Kwanini Mungu hakumuumba mwanaume akiwa ametahiriwa?

Kwanini Mungu hakumuumba mwanaume akiwa ametahiriwa?

Hili lilikua suala la kimila zaidi na kimaagano.
Ingawa kuna baadhi ya dini au jamii zinachukulia ni ustaarabu
Umesema vyema, it was all good mpaka mzungu alipokuja na kusema mila zetu dawa, mavazi yetu ni ushenzi. Haikuwa shida kwa mababu zetu kabla ya mzungu na dini.
 
Mungu huyo hawezi kunitokea kwa vile Hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Mnatetea kiumbe kisicho kuwepo.

Fiction God, imaginations just an illusion.
Kitu kikiwa illusion inamaana hakipo? Ndoto sio illusion? Haipo? Haina impact katika maisha yasiyo ya illusion?

Hapa ndipo utofauti wa tafsiri ya uwepo wa MUNGU unapotokea. Kutaka kumthibitisha katika ulimwengu usio wa kifikra, kinadharia, kiroho ilihali ulimwengu huo una limitation.
 
Kitaalamu,Ningependa kujua faida za kutahiriwa na hasara za kutotahiriwa .
 
Lakini ilikuwa symbol ya Utakatifu pia kabla paulo hajaja kuitoa
Ni kweli na ndivyo agano la kale lilivyokuwa yaani agano la sheria, ndio maana 'wayahudi' walijiita watu wa 'tohara' .

hata Kanisa la Mwanzo lilipitia mvutano huu kuhusu kuwakubali watu wasio wa tohara kuwa sehemu ya Kanisa.

Rejea kisa cha matendo ya mitume 11:2 pale Petro alipokwenda kwa Kornelio (asiye wa tohara) na wenzake kumnyooshea kidole, ila aliwaelezea kuhusu Yale maono na namna Roho Mtakatifu alivyowashukia wasio wa tohara.

Mtume Paulo kwenye waraka wake kwa Kanisa la Rumi (Warumi 2:25-29) alilieleza Kanisa la Rumi namna tohara ya kale ya mwilini ilivyo tofauti na ya agano jipya ambayo ni ya rohoni.

Warumi 2: 25
Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.

Warumi 2: 26
Basi ikiwa yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! Kutokutahiriwa kwake hakutahesabiwa kuwa kutahiriwa?

Warumi 2 :27
Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati?

Warumi 2 :28
Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;

Warumi 2 :29
bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.

Paulo alionyesha namna ndani ya agano jipya hatufungwi tena chini ya sheria za torati ya kale (ikiwemo tohara) na kwa kuthibitisha hilo hata Roho Mtakatifu aliwashukia nyumba ya Kornelio( wasio wa tohara).

Rabbon
 
Habari Mkuu Proved Za Muda mrefu..
Nafurahi kukuona Tena wewe Na Rabbon ni watu ninaowaheshimu kwa Tasnia ya utetezi wa Dini yenu Hongera sana..

Ila nahisi Bado unapata Ukakasi katika kumuelewa paulo..
Na ndo maana hasa mliandikiwa pia..

2 Petro 3:16

"vile vile kama katika nyaraka zake zote(Paulo) pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe."

Sasa Tuendelee..
Unasema hamfungwi chini ya sheria ila unasahau kuwa Yesu hakusema mahala.popote sheria haikufungi wala kukupa maagizo kinyume cha sheria..

Vipi kuhusu Paulo?

Warumi 7:7-8,12

"Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.

Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.

Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema."

Sasa mkuu Unapata wapi Ujasiri wa kusema hauko chini ya sheria na unaishi ulimwengu wa sheria?
 
Ni kweli na ndivyo agano la kale lilivyokuwa yaani agano la sheria, ndio maana 'wayahudi' walijiita watu wa 'tohara' .

hata Kanisa la Mwanzo lilipitia mvutano huu kuhusu kuwakubali watu wasio wa tohara kuwa sehemu ya Kanisa.

Rejea kisa cha matendo ya mitume 11:2 pale Petro alipokwenda kwa Kornelio (asiye wa tohara) na wenzake kumnyooshea kidole, ila aliwaelezea kuhusu Yale maono na namna Roho Mtakatifu alivyowashukia wasio wa tohara.

Mtume Paulo kwenye waraka wake kwa Kanisa la Rumi (Warumi 2:25-29) alilieleza Kanisa la Rumi namna tohara ya kale ya mwilini ilivyo tofauti na ya agano jipya ambayo ni ya rohoni.

Warumi 2: 25
Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.

Warumi 2: 26
Basi ikiwa yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, je! Kutokutahiriwa kwake hakutahesabiwa kuwa kutahiriwa?

Warumi 2 :27
Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati?

Warumi 2 :28
Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;

Warumi 2 :29
bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.

Paulo alionyesha namna ndani ya agano jipya hatufungwi tena chini ya sheria za torati ya kale (ikiwemo tohara) na kwa kuthibitisha hilo hata Roho Mtakatifu aliwashukia nyumba ya Kornelio( wasio wa tohara).

Rabbon
Ktk Uzi huu, itoshe kusema,

No comment!!

Kwa kuwa Mungu anajibu maswali, mtoa mada aingie katika maombi aulize atajibiwa!!
 
Universe was not created.

If everything must have a creator even the creator must be created.

It's not a must universe has been created.
Kama Dunia hii ikisimama dakika mbili tu utaanza kujijambia 😀😀
 
Mi sitaki kusoma argument zako siku hizi maana Huwa zinanifikirisha sana
Sasa hutaki argument fikirishi?

Anyway, naheshimu uhuru wako wa kutotaka argument fikirishi.

Bora wewe umesema wazi. Kuna wengi hawataki kusoma argument, ila wanataka kubishana tu kwa kutetea timu yao.
 
Sasa hutaki argument fikirishi?

Anyway, naheshimu uhuru wako wa kutotaka argument fikirishi.

Bora wewe umesema wazi. Kuna wengi hawataki kusoma argument, ila wanataka kubishana tu kwa kutetea timu yao.
Kuna sehemu nyingine kutetea inakuwa ngumu,maana unakosa majibu unaanza kusema tu sio vizuri kuhoji....
Kuna mtu hapo juu kaelezea vile Zipora mke wa Musa ilimlazimu kumtahiri mwanae mdogo Kwa jiwe gumu,la sivyo angeuwawa,nimejisikia uchungu sana kama mzazi mwenye mtoto wa kiume....Ni kama alifanyiwa ukatili...ila sio vizuri kuhoji
 
Katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu inawezekana kuna pahala alisahau au kosea wakati wa uumbaji.

Nawaza kwa upande wa mwanadamu/mwanaume hivi ni kwa nini hakuumbwa/zaliwa akiwa tayari ameshakwisha tahiriwa?

Inawezekana huenda Mungu alisahau au kosea au mnasemaje?
Hata kama ni wewe, unawezaje kuuza soda ambayo haina kizibo (kisoda).

Govi ni kama kizibo (kisoda) fungua wewe kwa matumizi yako na sio kiwanda kuleta soda zikiwa hazina kizibo (kisoda).
 
Kuna sehemu nyingine kutetea inakuwa ngumu,maana unakosa majibu unaanza kusema tu sio vizuri kuhoji....
Kuna mtu hapo juu kaelezea vile Zipora mke wa Musa ilimlazimu kumtahiri mwanae mdogo Kwa jiwe gumu,la sivyo angeuwawa,nimejisikia uchungu sana kama mzazi mwenye mtoto wa kiume....Ni kama alifanyiwa ukatili...ila sio vizuri kuhoji

Dunia hii ina maumivu mengi, mateso mengi, maradhi mengi, umasikini mwingi. Hivibkweli jamani mnaamini kabisa Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote kaumba dunia iwe hivi? Mateso yote haya kwa mabilioni ya watu masikini, njaa, vifo, magonjwa, majanga ya matetemeko na ma tsunami yanaua na kuumiza watu kwa mafungu? Huyo Mungu si atakuwa mkatili sana kuumba ukimwengu wa hivyo?

Kuna binti mmoja mdogo wa Ufilipino alimuukiza Papa Francis, kwa nini Mungu ameachia watoto wadogo wajiuze kwenye umalaya ili kupata mahitaji yao? Kwa nini Mungu kaumba dunia ambayo jambo baya kama hili linaweza kutokea?

Papa Francis alishindwa kujibu jibu linaloeleweka akaishia kusema abracadabra za maisha ni fumbo na Mungu ana miujiza na yeye hajui jibu kamili.

Yani kimsingi ndiyo kulekule unakosema kukataza kuhoji

Swali la msingi alilotuachia mtoa mada sijui kama limejibiwa.

Kama kutahiriwa ni kitu muhimu na cha lazima hivyo, kwa nini Mungu hajatuumba tuzaliwe tumetahiriwa?
 
Mimi humuuliza na ananijibu.
Sijakuuliza kama wewe humuuliza na kama anakujibu.

Nimekuuliza unahakikishaje Mungu anakujibu?

Maana unaweza kuwa na matatizo ya akili tu ukajiona unamuuliza Mungu na Mungu anakujibu.

Kumbe hallucinatiins tupu.

Umejibu swali ambalo sijakuuliza, na swali nililokuuliza hujalijibu.

Unahakikishaje Mungu anakujibu?

Yani, unapofikiri Mungu anakujibu, unahakikishaje ni Mungu anakujibu na hakuna kingine chochote kinachotokea hapo?
 
Mkuu mtoa hoja, kwenye hiyo avatar ndo wewe huyo? [emoji23] Jumlisha hilo sweta sasa, sijui hali yako itakuwa vipi
 
Sijakuuliza kama wewe humuuliza na kama anakujibu.

Nimekuuliza unahakikishaje Mungu anakujibu?

Maana unaweza kuwa na matatizo ya akili tu ukajiona unamuuliza Mungu na Mungu anakujibu.

Kumbe hallucinatiins tupu.

Umejibu swali ambalo sijakuuliza, na swali nililokuuliza hujalijibu.

Unahakikishaje Mungu anakujibu?

Yani, unapofikiri Mungu anakujibu, unahakikishaje ni Mungu anakujibu na hakuna kingine chochote kinachotokea hapo?
Wewe ndo una shida pahala,

Umehakikishaje kuwa Mimi ndiye niliyejibu reply Yako?

Mungu ni baba yangu, naijua sauti yake anaponijibu.
 
Back
Top Bottom