Kwanini Mungu na Shetani wasimalize tofauti zao?

Kwanini Mungu na Shetani wasimalize tofauti zao?

Hii logic ilishakuwa debunked na hii statemnt.

"Who paint the painter?"

Sababu picha imechorwa haimaanishi mchoraji amechorwa.

Sababu binadamu Ametengenezwa haimaanishi Mungu nae Ametengenezwa, Simple Logic.
Sio kila kitu kinachorwa... wengine hawachorwi wala hawajawahi kuchorwa....

Ila kuamini kwamba hii dunia ni so complicated hadi kwamba lazima ilikuwa created na being fulani lazima pia uamini kwamba huyo individual being lazima atakuwa more complicated hence kama complication mean you must be created hence na yeye alikuwa created !!!

And why one creator and not multiple ?!!!!
 
Mfano Utabiri

-kwamba Mtume atawapiga waroma at that time mtume alikuwa na kigenge tu cha watu sembuse jeshi na Roma ni super power ambayo wanajeshi tu wapo in terms of Million. Mfano wake leo hii nitabiri wamakonde wataipiga Usa ina Mashiko right?
Unajua kitu kinaitwa motivation ?!!!! Hata Wayahudi walikuwa wanapigwa sana na warumi miaka nenda rudi na walikuwa na Imani zao kwamba kuna siku atakuja messiah kuwaokoa sasa utasemaje wamakonde watawapiga USA wakati hakuna connection ?!!! Ila mababu zetu walikuwa wanasema kila Siku Kibanga atampiga mkoloni na eventually all empires fall and probability shows wanaowapinga ndio watawaangusha....
-utabiri wa kwamba Mabedui watashindana kujenga Maghorofa marefu Duniani. Mfano wake leo nitabiri Wamasai watashinda kujenga maghorofa marefu duniani ina mashiko pia? Hawa mabedui kwa maelfu ya miaka wanachunga tu kondoo huko jangwani na Ngamia ila ghalfla tu within short time Burj Khalifa, Milad, princess, clock towers etc zote zipo huko.

Kuna tabiri kibao nyengine zinatajwa wazi wazi hakuna fumbo lolote
Mhhh ebu fafanua hapa na hizo ghorofa refu duniani wanajenga kwamba wenyewe ndio architects au zinajengwa kwao na hao Mabedui kwamba ndio mashindano yamekwisha ? Au kesho wakishindwa tutasema utabiri ulikuwa ni uongo....
Kuna matapeli huyu jamaa (Notradamus) aliitwa the Man who Saw Tommorrow Je na yeye alikuwa Mungu ?
 
Kama kawaida yenu enyi mliokufuru, kufanya kejeli dhidi ya waliomuamini Mungu. Hamna jambo jipya mtakuja kulifanya ambalo baba zenu waliowatangulia ktk kukufuru hawakulifanya. Huwa mnarudi yale yale ila karibu mtakuja jua. Mwanadamu umri wako ni mchache sana.
Sawa wewe unayemtisha na kumuona duni yeye mwenye mtizamo tofauti na wako huoni kwamba na wewe ni walewale tu, tukiwa na open mind hapa huenda akabadilika akawa kama wewe ukimuonyesha kile unachokiamini wewe kwa mtizamo wake (sio kwa kutumia katiba yako lakini kama the only proof) sababu Katiba yako (Kitabu chako) kwake hakifanyi kazi na hakiamini ukishaamini kitabu hicho basi wewe ni muumini unayehitaji uelewa zaidi
 
Ni mtu mjinga peke yake ndiye atakaesema kuwa kifo hakitishi.Kifo kinauma na kinatisha maana ni mwanzo wa maisha ya milele kwa maana hakuna tena kufa baada ya kufa ila matukio yajayo mbeleni ndio yanatisha. Je utakuwa miongoni mwa waliofaulu ama waliofeli??
If that was the case hakuna watu wangejiua ?!!!, Kuna saa na wakati kujiua ni shortcut yaani mpambano wa kitaa unakuwa mgumu zaidi....

Au hujasikia watu kwenye pain wanaomba wapewe sumu wafe!!!
 
Hakika hakuna haijuaye SIKU wa SAA.
Kunywa Thiodan hapo ya kutosha nina uhakika utajua kifo chako sio saa tu..., bali utakuwa accurate 100 percent in seconds na sio dakika...
 
Kujua kwamba kitu fulani kitatokea baadaye, haimaanishi kwamba umeamua au umeamuru kitu hicho kiwe hivyo. Hivyo ni vipengele viwili tofauti kabisa--independent variables.

Tulia na kutafakari, utaelewa.


I believe you do not know what you're talking about.
Mungu anajua kuwa mtu huyu atachagua "A"

Mpaka hapo "A" ishakuwa ni lazima

Kama "A" ishakuwa lazima maana yake huyo mtu hawezi kuchagua vinginevyo

Kama huyo mru hawezi kuchagua vinginevyo, basi hayuko huru.

Hivyo kila kitendo afanyacho, atafanya akiwa hana uhuru

Ili uhuru uwepo inatakiwa kuwa na multiple options ambazo ni possible

Since "A" haiwezi kuepukika maana yake iko fixed, choice kuwa fixed....hakuna uhuru
 
Mungu haui watu.
Bali anawachukua na kuwa weka katika hatua nyingine.
Okay anawachukuaje kwa magonjwa usiku wakilala au anashuka na kunyofoa roho zao anawachukuaje tafadhali nieleweshe....
Mi ugomvi wangu ni hii imani ambayo watu wenye dhambi wanawaua watu wengine wenye dhambi kwa kisingizio cha wamemkosea Mungu.
Kwahio hawa wanaowauwa nani anawachukua ni Mungu anayewapeleka katika hatua nyingine ? au hawa wanaowauwa ndio wanachukuliwa..., yaani kuua na kuchukuliwa kuna tofauti ?
Hakuna Binadamu ambaye hatendi dhambi ndio maana Mungu katoa fursa ya kutubu kwake na ameahidi kusamehe.
Ingawa hii Shetani hakupewa ?
Kuchinja binadamu mwenza kwa kisingizio cha dini ni vitendo vya kishirikina kabisa.

Mungua ashatoa amri USIUE.
Ila ukiua si anakufa na kama siku zake hazijafika wewe usingemuua nini kingemuua Covid ?
 
Shirki (ushirikina) ni miongoni mwa madhambi makubwa! Na ni dhambi kubwa kuliko madhambi yote unayoyajua wewe.Kuiba,kuua,kuzini,kusema uongo,kusengenya n.k hakufikii ukubwa wa hii dhambi.

Shirki (Ushirikina) ni kitendo cha kumuwekea Mungu washirika katika masuala yote ya Ibada.

Mfano ukiamini kuwa kuna kitu,mtu au jini anaweza kukupa wewe riziki kama/Pamoja au zaidi ya Mungu. Hapa unakuwa umemuwekea Mungu mshirika. Mfano unaumwa au una matatizo ila ukaenda kumuomba babu yako aliyezikwa miaka mingi iliyopita kaburini akusaidie kukuponya au kukutatulia matatizo yako ,hapa unakuwa umemfanya babu yako kuwa nae ni Mungu pamoja na Mungu.Hivyo umemfanyia Mungu kuwa ana mshirika.

Au ukaitakidi kuwa mizimu au miti (mibuyu) ukienda kuiomba ina uwezo wa kukutatulia matatizo yako hapa unakuwa umefanya ushirikina.

Au unamatatizo ukaensa kwa mganga akupigie ramli na kuwaomba majini wakusaidie kukutatulia matatizo yako ya biashara,kupata mali au watoto....hapa unakuwa umefanya shirki. Unakuwa ni Mshirikina.

Au nafsini kwako ukiwa na itikadi kuwa kuna Mungu zaidi ya mmoja kama walivyo wahindi na mabudha.Huo unakuwa ni ushirikina.

Ina maana kuwa umeshajitoa katika imani ya Mungu mmoja apasae kuabudiwa peke yake.

Mfano mzuri ni pale Unapokuwa na biashara kisha ukamuajiri mtu akuuzie bidhaa zako...yule mtu akauza vizuri kisha pesa yako yote akaichukua na kwenda kumpa mtu mwingine ambaye huna share nae katika umiliki wa biashara yako.Na ukimuuliza why kafanya hivyo ,anakujibu kuwa hakuna ubaya kumpa mtu mwingine pesa yako kwani ww na yule wote ni sawa!...

Je unaona ubaya wa hii kitu?? Ni wazi kuwa utachukizwa na jambo hilo na ikiwezekana unaweza hata kumuadhibu huyo mfanyakazi wako kwa tendo alilolifanya.

Hii ndio SHIRKI (ushirikina)


Ni mada pana sana.Ushirikina una matawi yake mengi tu. Ila kiufupi huo ndio uhalisia wa dhambi ya SHIRKI.

Iwapo mtu atakufa akiwa na dhambi hii pasi na kutubia kwa mola wake ajue kuwa MUNGU haisamehi kamwe na amemuharamishia pepo mtu ambae atakufa hali ya kuwa ni mshirikina.
Kwahio in Short dhambi kubwa kuliko zote kwa Imani yao ni wale wanaoamini Mungu Tofauti na unayemwamini wewe ?

Au sijakupata vema ?
 
Kwanini Shetani hawezi kusamehewa na kuokoka?

Kuna asili tatu tu...
Mungu, Malaika na Binadamu.
Mungu huwa hakosei lakini malaika na binadamu wanaweza kukosea.

Shetani kwa asili ni malaika, mwanzoni alikuwa malaika mwema, Lusifa "mbeba nuru", alikuwa na nafasi mbinguni, lakini uovu ukachipuka moyoni mwake, akawaza na akataka kuwa kama Mungu yaani naye aabudiwe (Isaya 14, Ezekiel 28), kimsingi, alitaka kufanya mapinduzi, Biblia katika Ufunuo 12:7-9 inasema, kukawa na vita mbinguni.
Kwahio Dhambi / Ouvu uliumbwa kabla ya Shetani ? , Nani aliumba huu Uovu ?
Malaika waliomuunga mkono Shetani wakapigwa pamoja na Shetani mwenyewe wakaangushwa hadi chini wakafukuzwa mbinguni, Yesu alimwona Shetani akianguka kama umeme. Baada ya hayo Lusifa akageuka kuwa mkuu wa giza yaani Shetani na malaika waliomuunga mkono wakageuka kuwa malaika waovu yaani majini.
Kwenye hii vita ya mbingu malaika walikuwa wanakufa au wanapigwa vipi ? yaani ushindi kwenye hii vita ulikuwaje unaumia / unatoka damu unakufa au ? yaani ushindi ulikuja vipi
Sasa, Shetani na majini, wote wana asili ya umalaika, hawawezi kusamehewa na kuokoka kwa sababu MUNGU ALIPOKUJA KUOKOA HAKUFANYIKA KUWA MALAIKA BALI ALIFANYIKA KUWA MWANADAMU. Mwandishi wa Waebrania anasema, Maana ni hakika, (Yesu) hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. Ebr 2:16 SUV
Okay sawa kwahio hata kama hatukujua kama mwanadamu atasamehewa basi huwezi kujua huenda Shetani huko mbeleni na yeye akapata msamaha ....
Kwahiyo, malaika akipotea, anapotea milele, Biblia inasema kuhusu hili kwamba, Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. Yud 1:6 SUV
Wakati anamuumba Binadamu nadhani walipangia furaha ya milele ila happenstance ya dhambi ikafanya wapewe adhabu kwahio huenda kuna happestances nyingine au kama mnavyosema huenda siku/ miaka kwenye bible haimaanishi siku au miaka yetu huenda milele sio milele
Habari Njema ni kwamba, damu iliyomwagika msalabani ilikuwa ya Mungu-mwanadamu, siyo Mungu-malaika, ndio maana ina uwezo wa kukuokoa mwanadamu, MWANADAMU UNAOKOLEWA KWA KUAMINI KUWA DAMU ILIYOMWAGIKA NI KWAAJILI YA KUSAMEHE DHAMBI ZAKO. Amini hilo sasa, na wewe uliyeamini tayari usifanye dhambi makusudi maana yake unakuwa unaikanyaga damu ya agano na kumfanyia jeuri Roho wa neema.

Mambo haya niliyosema, yaani mambo ya wokovu, hata malaika wanatamani kuyaishi, wokovu ni mtamu mnooo unawatamanisha hata malaika. Kama Biblia isemavyo;

.... mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiria ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Hata malaika wanatamani kuyafahamu mambo haya.
1 Petro 1:12 NEN

Oscar Wissa
Anyway asante kwa kujaribu kuelezea sababu according to Imani yako ila Shetani kutokupewa msamaha wakati na yeye anakosea kama Binadamu inaondosha ile Justice ambayo The Almighty tunajua kwamba anayo
 
You're making a grave mistake kwa kudhani kwamba utashi wa mwanadamu umeumbwa mithili ya utendaji wa saa ama mashine ama roboti. Uelewa wako wa free will ni duni sana.

Twende pole pole....

aliyepanga all the moving parts yaani kama umetengeneza saa

Kama tungeumbwa mfano wa robots, hakuna dhambi ambayo ingetokea kwa malaika wala mwanadamu, kwa sababu hakuna ambaye miongoni mwao angekuwa na uhuru wa kufanya kadiri ya misukumo ya fikra zake.

huwezi kusema mshale mkubwa una free will ya kusogea au hapana

Kwa hiyo tambua kwamba uwepo wa dhambi duniani ni ushahidi mkubwa beyond reasonable doubt kwamba mwanadamu ni free will living being.

Sasa swali Mungu ni mtengenezaji wa hatua zote hizo au ni mtazamaji na anajua kutokana na hizo movement kama mimi na wewe tunavyojua kutokana na the actual design?!!!!

kwahio my destiny was determined by your design.....
 
watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa
Huenda Babu zako wakasema kile tulichopigania na kufa ili tubaki na Imani zetu hawa waliokuja kututawala sasa hivi wanafanya kwa urahisi sana (kwahio our fight was wasted)

Sio Busara kuona mtizamo wa mwingine ni inferior kuliko wako tena ukizingatia ni Imani na sio factual things
 
Huenda Babu zako wakasema kile tulichopigania na kufa ili tubaki na Imani zetu hawa waliokuja kututawala sasa hivi wanafanya kwa urahisi sana (kwahio our fight was wasted)

Sio Busara kuona mtizamo wa mwingine ni inferior kuliko wako tena ukizingatia ni Imani na sio factual things
Tulia mkuu wacha wenge
 
Mungu anajua kuwa mtu huyu atachagua "A"

Mpaka hapo "A" ishakuwa ni lazima

Kama "A" ishakuwa lazima maana yake huyo mtu hawezi kuchagua vinginevyo

Kama huyo mru hawezi kuchagua vinginevyo, basi hayuko huru.

Hivyo kila kitendo afanyacho, atafanya akiwa hana uhuru

Ili uhuru uwepo inatakiwa kuwa na multiple options ambazo ni possible

Since "A" haiwezi kuepukika maana yake iko fixed, choice kuwa fixed....hakuna uhuru

Hakuna uhusiano wowote kati ya KUJUA kwa Mungu na MAAMUZI ambayo mtu fulani ataweza kuyafanya baadaye. Hizi ni variables mbili zisizotegemeana (independent variables).

Mungu ana uwezo wa kusafiri kwenda mbele kiwakati na kuona mapema jinsi watu watakavyofanya maamuzi yao kwa utashi wao binafsi na kushuhudia matendo yao ya baadaye.

Matendo hayo hayatokani na Mungu per se, bali ni yaleyale kadiri ya utashi na maamuzi ya mwanadamu aliyeumba kwa uhuru wa kuchagua apendavyo.

God can see the future and the past events just as clearly as if they were happening at the present moment, right now before His very eyes. He has the ability to travel ahead in time, just as He can travel back into the past. As a matter of fact, He doesn't have to travel, for everything past, present and future is spread open before Him. His ability is not limited by space or time.

Again, the foreknowledge of God doesn't' translate into His predestination ama predetermination.
 
You're making a grave mistake kwa kudhani kwamba utashi wa mwanadamu umeumbwa mithili ya utendaji wa saa ama mashine ama roboti. Uelewa wako wa free will ni duni sana.
Kwahio kwa mfano wangu huo hapo juu conclusion yako ni kwamba nimefananisha saa / mashine na mtu ?

Hayo ya kuumbwa ni another argument altogether ambayo sitaki kuingia sababu hio ni Imani yako
Kama tungeumbwa mfano wa robots, hakuna dhambi ambayo ingetokea kwa malaika wala mwanadamu, kwa sababu hakuna ambaye miongoni mwao angekuwa na uhuru wa kufanya kadiri ya misukumo ya fikra zake.
Again tarudia mfano wangu wa saa kivingine..., Kwamba mshale mkubwa unafanya vile kwa kutegemea gears na connections za mishale mingine..., Kwahio kama Mungu aliumba mtu A na B na kumuekea coding zote na anajua kabisa mtu A atafanya nini hii ni Pre-written hata kabla hajazaliwa sasa huyu mtu A akataka kuua watoto wa mtu B iliyosababisha mtu B kutenda dhambi ya kumuua (usiue) mtu A ili asiue watoto wake..., unaweza kusema vipi Aliyetengeneza hawa hawa hausiki kwenye haya matukio ?

B kwenye free will huwezi kusema mtu kapewa chaguo la kuchagua either shetani au Mungu wakati anaambiwa akichagua shetani atachomwa milele na akichagua mungu ataishi milele kwa raha mustarehe (hio ni intimidation) na chaguo hilo ni la kushinikizwa....

Sasa kama wewe kwenye mfano wangu wa kukwambia kwamba ukifananisha mtabiri ambaye sio aliyetengeneza mvua radi na jua..., na Mungu ambaye ametengeneza hivyo vitu ni tofauti umetoa conclusion kwamba nafananisha binadamu na saa all I can say ni kwamba huenda tukakesha hapa....
Kwa hiyo tambua kwamba uwepo wa dhambi duniani ni ushahidi mkubwa beyond reasonable doubt kwamba mwanadamu ni free will living being.
And How is That......., Kwamba chagua dhambi nikuchome, au nichague mimi nisikuchome !!!!, Pili katika chaguzi zako nimeweka vikwazo ambavyo vitapelekea ugumu wa kunichagua ?
 
Wewe hujui kitu kuhusu maandiko!! Naona umenukuu andiko kutoka ktk kumbukumbu la torati ila nikikupa maandiko yahusuyo sheria kwenye biblia yako utageuka na kuyakataa kwamba yamepitwa na wakati.
Maandiko yana wakati, Yaani Expiry Date ?

Haya ya sasa yata-expire lini ?
 
Shetani hana toba ndani yake! Huo msamiati hana kwa hiyo hakuna namna anayoweza kusamehewa! Kanuni ya kusamehewa inadai uombe msamaha na ukubali kuacha uovu jumla! Shetani hawezi kusamehewa si kwa sababu Mungu hataki kumsamehe bali kwa sababu hawezi kufuata kanuni ya kupokea msamaha na Mungu anafanya kazi kwa kanuni!!

Ndio maana japo Mungu anawapenda watu wote bila upendeleo kuna ambao wamesamehewa dhambi zao na wengine bado!! Waliosamehewa walifuata kanuni ya kusamehewa dhambi kwa njia ya toba na imani kwa Yesu Kristo!! Je wewe umemwamini Yesu ili uokolewe? Yesu ndiye Njia, Kweli na Uzima!!
Kwahio huenda baada ya kuchomwa moto kwa karne kadhaa ataomba msamaha na all will be well ?, Au huo moto unavumilika ? Yaani kusema naomba unisamehe ni vigumu kuliko kuvumilia moto?
 
Back
Top Bottom