Ukisoma vitabu vya ngano viitwavyo vitakatifu vinadai kuwa Mungu alimuumba Adam tokana na udongo. Ajabu ya maajabu na kujichanganya, vitabu hivyo hivyo, vinasema:
Mosi, Pili aliumbwa kwa kufinyanga udongo.
Pili, je Mungu tunayesema hafananishwi na chochote, ilikuwaje akaumba kiumbe/viumbe kwa mfano wake kama ni kweli?
Tatu, ilikuwaje akakosa udongo wa kutosha wa kuumbia Eva hadi 'achomoe' ubavu wa Adam?
Nne, je kwanini viumbe wengine wote waliumbwa kuwa kusema kuwa na wakawa isipokuwa ngurumbili?
Tano, je inakuwaje wadudu na wanyama majike hawakutoka kwenye mbavu za madume?
Sita, je tulipigwa changa la macho?
Kabla ha kujibu, jikumbushe amri kumi za "Mungu."
Ni amri gani ambayo hawa washenzi waliotuletea dini hawakkuvunja? Walisema tusiue, wakatuua na kutuuza utumwani, Walisema tuwapende majirani zetu wakaishia kutubagua na kutuchukia hadi leo, Walisema usiibe wakatuibia hadi leo wanapowatoza maskini wetu fedha kwa hadaa mbali mbali kama vile sadaka na zaka na mambo mengine, Walisema tusiseme uongo wakatuongopea kuwa kila kitu cheupe ni safi na cheusi kimelaaniwa, Walisema tusiwe na miungu wengi wakajigeuza miungu wao na mila zao.
Waliseme tusizini wakahalalisha uzinzi kwa njia ya ndoa za mitala na upuuzi mwingine. Walipomaliza kutuibia, wakatwambia tusitamani mali wala mke wa mwenzetu wakati wao waliendelea kuwabaka na kuwazini dada zetu.
Wanangu tusaidiane. Nauliza kuna ukweli humu au changa la mato?