Kwanini Mungu hana ratiba ya kuja kuongea na binadamu hapa duniani?

Kwanini Mungu hana ratiba ya kuja kuongea na binadamu hapa duniani?

Habarin guys,

Najiuliza ikiwa Rais ama viongozi wa duniani wanakuwa wana muda wa kupitia kero za wananchi na hata kuongea nao na kuangalia sheria ambazo zimepitwa na wakati ila Mungu hana huo muda kabisa.

Hii inadhihirisha binadamu ni werevu kuliko Mungu? Kama Mungu hana ratiba ya kuja hata baada ya miezi 6 au kila mwaka duniani anajuaje kero zetu?

Binadamu tumekuwa watu wa kubadilisha mambo, kufanya maboresho ya changamoto za hapa duniani ila Mungu hana muda kabisa yeye amekaa kwenye kiti cha enzi anasubiri kuja kutuchoma, hii ni wazi kuwa huyu jamaa hayupo kabisa. Mzazi unakosaje muda wa kuongea na watoto wako!
Tatizo ni pale unapomchukulia Mungu kwa kutumia akili za ki mtu.
God ni kitu kipana sana. Kama upo tayari kujifunza ninakupa summary fupi tu.

GOD = ENERGY

Kama utashindwa kuelewa nitatoa ufafanuzi zaidi.
 
Mbona anakuja Sana tu? Sema haji kwa umbile lake halisi kwamaana yeye ni roho, aliwahi kuja rasmi mara moja tu Kama Yesu .lakini anasema na sisi na kutoa maagizo kwa kutumia ndoto,maono nk kitabu Cha Ayubu kinasema ,,mungu husema na mtu kwa njia ya ndoto mara moja Kama hasikii husema nae Tena Kama hasikii hurudia Tena..ndio maana unaweza kuota ndoto inayo jirudia rudia. Kwa ndoto Mungu hutuonya au hutushauri mambo mengi Sana..lakini zaidi husema na sisi kupitia kitabu chake Biblia au humtuma malaika akaja kwa sura ya kawaida Kama mteja,mpitanjia au mtu ambaye humjui kabisa...over
 
Tumpende shetan

Shetani angekuwa ni mzur kwa kusikia alafu haonekani tungempenda tatizo ni mbaya tunavyosikia alafu haonekani ndio tatizo tunaogopa kumpenda
Na watu washajengewa picha shetan ni likitu la kutisha kama vle linagata ukiliona [emoji3063]
 
Inasemwa yeye anakufahamu hata kabla hujazaliwa, anafahamu kabla hujatenda na anafahamu mwisho wako. Nadhani inakua haina umuhimu tena kushuka kusikia.

Ila la kujiuliza kwa nini tunaendelea kupewa mahubiri, kulazimishwa kuwa ufanye mambo fulani ufikie ufalme wake. Ikiwa yeye anajua kuwa hata ushinde kwenye maombi wewe utakufa kwenye dhambi au umasikini.
Anataka uwe na chaguo yaani until na kumchagua yeye..ndio maana alimwambia Cain ajihadhari ili asifanye dhambi..
 
Alipojaribu kwa kumtuma Bwana Yesu mlimuua

Kutoka 33 : 20 Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.
nenda kwanza kaongee na rasi samia kwanza
 
Tatizo ni pale unapomchukulia Mungu kwa kutumia akili za ki mtu.
God ni kitu kipana sana. Kama upo tayari kujifunza ninakupa summary fupi tu.

GOD = ENERGY

Kama utashindwa kuelewa nitatoa ufafanuzi zaidi.
we blacks = gods and goddesses?
 
Back
Top Bottom