Mimi nadhani kuna kitu hakipo sawa kwenye hizi habari za Mungu na shetani.
Kwanza kabisa, iliwezekana vipi kwa shetani (malaika) kumsaliti Mungu? Ni kipi hasa kilichomsukuma shetani kumsaliti Mungu?
Pili, tunaambiwa THELUTHI MOJA ya malaika mbinguni walimuunga shetani mkono!! Yaani katika kila malaika 10, zaidi ya malaika watatu walikua upande wa shetani! Ni kipi hasa ambacho malaika walikerwa na utawala wa Mungu kiasi cha kufikia theluthi yao kuunga mkono upinzani?
Tatu, tunaambiwa shetani alikua na JESHI na kwamba jeshi hilo lilienda vitani kupigana na jeshi la malaika!
a) Ina maana wakati shetani ana organize jeshi lake, wanafanya mazoezi, wananunua silaha za maangamizi, wana plan attacks nk Mungu yeye alikua amekaa tu anawaangalia? Si yeye anaona kila kitu?
b) Vita kati ya malaika wa Mungu na wa shetani ilipiganwa vipi? Wakati hao wote ni roho na tunajua roho haziumii wala hazifi? Silaha gani zilitumika? Ushindi ulipatikanaje?
Nne, tunaambiwa katika vita hiyo, shetani na jeshi lake walichakazwa vibaya sana na kutupwa duniani. Lakini hata hivyo, shetani na Mungu waliendelea kushirikiana katika "projects" mbalimbali, huku wakikutana mara kwa mara kupiga soga, kupanga majaribu nk.
Huku tena tunaambiwa shetani alipotupwa duniani, akaja kuanza kukimbizana na mwanamke gani sijui.. mara mwanamke akapewa mabawa ili shetani asimkamate!! Yaani shetani huyuhuyu ambae ametoka kupigana na Mungu, eti akashindwa kumkamata yule mwanamke 😆😆 seriously?
Kuna baadhi ya vitu ukisoma kwenye hivi vitabu yani unaona kabisa ni alfu lela ulela.