Kwanini Mungu hana ratiba ya kuja kuongea na binadamu hapa duniani?

Kwanini Mungu hana ratiba ya kuja kuongea na binadamu hapa duniani?

Mbona wenzako wanaongea nae kila siku.na ukimfata kwako kwa kwa kutembea yeye atakuja kwa kukukimbilia. Acha bangi focus nae utampata. Kama unataka umhis huo uwezo wenzako pia watu wa Musa ( amani iwe juu yake) walijaribu
Wakaomba wanaomba wamuone, wakaambiwa watulie waone mlima ule na ile nuru tu ya utukufu wake ilipojionesha mlima wote ukasagika.
Focus utampata
 
[emoji23][emoji23][emoji23] ndugu sicheki kwa mazuri ila maisha yangu ya kuunga unga sina kazi wala ela inabidi nijichekee tu.. lazima shida zikikusonga sana vitu kama hivi unajiuliza maswali ambayo ungekuwa huna shida hujiulizi kwa sababu hayakupi changamoto
Me huwa nawaza hili MPENDE ADUI YAKO
hivi MUNGU ANAMPENDA SHETANI?
Maana tunaambiwa tupendane na upendo mzuri unaanzia mwanzo bila kuwa na kizuizi chochote
Ukimpenda mtu akakupenda hakutakuwa na adui. Hapo tunapoambiwa USIPOKUWA NA UPENDO WEWE SIO KITU KABISA.
vipi kuhusu hilo MUNGU ANAMPENDA SHETANI.
Haya maswali ukiwa huna ngori za maisha huwezi jiuliza kabisa
Kitabu cha ayubu wana wa Mungu walipojihudhurisha mbele zake na shetani nae alikuwa katikati yao. Akamuuliza umetoka wapi? Akasema kuzungukazunguka huko duniani. Ndio wakaanza kumdiscuss ayubu kisha akaanza kujaribiwa.

Je angekuwa hana Upendo usio Bagua au kupimika angeanzia wapi kuongea na muasi. Mwaribifu mwovu..? Msaliti na mkufuru??
 
Huenda mfumo wake wa existance/uwepo hauruhusu kuonana na mwanadamu. Mfano kuna yale madude yanatengeneza barabara ila ikikamilika hayawezi kupita sababu yataiharibu.

Nafsi yenye nguvu ya uumbaji mpaka wa jua na nyota ukikutana nayo kwa mwili huu na nyama utaweza kuhimili mionzi yake kweli?
 
Anajificha? Kwanini atafutwe wakati alisema yeye ni wa viumbe vyote?
Unajua wakati mwingine tuache kujipa umwamba wakati tuna udhaifu mkubwa. Bora kuchallange dini ila MUNGU ni kuachana naye tu. Sasa kama yupo, na ndiye aliyeumba jua, hilo jua tu kulitazama likiwa kali huwezi, sasa utamtazama vipi aliyeliumba? Au ndo mambo ya kutikiasa mbuyu MAKALIO YACHEZE?
 
Haha ili kupata jibu la swali lako, inabidi ujiulize unajuaje kama hata huyo Mungu yupo kweli.
 
Habarin guys,

Najiuliza ikiwa Rais ama viongozi wa duniani wanakuwa wanamuda wa kupitia kero za wananchi na hata kuongea nao na kuangalia sheria ambazo zimepitwa na wakati ila mungu hana huo muda kabisa.

Hii inadhihirisha binadamu ni werevu kuliko Mungu? Kama Mungu hana ratiba ya kuja hata baada ya miezi 6 au kila mwaka duniani anajuaje kero zetu?

Binadamu tumekuwa watu wa kubadilisha mambo kufanya maboresho ya changamoto za hapa duniani ila Mungu hana muda kabisa yeye amekaa kwenye kiti cha enzi anasubiri kuja kutuchoma hii ni wazi kuwa huyu jamaa hayupo kabisa mzazi unakosaje muda wa kuongea na watoto wako
Ukimwona MUNGU utakufa,,,,,,,,MUNGU yupo jamaa!!
 
Mungu amejihifadhi katika dhamiri za watu. Ukitaka kuongea naye huisha dhamiri yako na jitakase, tubu madhambi yako
 
Kumtuma Yesu ulikuwa mkwara tu uliosukwa na Wale Wayahudi wenye akili kuliko wote duniani. Angalia imani ilvyotapakaa duniani hasa ulimwengu wa tatu. Mimi siamini hasa kwenye "ufufuko" ni fix iliyokubuhu. Uzi wako umekaa vizuri ndio maana "atheists" wanapinga uwepo wa Mungu. Aitembelee Dunia siku Moja ili watu waamini.
Pinga pinga ni kipaji sawa na upumbavu, niamini mimi hata akija tena kama alivyokuja katika mwili (Yesu) bado tu mtamkataa kuwa si yeye Mungu Muumba mbingu na nchi.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Binadamu tunapenda kujipa umuhimu Sana.

Binadamu vile unavyoyachukulia magari, au vitu unavyovitengeneza na kumiliki ndivyo Mungu anavyokuchukulia.

Aongee nini na Mwanadamu,
Wachungaji na masheikhe ndio huwadanganya Watu na kuwapa binadamu umuhimu. Hali inayowafanya binadamu kuwa wabinafsi.

Imagine binadamu anakula wanyama wengine lakini yeye hataki kuliwa.
Binadamu hataki kuliwa nakati kila kukicha ardhi inawala na kubakia mifupa tupu kupitia kifo?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Unajua wakati mwingine tuache kujipa umwamba wakati tuna udhaifu mkubwa. Bora kuchallange dini ila MUNGU ni kuachana naye tu. Sasa kama yupo, na ndiye aliyeumba jua, hilo jua tu kulitazama likiwa kali huwezi, sasa utamtazama vipi aliyeliumba? Au ndo mambo ya kutikiasa mbuyu MAKALIO YACHEZE?
[emoji38]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom