo yeye ndiye chanzo cha chanzo
Kama hana chanzo, unajuaje kama yupo?

Kama yeye alitokea tu ghafla bila kisababishi bhasi inawezekana pia hata ulimwengu nao uliibuka tu bila kisababishi.
 
Kama hana chanzo, unajuaje kama yupo?

Kama yeye alitokea tu ghafla bila kisababishi bhasi inawezekana pia hata ulimwengu nao uliibuka tu bila kisababishi
Kama vilivyoumbwa vipi, basi aliyeviumba asiye na mwanzo yupo
 
Kama vilivyoumbwa vipi, basi aliyeviumba asiye na mwanzo yupo
Hakuna kitu kisicho na Chanzo, chochote kilichopo kina chanzo, Chochote kisichokua na chanzo basi hakipo na hakitakuja tokea bila kuwepo chanzo chake.

Huwezi kusema vitu vimeumbwa na chanzo fulani bila kua na uhakika kama kipo au hakipo.

Hiyo mechanism iliyokitokeza hicho chanzo sio kwamba inaweza pia kuutokeza ulimwengu .

Ulimwengu una chanzo sababu upo, unaonekana, Ila hakuna mtu yeyote wa Dini au Sayansi mwenye uwezo wa kujua chanzo cha ulimwengu sababu wote tumejikuta tupo ndani yake.
 
Nami nakushauri uheshimu akili, ubunifu, na uchokonozi wa watu. Misingi mikuu ya akili ni uchokonozi na utafiti. Bashe kulbali na heshimu misingi hii ya kumkomboa mwanadamu toka kwenye utumwa wa dini.
Kama unaona ni utumwa hiyo ni ufinyu wa akili yako chonganishi, simamia kauli ya awali kwamba heshimu imani ya mwenzako. Kama elimu yako ni duni waweza mfata kiongozi wa dini ili akupe elimu na maarifa zaidi ya imani unayotaka.
 
Warumi na Wayunani walitunga uongo kuwa Yesu alizaliwa bila ya baba bali ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Ktk kitabu chao Biblia +Injili hawakutaka kuandika kwa kirefu kuhusu ukoo wa Mariamu na wa Yusufu. Pia, hawakupenda kuelezea kwa undani zaidi kuhusu uhusiano wao (Yusufu na Mariamu). Yaani hapa waliamua kufukia-fukia kwa lengo la kutimiza mpango wao.

Kama ukibahatika kukutana na Mapadri, Maaskofu, Wachungaji au Wainjilisti wasomi na walioamua kuasi... Watakueleza ukweli kuwa, Mariamu alipewa mimba na Yusufu kabla ya ndoa. Wazazi wa Mariamu (mzee Yoakimu na bibi Anna), waliamua kumfukuza binti yao (Mariamu) nyumbani, kwaajili ya kutimiza Sheria na taratibu za Kiyahudi.

Alifukuzwa na aliondoka kusikojulikana yeye pamoja na mume wake 'mtarajiwa' Yusufu, huko walipofikia (kwakuwa walikuwa ni wageni) waliamua kuhangaika kutafuta nyumba za kulala wageni... Wazee wa Kiyahudi, (walioitwa 'mamajusi') kwa lengo la kutimiza Sheria na Taratibu za Kiyahudi, waliamua kumtafuta Mariamu ili wamuue kutokana na kuasi Sheria za Torati.

Waliamua kutokomea mpaka nchini Misri, kwaajili ya kujihifadhi-kuepukana na fedheha! Kwa muda wa miaka 13. Huko pia, (Yusufu na Mariamu) walizaa watoto wengine wanne (Yakobo, Yuda, binti Yoana na binti Yose). Mzee Yusufu baba yake aliitwa mzee Yakobo, hivyo aliamua kutumia herufi 'Y' kwaajili ya majina ya watoto wake (Yesu, Yakobo, Yuda, Yoana na Yose).
 
Yesu hana chanzo.
 
Ata yesu alipokua anafundisha kwenye Moja ya Masinagogi, katika ufundishaji aliwaambia Yeye alikuwepo kabra ya Ibrahim apo ulitokea mtiti mkubwa.

Maana wao Wana mjua yeye ni mtoto wa juzi tena wa fundi sermala Sasa inakuwaje awepo kabla ya Ibrahim.
Ndicho kinacho endelea katika mabishanobyenu.
Kama mtu amekuja kukejeli na kubishana amta fikia mu afaka.
 
Ndg huwezi kujua jibu LA swali lako mpaka utambue na kujua Mungu ni nani kwa sababu Mungu si kama were na mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…