Habarin guys,
Najiuliza ikiwa Rais ama viongozi wa duniani wanakuwa wana muda wa kupitia kero za wananchi na hata kuongea nao na kuangalia sheria ambazo zimepitwa na wakati ila Mungu hana huo muda kabisa.
Hii inadhihirisha binadamu ni werevu kuliko Mungu? Kama Mungu hana ratiba ya kuja hata baada ya miezi 6 au kila mwaka duniani anajuaje kero zetu?
Binadamu tumekuwa watu wa kubadilisha mambo, kufanya maboresho ya changamoto za hapa duniani ila Mungu hana muda kabisa yeye amekaa kwenye kiti cha enzi anasubiri kuja kutuchoma, hii ni wazi kuwa huyu jamaa hayupo kabisa. Mzazi unakosaje muda wa kuongea na watoto wako!
Aliongea na Adamu, alivoondoka kidogo tu wakala tunda, aliongea na Kaini ,angalia dogo alichomjibu:
Mwanzo 4:9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema,
Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.